02-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kwa Walimwengu Wote
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
02-Ametumwa Kwa Walimwengu Wote
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa kwa watu wote uwe mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui. [Sabaa: 28]
Ina maana: Kwa walimwengu wote ambao watahesabiwa matendo yao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً
Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) -Al-Bukhaariy (5011)]
Kwa hiyo yeye ni pekee aliyetumwa kwa walimwengu wote wakiwemo majini na bin Aadam; wakiwa ni waarabu, waajemi, wahindi, waafrika na kadhaalika kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
وَبُعِثْتُ إِلَى كُلِّ أَحْمَر وَأَسْوَد
((… Na nimetumwa kwa (bin Aadam) wekundu wote na weusi)) [Muslim]
Mujaahid amesema: “Hii inamaanisha: Kwa majini na kwa bin Aadam.” Wengineo wamesema: “Kwa Waarabu na wasio Waarabu.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimuamrisha Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aseme:
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote. [Al-A’raaf: 158]
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾
Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]