11-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Kuazima

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلْعَارِيَةِ

11-Mlango Wa Kuazima[1]

 

 

 

 

 

751.

عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {عَلَى اَلْيَدِ مَا أَخَذَتْ حَتَّى تُؤَدِّيَهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ 

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ni wajibu wa mkono kwa ulichokichukua hadi ukirudishe.”[2] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

752.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَدِّ اَلْأَمَانَةَ إِلَى مَنْ اِئْتَمَنَكَ، وَلَا تَخُنْ مَنْ خَانَكَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَاسْتَنْكَرَهُ أَبُو حَاتِمٍ اَلرَّازِيُّ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tekeleza amana kwa aliyekuamini, wala usimkhini aliyekukhini.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy na amesema ni Hassan, na akaisahihisha Al-Haakim, na ameona ni Munkar (Hadiyth iliokataliwa) Abuu Haatim Ar-Raaziyy]

 

 

 

753.

وَعَنْ يَعْلَى بْنِ أُمَيَّةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِذَا أَتَتْكَ رُسُلِي فَأَعْطِهِمْ ثَلَاثِينَ دِرْعاً "، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! أَعَارِيَةٌ مَضْمُونَةٌ أَوْ عَارِيَةٌ مُؤَدَّاةٌ ؟ قَالَ: بَلْ عَارِيَةٌ مُؤَدَّاةٌ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

 Kutoka kwa Ya’laa bin Umayyah[3] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Utakapojiwa na wajumbe wangu, wape deraya (nguo za kivita) thelathini. Nikasema Ee Rasuli wa Allaah! Ni za kuazima zilizodhaminiwa[4] ama ni za kuazima na kurudisha kama kawaida? Akasema: Ni za kuazima na kurudishwa kama kawaida.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

754.

وَعَنْ صَفْوَانَ بْنِ أُمَيَّةَ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  اِسْتَعَارَ مِنْهُ دُرُوعاً يَوْمَ حُنَيْنٍ. فَقَالَ: أَغَصْبٌ يَا مُحَمَّدُ ؟ قَالَ: بَلْ عَارِيَةٌ مَضْمُونَةٌ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ  .

وَأَخْرَجَ لَهُ شَاهِدًا ضَعِيفًا عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ  

 

Kutoka kwa Swafwaan bin Umayyah[5] amesema  kuwa: “Nabiy  (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliazima kwake deraya siku ya vita vya Hunayn, akasema: Je unaninyang’anya ee  Muhammad? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Bali ni kuazima kwa dhamana.”[6] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]

Na akaishuhudisha kwa Hadiyth dhaifu kutoka kwa Ibn ‘Abbaas

 

 

 

755.

عَنْ سَعِيدِ بْنِ زَيْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنْ اِقْتَطَعَ شِبْرًا مِنْ اَلْأَرْضِ ظُلْماً طَوَّقَهُ اَللَّهُ إِيَّاهُ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ مِنْ سَبْعِ أَرَضِينَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Sa’iyd bin Zayd[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kukata shubiri moja ya ardhi kwa dhulma, Allaah atamvisha shingoni mwake siku ya Qiyaamah ardhi saba.”[8] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

[1] Katika lugha ya kiarabu مَضْمُونَةٌ اَلْعَارِيَةِ (Al-‘aariyah Madhwmuwnah) ni mkopo uliodhaminiwa na عَارِيَةٌ مُؤَدَّاةٌ (‘Aariyah Muaddah) ni kilichoazimwa (kisicho na dhamana). Kuhusu ya mwanzo ni kuwa dhamana ni muhimu. Jaalia mtu anachukua mkopo wenye dhamana na kilichoazimwa kikaharibika ikiwa kwa aliyekiazima, kilichokubaliwa ni kuwa muazimaji atalipa thamani yake, na ndio maana ikaitwa ‘Aariyah Madhwmuwnah. Hata hivyo ikiwa mtu ataazima kwa kuaminiwa kama ilivyo ‘Aariyah Muaddah (kisichokuwa na dhamana) na kitu chenyewe kikaharibika kwa aliyekiazima (bila uzembe kutoka kwake) hatotakiwa kulipa.

 

[2] Umetajwa “mkono” lakini makusudio ni mtu. Yaani aliyeazima kitu anawajibika kukirudisha alichokichukua hata kama ni kwa gharama. Hadiyth hii ni dalili kuwa ni wajibu mtu kurudisha mali ya mwenyewe ima kama aliazimia au kwa njia nyingine.

 

[3] Huyu ni Ya’laa bin Umayyah bin Abiy ‘Ubaydah At-Tamiym. Mama yake anaitwa Mun-yah, kwa hivyo huitwa Ibn Mun-yah. Ni Swahaba mashuhuri, alifariki baada ya mwaka wa 40 Hijriyyah.

 

[4] Vilivyoazimwa kwa dhamana uharibifu wake utalipwa na mwenye kuazima. Kuazima ni kumruhusu mtu kutumia mali ya mwingine, au faida ya kitu kile, na baada ya kutumia kukirejesha kwa mwenyewe. Lakini katika viazimwavyo ni vitu, hakuna mtu kuazima mkewe. Pia haifai mtu kuazima kitu ili akitumie katika kufanyia kitu cha haraam.

 

[5] Huyu ni Swafwaan bin Umayyah bin Khalaf bin Wahb Al-Qurayshiy Al-Jumahi Al-Makkiy, ni Swahaba alikuwa miongoni mwa watukufu wa ki Quraysh. Alikimbia siku ya Fat-hi Makkah (Ukombozi wa Makkah), akapewa Amani, akarudi. Alihudhuria pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) vita vya Hunayn na vita vya Twaaif akiwa ni kafiri, kisha akasilimu, na akawa Muislam bora. Alifariki siku za mauaji ya ‘Uthmaan

 

[6] Ikiwa mtu ameazima kitu na kikaharibika kwa bahati mbaya, muazimaji hatogharamia kwa hilo, lakini ikithibitika kuwa uharibifu huo ni wa makusudi au ni matokeo ya uzembe wake basi atatakiwa kulipa.

 

[7] Jina lake ni Sa’iyd bin Zayd bin ‘Amr bin Nufayl bin ‘Abdul ‘Uzza bin Riyaah Al-Qurayshi Al-‘Adawi na ukoo wake unakutana na ule wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa Ka’b bin Luay. Ni mmojawapo katika waliobashiriwa Jannah, ‘Umar bin Al-Katwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa ami yake upande wa kuumeni, kwa sababu ‘Amr bin Nufayl babake Sa’iyd na Al-Khatwaab bin Nufayl babake ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) walikuwa ndugu. Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa mume wa Faatwimah dada yake ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), alikua chachu iliyomsaidia kumsilimisha ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na dada yake Sa’iyd ‘Atikah alikuwa mke wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alijulikana kwa jina Sa’iyd kabla ya kuja kwa Uislam na baada ya kusilimu. Sa’iyd alikuwa katika Muhajirina wa mwanzo.

 

[8] Hii ina maana ya kupora ardhi ya mtu ni katika madhambi makubwa. Kupora ardhi ya mtu maana yake ni kuichukuwa na kuanza kuilima.

Share