Shaykh Fawzaan: Sunnah Khatwiyb Kuwaombea Waislamu Lakini Haijuzu Maamuma Kunyanyua Mikono Na Kuitikia “Aamiyn” Kwa Sauti
Sunnah Khatwiyb Kuwaombea Waislamu Lakini Haijuzu Maamuma Kunyanyua Mikono Na Kuitikia “Aamiyn” Kwa Sauti
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:
“Ni Sunnah kwa Khatwiyb kuwaombea Waislamu kwa yenye kutengeneza Dini na dunia yao, kumuombea Imaam wa Waislamu na viongozi wao kwa mambo yao kwa islahi na tawfiki.
Du’aa kwa viongozi katika khutbah ni maarufu kwa Waislamu na juu yake 'amali zao, kwani du’aa kwa viongozi hao ni katika Manhaj ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa‘ah na kuacha kwake ni katika Manhaj ya wazushi.
Haifai kwa Maamuma kuitikia Aamiyn kwa du’aa ya Khatwiyb kwa kunyanyua sauti wala mikono yake kwani kufanya hivyo ni haramu kwa itifaki ya Wanachuoni.”
[Al-Mulakhkhasw Al-Fiqhiy, Mj. 1, uk. 255, 264].