Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukmu Ya Kutawassal Kwa Aliyehai Na Aliyefariki
Hukmu Ya Kutawassal Kwa Aliyehai Na Aliyefariki
Imaam Ibn Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
“Basi hii (kutawassal kwa aliyehai) ni tawassul inayojuzu nayo ni kumuomba mtu unayetaraji kutakabaliwa kwake amuombee kwa Allaah Ta’aalaa, lakini ambalo linalopasa ni kwamba muulizaji anakusudia hayo yamfanye yeye nafsi yake na yamfae pia nduguye ambaye anamuomba amuombeee na si kukusudia kujinufaisha yeye pekee kwa sababu unapotaka kumnufuisha nduguyo na kujinufaisha nafsi yako huwa ni kumfanyia ihsaan. Basi mtu anapomuombea nduguye du’aa kwa siri Malaika husema: “Aamiyn nawe upate mfano wake.” Kwa hiyo naye huwa katika wafanyao ihsaan kwa du’aa hii, na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.” [Fataawaa Imaam Ibn ‘Uthaymiyn, Hukmu At-Tawassul]