03-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alisisitiza Mno Umma Wake Kuhusu Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

03-Alisisitiza Mno Ummah Wake Kuhusu Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesisitiza mno Husnul-Khuluq (tabia njema) katika Hadiyth nyingi, miongoni mwazo ni ambazo zinabashiria Al-Jannah (Pepo) na pia kuwa karibu naye huko Peponi:  

 

 

1-Aliye na Husnul-Khuluq ni kipenzi cha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atakuwa karibu naye Jannah:

 

عن جابر رضي اللَّه عنه أَن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: (( إِن مِنْ أَحَبِّكُم إِليَّ ، وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجلساً يَومَ القِيَامَةِ، أَحَاسِنَكُم أَخلاقا)) الترمذي حديث حسن

 

Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika walio vipenzi kwangu na watakaokuwa karibu na mimi siku ya Qiyaamah ni wale wenye tabia njema)) [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan].

 

 

2-Taqwa na Husnul-Khulq ndio sababu kuu ya kumwingiza mtu Jannah:

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ‏:‏ سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم‏:‏ مَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ الْجَنَّةَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ ((تَقْوَى اللهِ، وَحُسْنُ الْخُلُقِ)) قَالَ‏:‏ وَمَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ النَّارَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ ((الأَجْوَفَانِ‏:‏ الْفَمُ وَالْفَرْجُ‏.))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Jannah?” Akasema: ((Taqwa (kumcha Allaah) na Husnul-Khuluq (tabia njema)). Na akulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Motoni?” Akasema; ((Mdomo na sehemu za siri)) [Al-Adab Al-Mufrad, Swahiyh Ibn Maajah (3443)], Swahiyh At-At-Tirmidhiy (2004)]

 

 

3-Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amedhamini Jannah kwa anayeacha mabishano na kusema uongo na mwenye khulqa njema:

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ البَاهِلي (رضي الله عنه) قَال: قَال رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَنَا زَعِيم بَيْت فِي رَبَض الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْمِرَاء وَإِنْ كَانَ مُحِقًّا، وَبِبَيْتٍ فِي وَسَط الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْكَذِب وَإِنْ كَانَ مَازِحًا، وَبِبَيْتٍ فِي أَعْلَى الْجَنَّة لِمَنْ حَسُنَ خُلُقه)) حديث صحيح رواه أبو داود بإسناد صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Mimi ni mdhamini wa nyumba ya kando ya Jannah kwa anayeacha mabishano [wenye shaka] hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba iliyo katikati ya Jannah kwa anayeacha uongo japo ni kwa mzaha, na mdhamini wa nyumba iliyo mahala pa juu zaidi ya Jannah kwa ambaye tabia yake ni njema)). [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abu Daawuwd isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

4-Husnul-Khuluq (tabia njema) inasababisha Miyzaan ya matendo kuwa nzito Siku ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَا مِنْ شَىْءٍ أَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ حُسْنِ الْخُلُقِ ‏))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitakachokuwa kizito katika Miyzaan kama Husnul-Khuluq [tabia njema])) [Sunan Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah ((2/535), Swahiyh Al-Jaami’ 7=5721, Swahiyh Adab Al-Mufrad (204)]

 

 

Na pia:

 

عنْ أَنَسٍ قَالَ لَقِيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا ذَرٍّ فَقَالَ: ((يَا أَبَا ذَرٍّ أَلا أَدُلُّكَ عَلَى خَصْلَتَيْنِ هُمَا أَخَفُّ عَلَى الظَّهْرِ وَأَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ غَيْرِهِمَا)) قَالَ:  بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ . قَالَ: ((عَلَيْكَ بِحُسْنِ الْخُلُقِ وَطُولِ الصَّمْتِ فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ مَا عَمِلَ الْخَلائِقُ عَمَلا أَحَبَّ إِلَى اللَّهِ مِنْهُمَا))

 

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokutana na Abuu Dharr alisema: ((Ee Abuu Dharr; je, nikujulishe sifa mbili ambazo ni nyepesi mgongoni mwako na nzito katika kabisa katika Miyzaan kuliko nyinginezo?)) Akasema: “Ndio Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Shikimana na Husnul-Khuluq (tabia njema) na ukae kimya mda mrefu (usiongee upuuzi), kwani Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hakuna 'amali za viumbe Azipendazo Allaah kama hizo mbili)) [Al-Mu’jam Al-Awsatw (7287), At-Targhiyb wat-Tarhiyb ya Al-Mundiriy (3/355) kwa daraja ya Hadiyth Jayyid wasimulizi ni wenye kuaminika]

 

 

5-Husnul-Khuluq inazidisha umri wa mtu:

 

عن عائشة أم المومنينن رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم: ((...صِلةُ الرَّحِمِ وحُسنُ الخُلُقِ وحُسنُ الجِوارِ يَعمُرانِ الدِّيارَ، ويَزيدانِ في الأعمارِ))

Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuunga undugu na Husnul-Khuluq (tabia njema) na kumfanyia wema jirani inaamirisha nyumba na inaongeza umri)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (519), Swahiyh At-Targhiyb (2524)] 

 

 

6-Iymaan ya mtu haikamilikii ila kwa Husnul-Khuluq (tabia njema):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni yule aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni wale walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]

 

 

Hizo ni baadhi ya Hadiyth nyingi zenye kusisitiza Husnul-Khuluq baina ya watu kwa ujumla, kwa mke na mume, na hata kwa makafiri.

 

Share