32-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuchezeana Kwa Kuangaliana!

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

32-Kuchezeana Kwa Kuangaliana!

 

المداعبة عن طريق النّظر

 

Katika kuangalia kunaleta mvuto mkubwa katika moyo wa mwanaadamu na kunaamsha hisia kali za kimapenzi. Baadhi ya washairi wanaona kuwa kuangalia ni mshale unaoteka na kusibu lengo na kuua. Anasema mmoja wao:

 

Nami ninaona lau kama muangaliaji atawindwa

kwa kuangalia kwake mwanamke atakuwa ameniwinda

na kulisemwa zamani: muonaji ni bora ya muhadithiwa.

 

Kule kuona kunahadithia hisia za moyo wa mtu, na huelezea undani wa nafsi na kile ambacho nafsi imekibeba katika hisia za mapenzi ambazo zinapelekea kumsisimsha mtu na kudumisha ndoa.

 

Na ilikuwa ikisemwa hapo nyuma mambo manne hayashibishwi ila na mambo manne:Macho kwa kuona, mwanamke kwa mwanamme, Ardhi kwa kupata mvua na masikio kwa kupata habari.

 

Kuangaliana kwa wanandoa kunapelekea kukubaliana, kuvuta hisia, ambayo inapelekea katika mahaba na kuhurumiana. Hivyo tunaweza kuema Macho ni chanzo cha mvuto na kilele cha ladha ya mapenzi.

 

Na inatakiwa muono huu wa kuangalia uwe sio wa kukazia bali wa kuibia na kusinzia ili anaeonwa aingie haswa katika moyo. Antar kwa ushujaa wake na ugumu wa moyo wake katika kuua maadui zake anaelezea muono wa macho na athari yake kwa kusema:

 

Ee, wewe yule uliyetupa moyo wangu katika kupata

na kuufunika kwa mishale yenye sumu na kuuona kwake ugumu.

 

 

Share