40-Zawadi Kwa Wanandoa: Kujipamba Kwa Ajili Ya Mkeo

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

40-Kujipamba Kwa Ajili Ya Mkeo

 

التزّيّن للمرأة

 

 

Hapana budi kwa wanandoa kujipamba na kuwa safi daima  kila mmoja kwa ajili ya mwenzake. Kujipamba huku ni kwa kuvaa vizuri na kujitia manukato.

 

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

 

حبّب إليّ من دنياكم النّساء والطّيب

“Nimependezeshewa mimi katika dunia yenu wanawake na vitu vizuri vilivyosalimika na uchafu.” (An-Nasaaiy)

 

Kujipamba kunarithisha mapenzi na hujenga na kukuza sababu zote zinazopelekea katika kuzoeana. Kisha kumbuka, “Allaah Hupenda yaliyo mazuri.” (Muslim na At-Tirmidhiy)

 

Ibn 'Abbaas (Radhi ya Allaah iwe kwake na baba yake) anasema: Mimi napenda kujipamba kwa ajili ya mke wangu kama nilivyokuwa napenda yeye ajipambe kwa ajili yangu.

 

Kujipamba ni haki ya wanandoa wote wawili mwanamme na mwanamke. Ni vizuri sana tusilidharau jambo hili la kujipamba na kuona si la muhimu kwani mwenye kuhitajia maisha ya furaha ya ndoa na yenye matokeo mazuri hana budi kujishughulisha na kijipamba.

 

Share