20-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuoga Baina Ya Matendo Ya Ndoa
Zawadi Kwa Wanandoa
20-Kuoga Baina Ya Matendo Ya Ndoa
الإغتسال بين الجماع
'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: “Atakayemuingilia mke wake kisha akataka kurejea tena katika tendo la ndoa na asafishe tupu yake.” (Atw-Twabaraaniy).
Kadhalika imesimuliwa toka kwa Abu Rafi kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) siku moja aliwazungukia wake zake, akioga kwa huyu na akioga kwa yule. Nikamwambia (Abu Rafi): Ee, Mtume wa Allah, je, huwezi kujaalia josho moja? Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Hivi ni bora, vizuri zaidi na safi zaidi.” (Abu Daawuwd na Ibn Maajah). Katika hadithi nyingine Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anasema:
إذا أتى أحدكم أهله ثم أراد أن يعود , فليتوضأ بينهما وضوءه للصّلاة
“Atakayemuingilia mkewe kisha akataka kurudi tena (katika tendo la tendo) na atawadhe baina ya matendo mawili wudhuu wa Swalah.”
(Muslim, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)
Katika kuchukua wudhuu, kukosha au kuoga ni katika jumla ya kuchangamsha mwili na kuziibua upya nguvu za kiwiliwili. Na si hivyo tu kunahakikisha usafi katika tendo la ndoa (sexual Hygiene).