00-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Jeneza

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْجَنَائِزِ

00-Kitabu Cha Jeneza

 

 

 

 

425.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{أَكْثِرُوا ذِكْرَ هَاذِمِ‏ اَللَّذَّاتِ: اَلْمَوْتِ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Zidisheni kukumbuka kikatisha ladha, yaani kifo.”[1] [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

426.

وَعَنْ أَنَسٍ‏ رضى الله عنه‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{لَا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُكُمُ اَلْمَوْتَ لِضُرٍّ يَنْزِلُ بِهِ، فَإِنْ كَانَ لَا بُدَّ مُتَمَنِّيًا فَلْيَقُلْ: اَللَّهُمَّ أَحْيِنِي مَا كَانَتِ اَلْحَيَاةُ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَتِ اَلْوَفَاةُ خَيْرًا لِي} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Asitamani mmoja wenu mauti[2] kwa sababu ya kufikwa na madhara, ikiwa hana budi kutamani, basi aseme:

اَللَّهُمَّ أَحْيِنِي مَا كَانَتِ اَلْحَيَاةُ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَتِ اَلْوَفَاةُ خَيْرًا لِي

Ee Allaah! Nipe uhai, ikiwa uhai ni kheri kwangu, na Unifishe ikiwa mauti hayo ni kheri kwangu.”[3] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

 427.

وَعَنْ بُرَيْدَةَ ‏ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {اَلْمُؤْمِنُ يَمُوتُ بِعَرَقِ الْجَبِينِ} رَوَاهُ اَلثَّلَاثَةُ‏ وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Buraydah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muumini hufa na jasho[4] katika paji la uso wake.” [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

428.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ وَأَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَا: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{لَقِّنُوا مَوْتَاكُمْ‏ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ، وَالْأَرْبَعَةُ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd na Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) wamesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watamkieni wafu wenu “Laa Ilaaha Illa Allaah” (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah).” [Imetolewa na Muslim na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]

 

 

 

429.

وَعَنْ مَعْقِلِ بْنِ يَسَارٍ رضى الله عنه ‏ أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {اقْرَؤُوا عَلَى مَوْتَاكُمْ يس} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Ma’qil bin Yasaar[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wasomeni wafu wenu Suwrah Yaasiyn.”[6] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

430.

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {دَخَلَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏عَلَى أَبِي سَلَمَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ وَقَدْ شُقَّ بَصَرُهُ‏ فَأَغْمَضَهُ، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّ اَلرُّوحَ إِذَا قُبِضَ، اتَّبَعَهُ الْبَصَرُ" فَضَجَّ نَاسٌ مِنْ أَهْلِهِ، فَقَالَ: "لَا تَدْعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ إِلَّا بِخَيْرٍ.‏ فَإِنَّ اَلْمَلَائِكَةَ تُؤَمِّنُ عَلَى مَا تَقُولُونَ".‏ ثُمَّ قَالَ: "اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِأَبِي سَلَمَةَ، وَارْفَعْ دَرَجَتَهُ فِي اَلْمَهْدِيِّينَ، وَافْسِحْ لَهُ فِي قَبْرِهِ، وَنَوِّرْ لَهُ فِيهِ، وَاخْلُفْهُ فِي عَقِبِهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliingia kwa Abuu Salamah[7] alipofariki huku macho yake yakingali wazi, akayafumba na akasema: “Hakika roho inapochukuliwa, jicho huifuata.”[8] Baadhi ya ahli wake wakalia na kupiga mayowe, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Msijiombee du’aa yoyote isipokuwa kheri, kwani Malaika huitikia Aamiyn kwa mnayoyasema.” Kisha akasema: “Ee Allaah! Mghufirie Abuu Salamah dhambi zake, pandisha daraja yake miongoni mwa walioongoka, mkunjulie katika kaburi lake, na mpe nuru ndani yake, na mpe warithi katika vizazi vyake vilivyobakia.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

431.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا: {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ‏ صلى الله عليه وسلم ‏حِينَ تُوُفِّيَ سُجِّيَ بِبُرْدٍ حِبَرَةٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki, alifunikwa na nguo iliyokuwa na mistari.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

432.

وَعَنْهَا {أَنَّ أَبَا بَكْرٍ اَلصِّدِّيقَ‏ رضى الله عنه‏ قَبَّلَ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بَعْدَ مَوْتِهِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena kuwa: “Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimbusu[9] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

 433.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {نَفْسُ اَلْمُؤْمِنِ مُعَلَّقَةٌ بِدَيْنِهِ، حَتَّى يُقْضَى عَنْهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Roho ya Muumini imeunganishwa na deni[10] mpaka alipiwe.”[11] [Imetolewa na Ahmad na At-Tirmidhiy, na waliipa daraja la Hasan]

 

 

 

434.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ فِي اَلَّذِي سَقَطَ عَنْ رَاحِلَتِهِ فَمَاتَ: {اغْسِلُوهُ بِمَاءٍ وَسِدْرٍ، وَكَفِّنُوهُ فِي ثَوْبَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu mtu aliyeanguka kutoka juu ya mnyama wake na akafariki: “Muosheni kwa maji na mkunazi[12] na mumvishe sanda[13] ya nguo zake mbili.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

 435.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {لَمَّا أَرَادُوا غَسْلَ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالُوا: وَاَللَّهُ مَا نَدْرِي، نُجَرِّدُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏كَمَا نُجَرِّدُ مَوْتَانَا، أَمْ لَا ؟….‏.‏} اَلْحَدِيثَ، رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Watu walipotaka kumuosha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) walisema: “Wa-Allaahi hatujui kama tumvue nguo zote Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kama tunavyo wavua nguo wafu wetu.”[14] [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd]

 

 

 

436.

وَعَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {دَخَلَ عَلَيْنَا اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏وَنَحْنُ نُغَسِّلُ ابْنَتَهُ، فَقَالَ: "اغْسِلْنَهَا ثَلَاثًا، أَوْ خَمْسًا، أَوْ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، إِنْ رَأَيْتُنَّ ذَلِكَ، بِمَاءٍ وَسِدْرٍ، وَاجْعَلْنَ فِي الْآخِرَةِ كَافُورًا، أَوْ شَيْئًا مِنْ كَافُورٍ"، فَلَمَّا فَرَغْنَا آذَنَّاهُ، فَأَلْقَى إِلَيْنَا حِقْوَهُ.‏فَقَالَ: "أَشْعِرْنَهَا إِيَّاهُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ: {ابْدَأْنَ بِمَيَامِنِهَا وَمَوَاضِعِ اَلْوُضُوءِ مِنْهَا}

وَفِي لَفْظٍ للْبُخَارِيِّ: {فَضَفَّرْنَا شَعْرَهَا ثَلَاثَةَ قُرُونٍ، فَأَلْقَيْنَاهُ خَلْفَهَا}

Kutoka kwa Ummu ‘Atwiyyah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliingia tukiwa tunamuosha binti yake, akasema: “Muosheni kwa maji na mkunazi mara tatu au tano[15] au zaidi ya hivyo mkiona inafaa, na katika mara ya mwisho mtieni kaafuwraa au sehemu ya kaafuwraa.” Tulipomaliza tukamuarifu naye akatutupia kikoi chake, akasema: “Mzungushieni nalo hilo mwilini mwake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah nyengine: “Anzeni na kuliani kwake na sehemu za kutawadhwa.”

 

Na katika tamshi la Al-Bukhaariy: “Tulisuka nywele zake mikia mitatu na tukaiweka nyuma ya mgongo wake.”

 

 

 

437.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كُفِّنَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فِي ثَلَاثَةِ أَثْوَابٍ بِيضٍ سَحُولِيَّةٍ مِنْ كُرْسُفٍ، لَيْسَ فِيهَا قَمِيصٌ وَلَا عِمَامَةٌ.} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikafiniwa kwa mavazi matatu meupe ya kitambaa cha Sahuwliyyah[16] ambazo miongoni mwake hamkuweko kanzu wala kilemba.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

438.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ ‏رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا‏ قَالَ: {لَمَّا تُوُفِّيَ عَبْدُ اَللَّهِ بْنِ أُبَيٍّ جَاءٍ اِبْنُهُ إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏.‏ فَقَالَ: أَعْطِنِي قَمِيصَكَ أُكَفِّنْهُ فِيهِ، فَأَعْطَاهُ إِيَّاهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Alipofariki ‘Abdullaah bin Ubayy[17] mwanawe[18] alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akasema: Nipe kanzu yako nikamkafinie nayo, akampa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

439.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {الْبَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ الْبَيَاضَ، فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Vaeni nguo zenu nyeupe kwani ni miongoni mwa nguo zenu nzuri zaidi, na muwakafinieni wafu wenu.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

440.

وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{إِذَا كَفَّنَ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ فَلْيُحْسِنْ كَفَنَهُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akimkafini nduguye sharti amkafini kwa sanda nzuri.”[19] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

441.

وَعَنْهُ قَالَ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَجْمَعُ بَيْنَ اَلرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحَدٍ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ، ثُمَّ يَقُولُ: "أَيُّهُمْ أَكْثَرُ أَخْذًا لِلْقُرْآنِ ؟"، فَيُقَدِّمُهُ فِي اَللَّحْدِ، وَلَمْ يُغَسَّلُوا، وَلَمْ يُصَلِّ عَلَيْهِمْ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akikusanya baina ya watu wawili waliouawa Uhud katika nguo moja,[20] halafu akasema: “Nani kati yao alijua Qur-aan zaidi?” Kisha akamtanguliza kwenye mwanandani, hawakuoshwa wala hawakuswaliwa.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

442.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {سَمِعْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏يَقُولُ: "لَا تُغَالُوا فِي اَلْكَفَنِ، فَإِنَّهُ يُسْلُبُ سَرِيعًا"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: Msifanye israafu katika sanda, kwani itaoza haraka.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

443.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا ، أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ لَهَا: {لَوْ مُتِّ قَبْلِي فَغَسَّلْتُكِ} اَلْحَدِيثَ.‏ رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia: “Endapo utafariki kabla yangu, Mimi nitakuosha.”[21] [Imetolewa na Ahmad na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

444.

وَعَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ عُمَيْسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا: {أَنَّ فَاطِمَةَ عَلَيْهَا اَلسَّلَامُ أَوْصَتْ أَنْ يُغَسِّلَهَا عَلِيٌّ رَضِيَ اَللَّهُ تَعَالَى عَنْهُ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ

Kutoka kwa Asmaa bint ‘Umays (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Faatwimah[22] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) aliusia kuwa ‘Aliy[23] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ndiye amuoshe yeye (endapo atafariki kabla yake).” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy]

 

 

 

 445.

وَعَنْ بُرَيْدَةَ رضى الله عنه ‏فِي قِصَّةِ الْغَامِدِيَّةِ اَلَّتِي أَمَرَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏بِرَجْمِهَا فِي اَلزِّنَا‏ قَالَ: {ثُمَّ أَمَرَ بِهَا فَصُلِّيَ عَلَيْهَا وَدُفِنَتْ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Buraydah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia habari ya mwanamke wa Ghaamid ambaye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha apigwe mawe kwa sababu ya zinaa. Akasema: “Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha aswaliwe[24] na akazikwa.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

446.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {أُتِيَ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بِرَجُلٍ قَتَلَ نَفْسَهُ بِمَشَاقِصَ، فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيْهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Maiti ya mtu aliyejiua kwa mshale wenye kichwa butu ililetwa mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), hakumswalia.”[25] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

447.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه ‏فِي قِصَّةِ اَلْمَرْأَةِ اَلَّتِي كَانَتْ تَقُمُّ اَلْمَسْجِدَ‏ قَالَ: {فَسَأَلَ عَنْهَا اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا: مَاتَتْ، فَقَالَ: "أَفَلَا كُنْتُمْ آذَنْتُمُونِي" ؟ فَكَأَنَّهُمْ صَغَّرُوا أَمْرَهَا‏ فَقَالَ: "دُلُّونِي عَلَى قَبْرِهَا"، فَدَلُّوهُ، فَصَلَّى عَلَيْهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ‏ .‏

وَزَادَ مُسْلِمٌ، ثُمَّ قَالَ: {إِنَّ هَذِهِ اَلْقُبُورَ مَمْلُوءَةٌ ظُلْمَةً عَلَى أَهْلِهَا، وَإِنَّ اَللَّهَ يُنَوِّرُهَا لَهُمْ بِصَلَاتِي عَلَيْهِمْ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu mwanamke aliyekuwa akifagia Msikiti: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliuliza khabari zake. Maswahaba wakamuambia amefariki. Akasema: “Kwa nini hamkuniarifu?” Ikaonekana kana kwamba waliona jambo lake ni dogo. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Nijulisheni kaburi lake.” Wakamjulisha na akamswalia.”[26] [Al-Bukhaariy, Muslim]

Naye Muslim aliongezea: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Makaburi haya yamejaa giza kwa waliomo humo. Allaah Atayatia nuru kwa Swalaah yangu niliyowaswalia.”

 

 

 

448.

وَعَنْ حُذَيْفَةَ رضى الله عنه‏ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ‏ صلى الله عليه وسلم ‏كَانَ يَنْهَى عَنِ اَلنَّعْيِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ

Kutoka kwa Hudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akikataza kutangaza[27] vifo.” [Imetolewa na Ahmad na At-Tirmidhiy, aliyeipa daraja la Hasan]

 

 

 

449.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ‏ رضى الله عنه‏ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏نَعَى اَلنَّجَاشِيَّ فِي اَلْيَوْمِ اَلَّذِي مَاتَ فِيهِ، وَخَرَجَ بِهِمْ مِنَ الْمُصَلَّى، فَصَفَّ بِهِمْ، وَكَبَّرَ عَلَيْهِ أَرْبَعًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitangaza kifo cha An-Najaashiy[28] siku alipofariki, akatoka na watu hadi kwenye Muswalla (uwanja wa kuswalia), akawapanga katika safu, na akapiga Takbiyr mara nne.”[29] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

450.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: سَمِعْتُ اَلنَّبِيَّ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَقُولُ: {مَا مِنْ رَجُلٍ مُسْلِمٍ يَمُوتُ، فَيَقُومُ عَلَى جَنَازَتِهِ أَرْبَعُونَ رَجُلًا، لَا يُشْرِكُونَ بِاَللَّهِ شَيْئًا، إِلَّا شَفَّعَهُمْ اَللَّهُ فِيهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nimemsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Muislamu yeyote anapofariki na wakasimama watu arubaini wasio mshirikisha Allaah na chochote wakamswalia, Allaah Atawakubali wawe waombezi[30] wake.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

451.

وَعَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رضى الله عنه‏ قَالَ: {صَلَّيْتُ وَرَاءَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ‏عَلَى امْرَأَةٍ مَاتَتْ فِي نِفَاسِهَا، فَقَامَ وَسْطَهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Niliswali nyuma ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kumswalia mwanamke aliyefariki baada ya uzazi. Alisimama katikati ya mwili wake.”[31] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

452.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {وَاَللَّهِ لَقَدْ صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏عَلَى اِبْنَيْ بَيْضَاءَ فِي اَلْمَسْجِدِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalia maiti wa wana wawili wa Baydhwaa[32] Msikitini.”[33] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

453.

وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى قَالَ: {كَانَ زَيْدُ بْنُ أَرْقَمَ يُكَبِّرُ عَلَى جَنَائِزِنَا أَرْبَعًا، وَإِنَّهُ كَبَّرَ عَلَى جَنَازَةٍ خَمْسًا، فَسَأَلْتُهُ فَقَالَ: كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يُكَبِّرُهَا} رَوَاهُ مُسْلِمٌ وَالْأَرْبَعَةُ

Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abuu Laylah[34] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Zayd bin Arqam alikuwa akitamka Takbiyr mara nne wakati wa kuwaswalia maiti wao, lakini mara moja aliwahi kutamka mara tano[35] katika kumswalia maiti mmoja. Nilipomuuliza alisema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitamka Takbiyr hizo.” [Imetolewa na Muslim na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]

 

 

 

454.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه {أَنَّهُ كَبَّرَ عَلَى سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ سِتًّا، وَقَالَ: إِنَّهُ بَدْرِيٌّ} رَوَاهُ سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ وَأَصْلُهُ فِي "اَلْبُخَارِيِّ"

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nilitamka Takbiyr mara sita katika kuiswalia maiti ya Sahl bin Hunayf.[36] Alikuwa ni mmoja wa Maswahaba waliopigana Vita vya Badr.” [Imetolewa na Sa’iyd bin Manswuwr na chanzo chake ni Al-Bukhaariy]

 

 

 

455.

وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه‏ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يُكَبِّرُ عَلَى جَنَائِزِنَا أَرْبَعًا وَيَقْرَأُ بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ فِي اَلتَّكْبِيرَةِ اَلْأُولَى} رَوَاهُ اَلشَّافِعِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitamka Takbiyr mara nne katika Swalaah za maiti wetu na akawa anasoma Faatihatul-Kitaab (kifunguzi cha Kitaab - Suwratul-Faatihah)[37] baada ya Takbiyr ya kwanza.” [Imetolewa na Ash-Shafi’iyy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

456.

وَعَنْ طَلْحَةَ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَوْفٍ قَالَ: {صَلَّيْتُ خَلَفَ ابْنِ عَبَّاسٍ عَلَى جَنَازَةٍ، فَقَرَأَ فَاتِحَةَ الكْتِابِ فَقَالَ: "لِتَعْلَمُوا أَنَّهَا سُنَّةٌ"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Twalhah bin ‘Abdillaah bin ‘Awf[38] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Niliswali nyuma ya Ibn ‘Abbaas Swalaah ya jeneza na akasoma Faatihatul-Kitaab (kifunguzi cha Kitabu – Suwratul-Faatihah) kisha akasema: Nilifanya hivyo ili wajue kuwa hiyo ni Sunnah.”[39] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

457.

وَعَنْ عَوْفِ بْنِ مَالِكٍ رضى الله عنه‏ قَالَ: {صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏عَلَى جَنَازَةٍ، فَحَفِظْتُ مِنْ دُعَائِهِ: "اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ، وَارْحَمْهُ وَعَافِهِ، وَاعْفُ عَنْهُ، وَأَكْرِمْ نُزُلَهُ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُ، وَاغْسِلْهُ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَقِّهِ مِنْ اَلْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ‏ اَلثَّوْبَ اَلْأَبْيَضَ مِنَ الدَّنَسِ، وَأَبْدِلْهُ دَارًا خَيْرًا مِنْ دَارِهِ، وَأَهْلًا خَيْرًا مِنْ أَهْلِهِ، وَأَدْخِلْهُ اَلْجَنَّةَ، وَقِهِ فِتْنَةَ اَلْقَبْرِ وَعَذَابَ اَلنَّارِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Awf bin Maalik[40] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimswalia maiti nami nikakariri du’aa yake:[41]

 

 

 

اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ، وَارْحَمْهُ وَعَافِهِ، وَاعْفُ عَنْهُ، وَأَكْرِمْ نُزُلَهُ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُ، وَاغْسِلْهُ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَقِّهِ مِنْ اَلْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ‏ اَلثَّوْبَ اَلْأَبْيَضَ مِنَ الدَّنَسِ، وَأَبْدِلْهُ دَارًا خَيْرًا مِنْ دَارِهِ، وَأَهْلًا خَيْرًا مِنْ أَهْلِهِ، وَأَدْخِلْهُ اَلْجَنَّةَ، وَقِهِ فِتْنَةَ اَلْقَبْرِ وَعَذَابَ اَلنَّارِ

Allaahumma-ghfir lahu warham-hu, wa 'aafihi wa’-fu 'anhu, wa akrim nuzulahu, wa wassi' mudkhalahu, waghsilhu bilmaai wath-thalji walbaradi, wanaqqihi minal-khatwaayaa kamaa naqqaytath-thawbal abyadhwa minad-danas, wa abdilhu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wa adkhilhul-Jannah, waqihi fitnatal-qabri wa ‘adhaaban-naar  

Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mkirimu kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase dhambi kama vazi jeupe linavyotakaswa uchafu wake na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba  yake na ahli bora kuliko ahli zake, na Muingize Jannah na Mkinge na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto.[42] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

 

458.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏إِذَا صَلَّى عَلَى جَنَازَةٍ يَقُولُ: "اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِحَيِّنَا، وَمَيِّتِنَا، وَشَاهِدِنَا، وَغَائِبِنَا، وَصَغِيرِنَا، وَكَبِيرِنَا، وَذَكَرِنَا، وَأُنْثَانَا، اَللَّهُمَّ مَنْ أَحْيَيْتَهُ مِنَّا فَأَحْيِهِ عَلَى اَلْإِسْلَامِ، وَمَنْ تَوَفَّيْتَهُ مِنَّا فَتَوَفَّهُ عَلَى اَلْإِيمَانِ، اَللَّهُمَّ لَا تَحْرِمْنَا أَجْرَهُ، وَلَا تُضِلَّنَا بَعْدَهُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ، وَالْأَرْبَعَةُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliposwalia maiti, aliomba du’aa hii:

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لِحَيِّـنا وَمَيِّتِـنا وَشـاهِدِنا، وَغائِبِـنا، وَصَغيـرِنا وَكَبيـرِنا، وَذَكَـرِنا وَأُنْثـانا. اللهُـمِّ مَنْ أَحْيَيْـتَهُ مِنّا فَأَحْيِـهِ عَلى الإِسْلام، وَمَنْ تَوَفَّـيْتَهُ مِنّا فَتَوَفَّـهُ عَلى الإِيـمان، اللهُـمِّ لا تَحْـرِمْنـا أَجْـرَهُ، وَلا تُضِـلَّنا بَعْـدَهُ

Allaahumma-ghfir li-hayyinaa wa mayyitinaa, wa shaahidinaa, wa ghaaibinaa, wa swaghiyrinaa, wa kabiyrinaa, wa dhakarinaa, wa unthaanaa. Allaahumma man ahyaytahu minnaa fa Ahyihi ‘alal-Islaami, waman tawaffaytahu minnaa fatawaffahu ‘alal-iymaan. Allaahumma laa tahrimnaa ajrahu, walaa tudhwillanaa ba’-dahu

 

Ee Allaah, Mghufurie aliyehai katika sisi na aliyekufa, aliyepo na asiyekuwepo, mdogo kati yetu na mkubwa, mwanamume kati yetu na mwanamke.  Ee Allaah,  Unayemweka hai kati yetu basi Muweke katika Uislamu, na Unayemfisha basi mfishe juu ya iymaan.  Ee Allaah,  Usitunyime thawabu zake wala usitupoteze baada yake.”[43] [Imetolewa na Muslim na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]

 

 

 

459.

وَعَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {إِذَا صَلَّيْتُمْ عَلَى اَلْمَيِّتِ فَأَخْلِصُوا لَهُ اَلدُّعَاءَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnapomswalia maiti, mtakasieni du’aa.”[44] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

460.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه‏ عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {أَسْرِعُوا بِالْجَنَازَةِ، فَإِنْ تَكُ صَالِحَةً فَخَيْرٌ تُقَدِّمُونَهَا إِلَيْهِ، وَإِنْ تَكُ سِوَى ذَلِكَ فَشَرٌّ تَضَعُونَهُ عَنْ رِقَابِكُمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Liharakisheni jeneza, kwani akiwa mwema, mtakuwa mnampeleka mwisho mzuri, na akiwa muovu basi ni uovu huo mnauondoa shingoni mwenu.”[45] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

461.

وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{"مَنْ شَهِدَ اَلْجِنَازَةَ حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهَا فَلَهُ قِيرَاطٌ، وَمَنْ شَهِدَهَا حَتَّى تُدْفَنَ فَلَهُ قِيرَاطَانِ".‏ قِيلَ: وَمَا اَلْقِيرَاطَانِ ؟ قَالَ: "مِثْلُ اَلْجَبَلَيْنِ اَلْعَظِيمَيْنِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ‏

وَلِمُسْلِمٍ: {حَتَّى تُوضَعَ فِي اَللَّحْدِ}

وَلِلْبُخَارِيِّ: {مَنْ تَبِعَ جَنَازَةَ مُسْلِمٍ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا، وَكَانَ مَعَهُ حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهَا وَيُفْرَغَ مِنْ دَفْنِهَا فَإِنَّهُ يَرْجِعُ بِقِيرَاطَيْنِ، كُلُّ قِيرَاطٍ مِثْلُ أُحُدٍ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayehudhuria jeneza mpaka iswaliwe hupata Qiyraatw moja, na anayehudhuria hadi maiti amezikwa, mtu huyo atapata Qiyraatw mbili.” Akaulizwa Qiyraatw ni nini? Akasema: “Ni kama vilima viwili vikubwa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Mpaka awekwe katika mwanandani.”

Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy pia kutokana na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Mwenye kufuata maziko ya Muislam, kwa Iymaan na kutaka fadhila za Allaah, na akakaa hadi akaswaliwa na akamalizwa kuzikwa, atarejea na thawabu za Qiyraatw mbili, na kila Qiyraatw ni kama mlima wa Uhud.”

 

 

 

462.

وَعَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّهُ رَأَى اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏وَأَبَا بَكْرٍ وَعُمَرَ، يَمْشُونَ أَمَامَ الْجَنَازَةِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ، وَأَعَلَّهُ النَّسَائِيُّ وَطَائِفَةٌ بِالْإِرْسَالِ

Kutoka kwa Saalim[46] alisimulia kutoka kwa baba yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa: “Alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakr na ‘Umar wanatembea mbele ya jeneza.”[47] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Hibbaan, na An-Nasaaiy na wengine wakasema ina dosari]

 

 

 

463.

وَعَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {نُهِينَا عَنِ اتِّبَاعِ الْجَنَائِزِ، وَلَمْ يُعْزَمْ عَلَيْنَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ummu ‘Atwiyyah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “(Wanawake) tumekatazwa kufuata jeneza, lakini haikusisitizwa kwetu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

464.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ ‏ رضى الله عنه ‏ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {إِذَا رَأَيْتُمُ الْجَنَازَةَ فَقُومُوا، فَمَنْ تَبِعَهَا فَلَا يَجْلِسْ حَتَّى تُوضَعَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkiliona jeneza simameni, na yeyote atakayelifuata asiketi[48] chini hadi jeneza hilo liwekwe chini.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

465.

وَعَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ يَزِيدَ رضى الله عنه {أَدْخَلَ الْمَيِّتَ مِنْ قِبَلِ رِجْلَيِ الْقَبْرَ، وَقَالَ: هَذَا مِنَ السُّنَّةِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa Abuu Ishaaqa[49] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema ‘Abdullaah bin Yaziyd[50] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Alimtua chini maiti katika upande wa miguu yake na akasema: “Hii ni Sunnah.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

466.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {إِذَا وَضَعْتُمْ مَوْتَاكُمْ فِي الْقُبُورِ، فَقُولُوا: بِسْمِ اللَّهِ، وَعَلَى مِلَّةِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ، وَأَعَلَّهُ الدَّارَقُطْنِيُّ بِالْوَقْفِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkimuweka maiti wenu kaburini, semeni: BismiLLaahi wa ‘alaa millati Rasuwli-LLaah (Kwa jina la Allaah na kwa kufuata mila ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).”[51] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan, na Ad-Daaraqutwniy aliita Mawquwf (maneno ya Maswahaba)]

 

 

 

467.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {كَسْرُ عَظْمِ الْمَيِّتِ كَكَسْرِهِ حَيًّا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ عَلَى شَرْطِ مُسْلِمٍ

وَزَادَ ابْنُ مَاجَهْ مِنْ حَدِيثِ أُمِّ سَلَمَةَ: {فِي الْإِثْمِ}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad inayokidhi masharti ya Muslim]

Na Ibn Maajah ameongezea kutokana na Hadiyth ya Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) yasema: “Katika kupata dhambi.”

 

 

 

468.

وَعَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {أَلْحَدُوا‏ لِي لَحْدًا، وَانْصِبُوا عَلَى اللَّبِنِ نُصْبًا، كَمَا صُنِعَ بِرَسُولِ اللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَلِلْبَيْهَقِيِّ عَنْ جَابِرٍ نَحْوُهُ، وَزَادَ: {وَرُفِعَ قَبْرُهُ عَنِ الْأَرْضِ قَدْرَ شِبْرٍ} وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

وَلِمُسْلِمٍ عَنْهُ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏أَنْ يُجَصَّصَ الْقَبْرُ، وَأَنْ يُقْعَدَ عَلَيْهِ، وَأَنْ يُبْنَى عَلَيْهِ}

Kutoka kwa Sa’d bin Abii Waqqaasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nitengenezeeni mwanandani na mpange matofali juu ya kaburi langu kama alivyofanyiwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).”[52] [Imetolewa na Muslim]

 

Na Al-Bayhaqiyy alinukuu masimulizi kama hayo kutoka kwa Jaabir, na akaongezea: “Na kaburi lake lilipandishwa juu takribani shubiri moja[53] kutoka ardhini.” [Aliisahihisha Ibn Hibbaan]

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikataza makaburi yasipakwe chokaa, kukaliwa juu yake na kujengwa juu yake.”[54]

 

 

 

469.

وَعَنْ عَامِرِ بْنِ رَبِيعَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏صَلَّى عَلَى عُثْمَانَ بْنِ مَظْعُونٍ، وَأَتَى الْقَبْرَ، فَحَثَى عَلَيْهِ ثَلَاثَ حَثَيَاتٍ، وَهُوَ قَائِمٌ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ

Kutoka kwa ‘Aamir bin Rabiy’ah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalia maiti ya ‘Uthmaan bin Madhw’uwn,[55] kisha akaenda kwenye kaburi lake na akatupia mikono mitatu ya udongo juu yake huku amesimama wima.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy]

 

 

 

470.

وَعَنْ عُثْمَانَ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏إِذَا فَرَغَ مِنْ دَفْنِ الْمَيِّتِ وَقَفَ عَلَيْهِ وَقَالَ: "اِسْتَغْفِرُوا لِأَخِيكُمْ وَسَلُوا لَهُ التَّثْبِيتَ، فَإِنَّهُ الْآنَ يُسْأَلُ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ الْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Uthmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokwisha kuzika maiti, alisimama karibu na kaburi na kusema: “Muombeeni maghfirah ndugu yenu na muombeeni kuthibitishwa[56] kwani hivi sasa anaulizwa.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisaihisha Al-Haakim]

 

 

 

471.

وَعَنْ ضَمْرَةَ بْنِ حَبِيبٍ أَحَدِ التَّابِعِينَ قَالَ: {كَانُوا يَسْتَحِبُّونَ إِذَا سُوِّيَ عَلَى الْمَيِّتِ قَبْرُهُ، وَانْصَرَفَ اَلنَّاسُ عَنْهُ، أَنْ يُقَالَ عِنْدَ قَبْرِهِ: يَا فُلَانُ! قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ.‏ ثَلَاثُ مَرَّاتٍ، يَا فُلَانُ! قُلْ: رَبِّيَ اللَّهُ، وَدِينِيَ الْإِسْلَامُ، وَنَبِيِّ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم‏} رَوَاهُ سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ مَوْقُوفًا

وَلِلطَّبَرَانِيِّ نَحْوُهُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي أُمَامَةَ مَرْفُوعًا مُطَوَّلًا

Kutoka kwa Dhwamrah bin Habiyb[57], mmoja wa At-Taabi’iyna amesema: Wao (Maswahaba) walipomaliza kusawazisha kaburi na watu wakaondoka, walipendelea kusemwe kaburini pake: “Ee fulani! Sema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ.‏ ثَلَاثُ مَرَّاتٍ، يَا فُلَانُ! قُلْ: رَبِّيَ اللَّهُ، وَدِينِيَ الْإِسْلَامُ، وَنَبِيِّ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah mara tatu; Ee Fulani! Sema: Rabb wangu ni Allaah, Dini yangu ni Uislam, na Nabiy wangu ni Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).” [Imetolewa na Sa’iyd bin Manswuwr na akasema ni Mawquwf]

 

Na Atw-Twabaraaniyy alisimulia vivyo hivyo kupitia kwa Abuu Umaamah, Hadiyth hii ni Marfuw’.

 

 

 

472.

وَعَنْ بُرَيْدَةَ بْنِ الْحَصِيبِ الْأَسْلَمِيِّ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{نَهَيْتُكُمْ عَنْ زِيَارَةِ الْقُبُورِ فَزُورُوهَا} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

زَادَ اَلتِّرْمِذِيُّ: {فَإِنَّهَا تُذَكِّرُ الْآخِرَةَ}

زَادَ ابْنُ مَاجَهْ مِنْ حَدِيثِ ابْنِ مَسْعُودٍ: {وَتُزَهِّدُ فِي الدُّنْيَا}

Kutoka kwa Buraydah bin Al-Haswiyb Al-Aslamiyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nilikukatazeni kuzuru makaburi, sasa yazuruni.”[58] [Imetolewa na Muslim]

Na akaongezea At-Tirmidhiy: “Kwani hiyo inakumbusha Aakhirah.”

Akaongezea Ibn Maajah kutokana na Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd: “Humfanyisha kuipa mgongo dunia.”

 

 

 

473.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏لَعَنَ زَائِرَاتِ الْقُبُورِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amewalaani[59] wanawake wanaozuru makaburi.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

474.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ‏ رضى الله عنه‏ قَالَ : {لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ‏ صلى الله عليه وسلم ‏اَلنَّائِحَةَ ، وَالْمُسْتَمِعَةَ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amemlaani mwanamke anayeomboleza (kwa kelele) na anayemsikiliza.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

475.

وَعَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {أَخَذَ عَلَيْنَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏أَنْ لَا نَنُوحَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ummu ‘Atwiyyah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichukua ahadi kwetu kuwa hatutaomboleza tukifiwa.”[60] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

476.

وَعَنْ ابْن عُمَرَ رضى الله عنه‏ عَنِ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {اَلْمَيِّتُ يُعَذَّبُ فِي قَبْرِهِ بِمَا نِيحَ عَلَيْهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Maiti huadhibiwa kaburini[61] kwa sababu ya kuombolezwa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

477.

وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه‏ قَالَ: {شَهِدْتُ بِنْتًا لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ‏تُدْفَنُ ، وَرَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏جَالِسٌ عِنْدَ اَلْقَبْرِ، فَرَأَيْتُ عَيْنَيْهِ تَدْمَعَانِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilishuhudia maziko ya binti ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikaa karibu na kaburi nikamuona akitokwa na machozi.”[62] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

478.

وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {لَا تَدْفِنُوا مَوْتَاكُمْ بِاللَّيْلِ إِلَّا أَنْ تُضْطَرُّوا} أَخْرَجَهُ ابْنُ مَاجَهْ ‏ وَأَصْلُهُ فِي "مُسْلِمٍ"، لَكِنْ قَالَ: زَجَرَ أَنْ يُقْبَرَ اَلرَّجُلُ بِاللَّيْلِ، حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهِ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msizike wafu wenu usiku[63] isipokuwa ikilazimika hivyo.” [Imetolewa na Ibn Maajah, na chanzo chake kipo katika Swahiyh Muslim, isipokuwa alisema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikemea maiti kuzikwa usiku hadi aswaliwe]

 

 

 

479.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ جَعْفَرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {لَمَّا جَاءَ نَعْيُ جَعْفَرٍ ‏حِينَ قُتِلَ‏ قَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "اصْنَعُوا لِآلِ جَعْفَرٍ طَعَامًا، فَقَدْ أَتَاهُمْ مَا يَشْغَلُهُمْ"} أَخْرَجَهُ الْخَمْسَةُ، إِلَّا النَّسَائِيَّ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Ja’far[64] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Ilipokuja taarifa ya kifo cha Ja’far, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema: “Andaeni chakula kwa ajili ya familia ya Ja’far kwani wamepata jambo la kuwashughulisha.”[65] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy]

 

 

 

480.

وَعَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يُعَلِّمُهُمْ إِذَا خَرَجُوا إِلَى اَلمَقَابِرِ: {اَلسَّلَامُ عَلَى أَهْلِ اَلدِّيَارِ مِنَ اَلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُسْلِمِينَ، وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اَللَّهُ بِكُمْ لَلَاحِقُونَ، أَسْأَلُ اَللَّهَ لَنَا وَلَكُمُ الْعَافِيَةَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Sulaymaan bin Buraydah[66] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kwa upokezi wa babake kwa kusema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akifunza Swahaba wake wakienda makaburini (waseme):

اَلسَّلَامُ عَلَى أَهْلِ اَلدِّيَارِ مِنَ اَلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُسْلِمِينَ، وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اَللَّهُ بِكُمْ لَلَاحِقُونَ، أَسْأَلُ اَللَّهَ لَنَا وَلَكُمُ الْعَافِيَةَ

 

As-Salaamu ‘alaa ahlid-diyaari minal-Muuminiyna wal-Muslimiyna, wa innaa In Shaa Allaahu bikum lalaahiquwna, as-alu-Allaah lanaa wa lakumul-‘aafiyah

(Amani iwe juu yenu mliyomo kwenye makazi haya miongoni mwa Waumini na Waislamu. Allaah Akipenda na sisi tutajiunga nanyi. Tunamuomba Allaah Atupe al-‘aafiyah[67] sisi na nyinyi.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

481.

وَعَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {مَرَّ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏بِقُبُورِ اَلْمَدِينَةِ، فَأَقْبَلَ عَلَيْهِمْ بِوَجْهِهِ فَقَالَ: "اَلسَّلَامُ عَلَيْكُمْ يَا أَهْلَ اَلْقُبُورِ، يَغْفِرُ اَللَّهُ لَنَا وَلَكُمْ، أَنْتُمْ سَلَفُنَا وَنَحْنُ بِالْأَثَرِ"} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَقَالَ: حَسَنٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipita katika makaburi ya Al-Madiynah, akayaelekea kwa uso wake akasema:

 

اَلسَّلَامُ عَلَيْكُمْ يَا أَهْلَ اَلْقُبُورِ، يَغْفِرُ اَللَّهُ لَنَا وَلَكُمْ، أَنْتُمْ سَلَفُنَا وَنَحْنُ بِالْأَثَرِ

As-salaam ‘alaykum yaa Ahlal-qubuwr, Yaghfiru-Allaahu lanaa wa lakum, antum salafunaa wa nahnu bil-athar

(Amani iwe juu yenu enyi wakazi wa makaburi haya. Namuomba Allaah Atughufurie sisi na nyinyi, mumetangulia kabla yetu na sisi tutafuata baada yenu).”[68] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na alisema ni Hasan]

 

 

 

482.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{لَا تَسُبُّوا الْأَمْوَاتَ، فَإِنَّهُمْ قَدْ أَفْضَوْا إِلَى مَا قَدَّمُوا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَرَوَى اَلتِّرْمِذِيُّ عَنِ اَلمُغِيرَةِ نَحْوَهُ، لَكِنْ قَالَ: {فَتُؤْذُوا الْأَحْيَاءَ}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msitukane wafu kwani wameshafikia waliyoyatanguliza.” [Imetolewa na al-Bukhaariy]

 

Na katika tamshi la At-Tirmidhiy imesimulia vivyo hivyo kupitia kwa Al-Mughiyrah lakini ikaongezea maneno haya: “Usije ukawadhuru watu walio hai.”[69]

 

[1] Kutajwa kwa kifo aghalabu huleta hisia ya kujinyima, kujikagua kuhusu matendo yako, na khofu ya Qiyaamah, na humhamasisha mtu kutenda mema na kujikita katika hali ya kiakili ya kujiandaa kwa ajili ya siku ya Hesabu.

[2] Kumekatazwa kuomba au kupendelea kifo kwa sababu ya kawaida ya kidunia, ufukara, ugonjwa, n.k. kuomba kukutana na Allaah (سبحانه وتعالى)  hakika ni dalili ya kukamilika kwa Iymaan ya mtu. Kwa hivyo inaruhusiwa kwa mtu kuomba kifo kwa woga wa kupotoka mbali na njia sahihi ya Dini.

[3] Kwa Muumini, maisha ni zawadi au faida. Hadiyth moja inasema: “Muumini, akiwa mwenye taqwa, atakusanya taqwa zaidi. Maisha ni faida kwa mtenda dhambi pia, kwani anaweza kutubu wakati wa uhai wake.”

[4] Uelewa wa hili umepindishwa kwa njia nyingi. Ufafanuzi sahihi ni kwamba, mtu hutoka jasho kadiri machungu ya kifo yanavyozidi kuwa makali. Na machungu ya Muumini hufanywa kuwa makali ili iwe ni toba kwa madhambi yake yote aliyoyatenda duniani nayo husamehewa papa hapa. Hii pia ni zawadi ya Allaah (سبحانه وتعالى)  kwa Waumini.

[5] Ma’qil bin Yasaar ni Swahaba wa Kabila la Muzaynah. Alisilimu kabla ya msafara wa kivita wa Hudaybiyah, na alishiriki katika Bay’atur-Ridhwaan. Mto aliouchimba kule Basra kwa amri ya ‘Umar, uliitwa jina lake. Na tokea wakati ule, ipo mithali isemayo kuwa: “Ikiwa mto wa Allaah utakuja ukibubujika, mto wa Ma’qil utakuwa hauna kazi.” Inasemekana kuwa alifariki Basra mwishoni mwa utawala wa Mu’awiyah mwaka 60A.H. au wakati wa utawala wa Yaziyd.

[6] Hadiyth hii ni dhaifu kwa mujibu wa Shaykh Al-Albani, angalia Al-Irwaa’ (3/150) namba (688).

[7] Huyu Abuu Salamah ndiye ‘Abdullaah bin ‘Abdil-Asad Al-Makhzuwmiy Al-Qurayshiy, mwana wa shangazi (kwa upande wa baba) wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), pia ni ndugu wa Hamzah kwa kunyonya. Wote wawili walinyonyeshwa na Thuwaybah, mjakazi aliyeachwa huru na Abuu Lahab. Abuu Salamah akahamia Uhabeshi (Ethiopia) pamoja na mkewe Ummu Salamah. Alishiriki katika vita vya Badr, na alijeruhiwa katika vita vya Uhud. Jeraha lake likapona, lakini likachipua tena, akafariki mnamo tarehe 3 Jamaadal-Uwlaa mwaka 4.A.H., akamuacha Ummu Salamah ambaye baadaye aliolewa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mnamo mwezi wa Shawwaal mwaka wa 4A.H.

[8] Hii inatufunza sisi kuwa, macho ya mtu anayefariki huwa wazi na hupanuka wakati anapoitazama roho yake wazipendazo ikimtoka. Macho ya mfu yafungwe haraka kwani hayafungiki baada ya mwili kwisha joto lake, na hutia khofu na woga katika akili za watu.

[9] Hii inaonyesha kuwa inaruhusiwa kuubusu mwili wa maiti, ilimradi awe ni Muislam.

[10] Kwa mujibu wa Hadiyth hii, mtu hubaki chini ya deni lake hata baada ya kufariki kwake, kadiri deni lake litavyokuwa bado halijalipwa.

 

[11] Hii ni kwa sharti kwamba, aliyefariki, licha ya kumiliki mali na kuwa na uwezo wa kulipa deni lake, alifariki bila kulipa. Ikiwa mtu atakufa ghafla na akawa hakuwa na muda wa kutosha kulipa deni hilo, au mtu ambaye hana mali lakini ana niyyah njema ya kulipa deni hilo, hata hivyo husamehewa kulipa deni hilo. Moja ya matumizi ya Zakkah ni kulipa madeni ya watu wanaodaiwa.

[12] Kuyaponda au kusaga majani ya mkunazi huosha uchafu kama ifanyavyo sabuni.

 

[13] Mtu alikuwa amesimama ‘Arafah pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alianguka chini ya mlima na akapigwa teke na ngamia jike, halafu akafariki. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawataka watu waliokuwepo pale wasimfunike kichwa wala wasimnyunyuzie marashi mwilini mwake, kwa kuwa Allaah (عزّ وجلّ)  Atamwamsha Siku ya Kufufuliwa akiwa katika hali ya kutamka Talbiyah.

[14] Hadiyth inasema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki, watu walitaharuki juu ya kama wamvue nguo zake zote ili waoshe maiti yake au wafanyeje. Ghafla, watu wakalemewa na hisia ya usingizi, na sauti isiyojulikana ikasikika ikisema kutokea katika kona ya nyumba ile kuwa maiti isivuliwe nguo zake kamwe, na amri hiyo ikatekelezwa na maiti ikaoshwa kama ilivyotakiwa.”

[15] Inaweka wazi kwamba josho la maiti sharti kwa uchache mara tatu. Ikitakikana zaidi ya hapo, basi inaweza kuwa mara tano au saba, lakini Wanazuoni wengi wameafikiana kuwa kuoshwa mara moja kunatosheleza.

[16] Sahuwl ni jina la kijiji kule Yemen, na kitambaa hicho kilitoka huko.

[17] ‘Abdullaah bin Ubayy alikuwa ni Sultani wa kabila la Al-Khazraj wakati wa Jaahiliyyah kabla ya Unabiy wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na akawa mkuu wa wanafiki baada ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuhamia Al-Madiynah. ‘Abdullaah bin Ubayy pamoja na watu wake mia tatu walijitoa kutoka kwenye vita vya Uhudi, na ndiye aliyechangia zaidi kumsingizia ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا). Ndiye pia aliyesema: “Tukirejea Al-Madiynah, mwenye nguvu (yaani yeye) atamfukuza mnyonge (yaani Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).” Pia ndiye aliyesema: “Msiwalishe watu walio pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mpaka wasambaratike.” Alifariki mnamo Dhul Qa’dah mwaka wa 9A.H. mama yake aliitwa Saluwl.

 

[18] Mwanaye ‘Abdullaah bin Ubayy ni ‘Abdullaah bin ‘Abdillaah bin Ubayy bin Saluwl. Alikuwa mmoja wa Maswahaba wema, wadilifu na wakarimu, na alifariki shahidi katika vita vya Al-Yamaamah. Alikuwa ndiye mpinzani mkali kuliko wote dhidi ya baba yake kiasi kwamba aliomba ruhusa amkate kichwa pale baba yake aliposema: “Mwenye nguvu atamfukuza mnyonge.” Jina lake wakati wa Ujaahiliyyah lilikuwa Hubab lakini Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa jina jingine, ambalo ni ‘Abdullaah.

[19] Inamaanisha kuwa, hiyo sanda sharti iwe safi na maridadi, isiwe ghali, kwani kuna Hadiyth inayokataza hilo.

[20] Hii ilikuwa ni dharura tu, kwa vile hakukuweko vitambaa vya kutosha kuwakafini mmoja mmoja wakati ule. Ni utaratibu wa kawaida pia kwamba wanaofariki shahidi hawaswaliwi Swalaah ya Janaazah.

[21] Inamaanisha kuwa, mwanaume anaweza kuosha maiti ya mkewe, na kwa hivyo, watu wengi wanafuata mwenendo huu. Watu wengine wanaipinga hiyo, lakini wengi wa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wanazipinga hoja za wapinzani hao. ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuosha Faatwimah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا), na hali kadhalika ‘Asmaa (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) alimuosha Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Matukio haya yanathibitisha kwamba mme anaweza kumuosha mke, na mke pia anaweza kumuosha mme; na wameafikiana wengi kuwa Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) waliyanyamazia mambo hayo mawili.

[22] Faatwimah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) alikuwa binti mdogo zaidi kuliko mabinti wote wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na ndiye mwanamke mwenye hadhi kubwa zaidi ya Ummah huu. ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuoa mnamo mwezi wa Ramadhwaan mwaka wa 2 A.H. na wakaanza kuishi pamoja mnamo mwezi wa Dhul Hijjah. Wakati ule alikuwa na umri wa miaka 15 na miezi 5. Alifariki mnamo mwezi wa Ramadhwaan mwaka wa 11 A.H, miezi sita baada ya kifo cha baba yake.

[23] ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alitekeleza wasia wa mke wake.

[24] Tafsiri zingine zinasema neno: “Faswuliya” limetumika, ambalo ni “Majhuwl (haijulikani)”, na inamaanisha kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwenyewe hakushiriki katika Swalaah ya maiti yule, bali Maswahaba walimswalia. Ukweli ni kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwenyewe alimswalia Swalaatul-Janaazah, maiti yule.

[25] Kuna kutofautiana maoni kuhusu kumswalia mtu aliyejiua mwenyewe. Wengi wanakubali kuwa Swalaah ya Janaaza kwa mtu huyo ni sharti iwepo. Qaadhi ‘Iyaadh anasema kwa mujibu wa chanzo chake, Wanazuoni wote wanaafikiyana juu ya Swalaah Janaazah ya watu walioadhibiwa au wamepigwa mawe hadi wakafariki, kwa kanuni za Shariy’ah, waliojiua wenyewe, na watoto waliozaliwa nje ya ndoa. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa hahudhurii baadhi ya Swalaah kama hizo za Janaazah, lakini alikuwa akiwaagiza watu wahudhurie.

[26] Inamaanisha kuwa: (a) Ni ruhusa kuswali Swalaah ya Janaazah katika kaburi la mtu, (b) Hakujawekwa kiwango cha muda wa kuweza kumswalia maiti. Hata Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaswalia mashahidi wa Uhud miaka minane baada ya kifo chao. (c) Pia maiti anaweza kuswaliwa mara mbili hadi tatu.

[27] Maana ya neno “Na’y” ni kuwasilisha khabari za kifo cha mtu, ambayo ilikuwa mila ya kijaahiliyyah kuwa kila mtu maarufu alipofariki, khabari ya kifo chake ilitangazwa mji mzima. Mtindo huo umekatazwa. Hata hivyo, unaweza kuwaarifu ndugu na jamaa na wenye taqwa kushiriki katika kumswalia maiti huyo.

[28] An-Najaashiy kilikuwa cheo cha mtawala wa Uhabeshi (Ethiopia) ambaye jina lake halisi lilikuwa Ashama bin Al-Abjar. Waislam wa Makkaah walikimbilia kwake Uhabeshi kwa ajili ya Iymaan na Dini yao, kukimbia ukandamizaji wa makafiri wa Makkah. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma ‘Amr bin Umayyah Ad-Damar mwishoni mwa mwaka wa 6 A.H. au mwezi wa Muharram mwaka wa 7 A.H. kumpelekea An-Najaashiy ujumbe ili apate kusilimu. Aliipokea barua ile, akaiweka juu ya macho yake, akashuka kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, akasilimu. Ja’far bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuandikia barua Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kumpa taarifa hiyo. An-Najaashiy alifariki mnamo mwezi wa Rajab mwaka wa 9 A.H. baada ya vita vya Tabuwk. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Swalaatul-Janaazah kighaybu (Swalaah ya jeneza ya mbali). Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuandikia barua mrithi wa utawala wake ili naye asilimu.

 

[29] Inataja kuruhusiwa kumswalia maiti bila ya mwili wake kuwepo hapo anaposwaliwa. Wengine wanaikanusha hii bila ushahidi wowote.

[30] Inafundisha uombezi wa Muislam kwa Muislam, kwa kumuombea du’aa anusurike, inakubaliwa na Allaah.

[31] Ikiwa maiti ni ya mwanaume, Imaam asimame sehemu ya kichwani, na ikiwa mwanamke Imaam sharti asimame sehemu ya katikati ya maiti.

[32] Baydhwaa ni jina la utani la Mama aitwae Da’ad bint Al-Juhdum Al-Fihriyya, na wanawe wavulana wawili wanaitwa Sahl na Suhayl aliowazaa na Wahaab bin Rabi’a Al-Qurayshiy Al-Fihr. Sahl ndiye aliyeikanusha Sahifa iliyoandikwa na Maqurayshi ili wawasuse Banuu Haashim na Waislam. Ilisemekana kuwa yeye alisilimu waziwazi kule Makkah. Inasemekana pia kuwa aliificha Iymaan yake ya Uislam na akalazimishwa kujiunga na jeshi la Maquraysh apigane vita vya Badr. Alitekwa na Waislam, na ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd alimshuhudia kuwa alimuona akiswali kule Makkah. Kwa hivyo aliachiwa, na akafariki Madiynah. Lakini Suhayl alisilimu mapema sana, akashiriki katika Hijratayn (kuhama mara mbili kuenda Uhabeshi), na kuhudhuria vita vya Badr na vingine vyote muhimu. Alifariki Al-Madiynah mnamo mwaka wa 9 A.H. baada ya vita vya Tabuwk. Mwana wa tatu wa Al-Baydhwaa anaitwa Safwaan ambaye alifariki shahidi kule Badr ilisemwa pia kuwa ulipita muda mrefu baada ya kifo cha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

[33] Watu wengine wanasema si sawa kuswalia maiti ndani ya Msikiti, lakini hawana ushahidi wowote. Isitoshe, imesimuliwa na Ibn Abiy Shayba (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa maiti ya Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) iliswaliwa Msikitini, Imaam akiwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Pia imesimuliwa katika Musnad Sa’iyd bin Mas-‘uwd kuwa maiti ya ‘Umar iliswaliwa Msikitini Imaam akiwa Suhayb (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na pia maiti ya Sa’d bin Abiy Waqqaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) iliswaliwa Msikitini.

[34] ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylah alikuwa Answaar wa mji wa Madiynah kisha akahamia mji wa Kufa. Alikuwa mmoja wa Taabi’iyna wakongwe katika kusimulia Hadiyth. Alipewa jina la utani la Abuu ‘Iysaa na alisimulia Hadiyth kutoka katika kundi la Maswahaba. Alizaliwa mwanzoni mwa miaka sita ya mwisho ya Ukhalifa wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alifariki mwaka wa 86 A.H. katika vita vya Al-Jamajim; na ilisemekana kuwa alizama katika mto wa Basra.

[35] Inasemekana kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwahi kutamka Takbiyr mara nne, tano, sita, saba. ‘Umar aliwathibitisha watu katika Takbiyr nne na ndio inayoendelea hadi leo hii.

[36] Sahl bin Hunayf ni Answaar na Aws (kutoka katika kabila la Aws). Alishiriki vita vya Badr na vilivyofuata. Alisimama imara sana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika vita vya Uhud. Baadaye, ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimteua kuwa mtawala wa Basra, na alishiriki pamoja naye katika vita vya Siffin. Kulikuweko fungamano la udugu kati yake na ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) baada ya Hijra. Alifariki mnamo mwaka wa 38. A.H.

[37] Hadiyth hii ni ushahidi kuwa, kusomwa kwa Suwratul-Faatihah ndani ya Swalaah ya Janaazah ni waajib.

[38] Twalhah bin ‘Abdillaah bin ‘Awf ni Zuhri na Mkurayshi, na ni mwana wa kaka wa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf. Alipewa jina la utani la Twalhah An-Nada, na alikuwa wa kutegemewa, msomi, na alihifadhi Hadiyth nyingi. Alikuwa miongoni mwa Taabi’iyn wa katikati na alifariki mwaka wa 97 A.H akiwa na umri wa miaka 72.

[39] Katika Swalaatul Janaaza, Suwratul-Faatihah husomwa kwa sauti ya chini. Ndiyo sababu Ibn ‘Abbaas aliisoma kwa sauti kubwa na akaeleza: “Niliisoma kwa sauti kubwa ili nyote mjue ni Sunnah.”

[40] ‘Awf bin Maalik alikuwa Swahaba kutoka katika ukoo wa Ashja’, na mwanzoni alishiriki katika vita vya Khaybar, ndiye aliyeshika bendera ya Ashja’ wakati Makkah ilipotekwa. Alilowea Sham na akafariki huko mwaka 73 A.H.

 

[41] Upo uwezekano kuwa ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiisoma du’aa hiyo kwa sauti kubwa, au aliulizia du’aa hii na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamfundisha.

[42] Zipo du’aa mbalimbali zilizosomwa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika Swalaatul-Janaaza, na mtu anaweza kusoma yoyote anayoitaka. Kama ni maiti ya mtoto, soma:

 

اللهُـمِّ اجْعَلْـهُ لَنا فَرَطـاً وَسَلَـفاً وَأَجْـراً

Allaahummaj-’alhu lanaa faratwan wa salafan wa ajraa.

Ee Allaah mfanye kwetu sisi ni kitangulizi cha malipo na dhamana na malipo)

 

 

 

[43] Du’aa nyingi zisomwazo ndani ya Swalaah ya Janaazah zilitoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ); na hii ya hapo juu ni mojawapo. Na kwa vile ni fupi, inapendwa zaidi.

[44] Inaweka wazi, hata kama aliyefariki alikuwa mtu wa dhambi, mtu sharti ulikuze hilo du’aa katika kumuombea kwa Allaah ili Amghufirie madhambi yake. Kuna wengine wanaodai mtu mwenye dhambi ni bora alaaniwe. Maoni kama hayo ni ya makosa na mabaya sana.

[45] Kwa hivyo tunafunzwa kwamba sharti tusikawie kuzika. Wapo watu siku hizi wanaokawiza kuzika maiti, ilhali Shariy’ah ya Kiislam inakataza.

[46] Saalim ndiye Abuu ‘Abdullaah au Abuu ‘Umar Saalim bin ‘Abdillaah bin ‘Umar bin Al-Khatwaab, mmoja wa Taabi’iyn na miongoni mwa Maulamaa maarufu. Alikuwa mmoja wa Wanazuoni saba wa Fiqh, na alikuwa mpokezi wa Hadiyth, mwenye ujuzi na muadilifu. Alifanana na baba yake katika elimu na matumizi yake. Alikufa mnamo mwezi wa Dhul Qa’da mwaka 106 A.H.

 

[47] Wakati wa kuenda mazikoni, ni hiari mtu kuwa mbele ya jeneza, nyuma, kuumeni au kushotoni kwake. Bin Manswuwr kwa upokezi wa Hasan bin ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesimulia kuwa, thawabu azipatazo mtu anayetembea nyuma ya jeneza ni kubwa zaidi kuliko za kutembea mbele ya jeneza. Tofauti yake inaweza kulinganishwa na Swalaah ya mtu anayeswali peke yake na Swalaah ya Jamaa.

[48] Neno “Kuketi” linamaanisha tu kuwa watu wote wanatakiwa wachangie kuzika. Wasiachiwe ndugu tu wa aliyefariki kufanya kila kitu ilhali watu wengine wote wanatazama.

[49] Abuu Is-haaq ndiye ‘Amr bin ‘Abdillaah As-Sabi’i Al-Hamdaaniy Al-Kufi. Ni Taabi’iy maarufu, alisimulia Hadiyth nyingi, lakini alikuwa Mudallis aliyekuja kuwa dhaifu kutokana na uzee katika miaka yake ya mwisho. Alizaliwa miaka miwili kabla ya mwisho wa Ukhalifa wa ‘Uthmaan, na akafa mnamo mwaka 129 A.H.

 

[50] ‘Abdullaah bin Yaziyd ni Khutami, Answaar na Aws. Alihudhuria Al-Hudaybiyyah huku akiwa na umri wa miaka 17, na alikuwa na ‘Aliy katika vita vya Jamal na Siffin. Alilowea Kufa, akawa gavana wake katika wakati wa Az-Zuhayr, na akafariki katika utawala wake.

[51] Imaam Bayhaqiyy alisimulia kwa Isnaad dhaifu ya wapokezi kuwa: “Wakati Ummu Kulthum (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) binti wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akishushwa kaburini, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisoma: “Kutokana nayo (ardhi) Tumekuumbeni, na humo Tutakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine.” [Suwrah Twaahaa: 55]

 بِسْمِ لله وَفي سبيل الله وعلى ملة رسول الله

 

  (Kwa jina la Allaah, kwa njia ya Allaah na kwa kufuata mila za Rasuli wa Allaah (maiti huyu hapa anazikwa).” Zipo du’aa nyingi zingine zilizotajwa katika Hadiyth, ambazo mtu anaweza kuzisoma kadiri anavyopenda.

[52] Hadiyth hii ni ushahidi kwamba kaburi alilotayarishiwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) lilikuwa na Lahd. Maswahaba walitofautiana rai zao kuwa kaburi la Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) liwe la Lahd (mwandani wa katikati) au la Shiq (mwanandani wa pembeni). Kulikuweko wachimba kaburi wawili kule Al-Madiynah siku zile, mmoja aliyekuwa stadi wa kuchimba Lahd, na mwingine wa Shiq. Ilikubaliwa miongoni mwa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuwa mchimba kaburi yeyote atakayekuja kwanza, aanze kazi yake. Kwa hivyo yule stadi wa kuchimba Lahd ndiye aliyekuja kwanza, na akaandaa kaburi ipasavyo.

[53] Shariy’ah ya Kiislam inakataza kuliinua kaburi zaidi ya dhiraa moja (marefu ya kiganja cha mkono). Hivyo ndivyo lilivyokuwa kaburi la Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Mwanzo lilikuwa na umbile bapa au sawasawa. Lakini kuta za chumba cha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) zilipoanguka (kwa sababu ya kutokarabatiwa au kuoza), Waliyd bin ‘Abdil-Maalik alikarabati zile kuta na akalijenga kaburi lile kwa umbile la nundu ya mgongoni kwa ngamia. Makaburi ya Abuu Bakr na ‘Umar Faruwq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) pia yana umbo hilo la ngamia.

[54] At-Tirmidhiy pia anaongeza kuwa makaburi yasiwe na maandishi yoyote, na kusijengwe kitu chochote juu yake, na yasikanyagwekanyagwe. Hadiyth hii imenukuliwa na At-Tirmidhiy kuwa ni sahihi. An-Nasaaiy alisimulia kuwa kusitupiwe mchanga wowote juu yake isipokuwa mchanga uliochimbwa kutoka humo.

[55] ‘Uthmaan bin Mathw’uwn alikuwa Jumahi na Qurayshi. Alikuwa mmoja wa Maswahaba waadilifu na wajumi; na alijinyima ulevi wakati wa jaahiliyyah. Alikuwa wa kumi na nne kusilimu, alishiriki katika Hijrah mbili, na alipigana Badr. Alikuwa Muhaajir wa kwanza kufariki Al-Madiynah. Kifo chake kilitokea mwezi Sha’baan, mwezi wa thelathini tokea Hijrah, naye akazikwa Al-Baqi’. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alibusu uso wake baada ya kufariki, na baada ya kuzikwa akasema: “Huyu ni mtangulizaji mzuri kwetu sisi.” ‘Uthmaan bin Mathw’uwn alikuwa ni ndugu ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa kunyonya.

[56] Kwa hivyo tumefunzwa kwamba, baada ya maziko, kumuombea aliyefariki aghufiriwe dhambi zake, na kumuombea athibitike anapokabiliwa na maswali matatu kaburini ni Mustahabb (Inapendeza) na imesuniwa.

[57] Dhwamrah bin Habiyb ndiye Abuu ‘Utbah Dhwamrah bin Habiyb bin Suhayb Az-Zubayd Al-Himsi ni Taabi’iy anayetegemewa wa daraja la nne.

[58] Kuzuru makaburi ni miongoni mwa matendo yanayopendeza, lakini si lazima. Lakini kuyazuru makaburi ya wazazi kumesisitizwa sana. Mtu anapaswa kuzuru mara kwa mara na awaombee du’aa kwa Allaah.

[59] Kuna kutofautiana miongoni mwa Wanazuoni kuhusu iwapo wanawake wanaruhusiwa kuzuru makaburi au laa. Ni bora wanawake wasiende huko.

[60] Hadiyth hii inakataza kupiga mayowe, kunung’unika, na kuomboleza kwa ajili ya maiti. Kububujika machozi kwa sababu ya hisia ya huzuni hakukatazwi kwa kuwa kunadhihirisha ulaini wa moyo wa mtu, yaani kukataza hakuhusiani na tendo la macho yake mtu, bali kunahusu matendo ya mikono na ulimi tu.

[61] Maiti hupata mateso kwa ajili watu wanaolia kwa mayowe kwa kupinga Aayah isemayo: “Na wala nafsi yoyote haitochuma (khayr au shari) ila ni juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine.” [Al-An’aam: 164]. Hii inahusu hali fulani ambapo kulia kumeonekana katika baadhi ya majumba ya matajiri kama jambo la fahari na majivuno. Watu wengine huacha wasia kuwa vifo vyao vililiwe, wakati wengine hutoa tu idhini kuwa vifo vyao vyaweza kuliliwa. Katika hali kama hizi maiti ndiye atakayepata mateso. Endapo mtu ataacha maagizo kuwa asililiwe, basi yeye hatoteswa. Kwa hivyo ni bora mtu kuwakataza watu wasimlilie pindi atakapofariki.

[62] Hii inatufunza kwamba, kulia kwa kutokwa machozi kutokana na huzuni haikukatazwa. Mwana wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Ibrahiym alipofariki, machozi yalikuwa yakibubujika kutoka machoni mwake. Baada ya kuona hivyo, ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf akamuuliza: “Ee Rasuli wa Allaah!, hata wewe hulia pia? Naye Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akajibu: “Ndiyo huwa nalia, lakini kwa ajili ya upendo siyo kushindwa uvumilivu.”

[63] Hii ina sababu nyingi: moja ni kwamba si watu wengi wanaoweza kushiriki maziko ya usiku. Sababu nyingine ni kuwaepusha watu na vidudu vihalifu vinavyozuru makaburi nyakati za usiku.

[64] Huyu ni Ja’far bin Abiy Twaalib, na ndiye kaka mkubwa (kwa miaka kumi) wa ‘Aliy bin Abiy Twaalib. Alihamia Uhabeshi ambako alibakia akiishi kule ambako Mfalme wa kule An-Najaashiy na wale waliomfuata walisilimishwa na yeye ‘Abdullaah, baadaye alihamia Al-Madiynah, na akafika Khaybar baada ya kutekwa kwake. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Sijui ni ipi ni furaha kubwa zaidi kumuona Ibn Ja’far au kwa kuiteka Khaybar.” Abuu Ja’far alikuwa mmoja wa watu wakarimu sana. Alikufa shahidi katika vita vya Mut’ah mnamo mwaka wa 8 A.H wakati alipokuwa kamanda wa jeshi. Mikono yake yote miwili ilikatwa, na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah alimpa mbawa mbili badala ya mikono yake iliyokatwa, na kwa mbawa hizo anaweza kuruka kwenda popote anapopataka huko Jannah.” Na kwa sababu hii, alikuwa akiitwa “Ja’far mrukaji” na “Ja’far mwenye mbawa mbili.”

[65] Hadiyth inatufundisha kwamba, kuwalisha ndugu wa maiti ni Sunnah. Kuhusu haki za kuwalisha waliofiwa, ni suala la majirani ambao wako msitari wa mbele. Kutoa vyakula siku ya kwanza ni Sunnah, na siku ya pili ni Makruwh (haipendezi), na imekatazwa pia kwa siku ya tatu. Iwapo wanawake waliomo katika nyumba ambamo chakula kinaandaliwa wao wenyewe ni wenye kilio, hapo maoni ya Wanazuoni kuhusu chakula hicho hutofautiana. Ile desturi ya ndugu kukusanyika katika nyumba ya wafiwa, na kwa hiyo wao kuwa mzigo usiokuwa wa lazima kwa familia ya maiti. Tabia hii hufanywa na watu wengi, ni mbaya sana.

[66] Sulaymaan bin Buraydah ndiye Al-Husayb na ni Aslami na Marwazi. Alikuwa Taabi’iy ambaye kutegemewa kwake kulithibitishwa na Ibn Ma’in na Abuu Haakim. Al-Haakim amesema: “Hakutaja kama aliwahi kusikia Hadiyth kutoka kwa babake.” Naye Al-Khazraji amesema: “Hadiyth alizosimulia kutoka kwa baba yake zimo katika sehemu mbalimbali ndani ya Swahiyh Muslim.”

[67] Al-‘Aafiyah maana yake ni: Afya, siha, hifadhi ya kila shari, amani, salama ya Dini duniani na Aakhirah.

[68] Kuenda makaburini na kuwaombea maghfirah maiti ni Sunnah kama ilivyothibitishwa na Hadiyth nyingi. Mtu aendae makaburini azingatie mambo mawili: (a) Kuwaombea maiti du’aa (b) Kukumbuka kifo. Mtu yeyote anayekwenda makaburini kwa ajili ya jambo lolote jingine lisilokuwa haya mawili yaliyotajwa hapo juu, yaani kulia, kuomba maghfirah, kurukuu na kusujudu, na kuomba kukidhiwa haja zake, kuzuru kwake makaburi ni shirki na haraam.

[69] Hadiyth hii inatufunza kuwa, si vizuri kuwataja maiti kwa mabaya au madhambi na kuwatangazia watu, lakini hukmu hii imeamrishwa hususani kwa Waislamu na wenye taqwa.

Share