02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Kutangamana Na Wake
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلنِّكَاحِ
Kitabu cha Nikaah (Ndoa)
بَابُ عِشْرَةِ اَلنِّسَاءِ
02-Mlango Wa Kutangamana Na Wake
865.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَلْعُونٌ مَنْ أَتَى اِمْرَأَةً فِي دُبُرِهَا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ، وَلَكِنْ أُعِلَّ بِالْإِرْسَالِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Amelaaniwa mwenye kumjamii mkewe katika duburi yake.”[1] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, matini ya Hadiyth ni yake. Wapokezi wake ni madhubuti lakini imedhoofishwa kwa kuwa ni Mursal]
866.
وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا يَنْظُرُ اَللَّهُ إِلَى رَجُلٍ أَتَى رَجُلاً أَوْ اِمْرَأَةً فِي دُبُرِهَا} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَأُعِلَّ بِالْوَقْفِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Hamtazami mwanamume aliyemjamii mwanamume au mwanamke katika uchi wake wa nyuma.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan na imedhoofishwa kwa kuwa ni Mawquwf]
867.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاَللَّهِ وَالْيَوْمِ اَلْآخِرِ فَلَا يُؤْذِي جَارَهُ، وَاسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا، فَإِنَّهُنَّ خُلِقْنَ مِنْ ضِلَعٍ، وَإِنَّ أَعْوَجَ شَيْءٍ فِي اَلضِّلَعِ أَعْلَاهُ، فَإِنْ ذَهَبْتَ تُقِيمَهُ كَسَرْتَهُ، وَإِنْ تَرَكْتَهُ لَمْ يَزَلْ أَعْوَجَ، فَاسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
وَلِمُسْلِمٍ: {فَإِنْ اِسْتَمْتَعْتَ بِهَا اِسْتَمْتَعْتَ وَبِهَا عِوَجٌ، وَإِنْ ذَهَبْتَ تُقِيمُهَا كَسَرْتَهَا، وَكَسْرُهَا طَلَاقُهَا}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayemuamini Allaah na siku ya mwisho, asimuudhi jirani yake.[2] Wafanyieni kheri wanawake, hakika wao wameumbwa kwa ubavu, na hakika kitu kilichopotoka zaidi katika ubavu ni ule wa juu, ukitaka kuunyosha utauvunja[3] na ukiuwacha utaendelea kupotoka, kwa hivyo wafanyieni wema wanawake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Ukistarehe naye utastarehe naye akiwa na upotofu. Na ukitaka kumnyoosha utamvunja na kumvunja kwake ni kumtaliki.”
868.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {كُنَّا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فِي غَزَاةٍ، فَلَمَّا قَدِمْنَا اَلْمَدِينَةَ، ذَهَبْنَا لِنَدْخُلَ. فَقَالَ: " أَمْهِلُوا حَتَّى تَدْخُلُوا لَيْلًا يَعْنِي: عِشَاءً لِكَيْ تَمْتَشِطَ اَلشَّعِثَةُ، وَتَسْتَحِدَّ اَلْمَغِيبَةُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ:{إِذَا أَطَالَ أَحَدُكُمُ الْغَيْبَةَ، فَلَا يَطْرُقْ أَهْلَهُ لَيْلاً}
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika vita, tuliporudi Madiynah tulitaka kuingia (majumbani mwetu) Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatuambia: Subirini,[4] ili muingie usiku yaani wakati wa ‘Ishaa ili (mke) mwenye nywele timtim apate kujichana, na yule aliyempoteza mumewe apate kujinyoa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Katika Riwaayah ya Bukhaariy imesema: “Mmoja wenu atakapokuwa safarini muda mrefu basi asiwagongee katu watu wake wakati wa usiku.”
869.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِنَّ شَرَّ اَلنَّاسِ مَنْزِلَةً عِنْدَ اَللَّهِ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، اَلرَّجُلُ يُفْضِي إِلَى اِمْرَأَتِهِ وَتُفْضِي إِلَيْهِ، ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika uovu wa watu kwa daraja kubwa mbele ya Allaah siku ya Qiyamah ni mwanamume anamjamii mkewe kisha akaeneza siri yake, na mwanamke anamjamii mme wake kisha anaeneza siri yake.”[5] [Imetolewa na Muslim]
870.
وَعَنْ حَكِيمِ بْنِ مُعَاوِيَةَ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: {قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَا حَقُّ زَوْجِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ ؟ قَالَ: " تُطْعِمُهَا إِذَا أَكَلْتَ، وَتَكْسُوهَا إِذَا اِكْتَسَيْتَ، وَلَا تَضْرِبِ الْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، وَلَا تَهْجُرْ إِلَّا فِي اَلْبَيْتِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَعَلَّقَ اَلْبُخَارِيُّ بَعْضَهُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Hakiym bin Mu’aawiyah kutoka kwa baba yake amesema: “Niliuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Ni nini wajibu wa mke kwa mumewe? Akasema: Ni umlishe unapokula, umvishe unapovaa, wala usimpige uso, wala usimkaripie wala usimgure ila nyumbani tu.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah. Al-Bukhaariy ameifanya ni Mu’alaqqah baadhi yake. Akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
871.
وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَتِ الْيَهُودُ تَقُولُ: إِذَا أَتَى اَلرَّجُلُ اِمْرَأَتَهُ مِنْ دُبُرِهَا فِي قُبُلِهَا، كَانَ اَلْوَلَدُ أَحْوَلَ. فَنَزَلَتْ: "نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوْا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ" [اَلْبَقَرَة : 223]} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Mayahudi walikuwa wakisema: Mwanamume akimjamii mkewe kinyume nyume kwa uchi wa mbele mtoto akizaliwa atakuwa makengeza. Ikateremka Aayah hii: “Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo” [Al-Baqarah: 223] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
872.
وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَوْ أَنَّ أَحَدَكُمْ إِذَا أَرَادَ أَنْ يَأْتِيَ أَهْلَهُ قَالَ: بِسْمِ اَللَّهِ. اَللَّهُمَّ جَنِّبْنَا اَلشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا، فَإِنَّهُ إِنْ يُقَدَّرْ بَيْنَهُمَا وَلَدٌ فِي ذَلِكَ، لَمْ يَضُرَّهُ اَلشَّيْطَانُ أَبَدًا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau mmoja wenu anapomuendea mkewe (amjamii) aseme:
اَللَّهُمَّ جَنِّبْنَا اَلشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا
BismiLlaah, Allaahumma jannibnaa ash-shaytwaana wa jannibi ash-shaytwaana maa razaqtanaa (Kwa jina la Allaah, Ee Allaah Tuepushe na shaytwaan, na umuepushe shaytwaan katika Utakachoturuzuku). Kisha wakajaaliwa kupata mtoto, shaytwaan hawezi kumdhuru (mtoto huyo) milele.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
873.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {إِذَا دَعَا اَلرَّجُلُ اِمْرَأَتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ فَأَبَتْ أَنْ تَجِيءَ، لَعَنَتْهَا اَلْمَلَائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
وَلِمُسْلِمٍ: {كَانَ اَلَّذِي فِي اَلسَّمَاءِ سَاخِطًا عَلَيْهَا حَتَّى يَرْضَى عَنْهَا}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwanamume atakapomuita mkewe kitandani akakataa kumuendea, akalala, Malaika wanamlaani (mke huyo) mpaka apambazukiwe.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim imesema: “…Aliye mbinguni Atamkasirikia (mke huyo) mpaka mumewe amridhie.”
874.
وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَعَنَ اَلْوَاصِلَةَ وَالْمُسْتَوْصِلَةَ، وَالْوَاشِمَةَ وَالْمُسْتَوْشِمَةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Amemlaani mwanamke[6] mwenye kuunga na mwenye kuungwa nywele na mwenye kuchanja na mwenye kuchanjwa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
875.
وَعَنْ جُذَامَةَ بِنْتِ وَهْبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ:{حَضَرْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فِي أُنَاسٍ، وَهُوَ يَقُولُ: لَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ أَنْهَى عَنِ الْغِيلَةِ، فَنَظَرْتُ فِي اَلرُّومِ وَفَارِسَ، فَإِذَا هُمْ يُغِيلُونَ أَوْلَادَهُمْ فَلَا يَضُرُّ ذَلِكَ أَوْلَادَهُمْ شَيْئًا" . ثُمَّ سَأَلُوهُ عَنِ الْعَزْلِ ؟ فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ "ذَلِكَ اَلْوَأْدُ اَلْخَفِيُّ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Judhaamah bint Wahb[7] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipowaambia watu: Nilitamani kukataza Ghiylah,[8] Nikatazama Warumi na Wafursi nikawakuta wanawafanyia Ghiylah watoto wao wala hilo halidhuru chochote watoto wao. Kisha Maswahaba wakamuuliza kuhusu ‘Azli’[9] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia Huko ndiko kuua kwa siri.” [Imetolewa na Muslim]
876.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَجُلاً قَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ لِي جَارِيَةً، وَأَنَا أَعْزِلُ عَنْهَا، وَأَنَا أَكْرَهُ أَنْ تَحْمِلَ، وَأَنَا أُرِيدُ مَا يُرِيدُ اَلرِّجَالُ، وَإِنَّ اَلْيَهُودَ تُحَدِّثُ: أَنَّ اَلْعَزْلَ المَوْؤُدَةُ اَلصُّغْرَى. قَالَ: " كَذَبَتْ يَهُودُ، لَوْ أَرَادَ اَللَّهُ أَنْ يَخْلُقَهُ مَا اِسْتَطَعْتَ أَنْ تَصْرِفَهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَاَلطَّحَاوِيُّ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa “Mtu mmoja alimjia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nina mjakazi, nami namfanyia ‘azli nachukia kubeba kwake mimba, nami nataka wanayotaka wanaume (kujimai) na Mayahudi huwa wanasema kuwa kufanya ‘azli ni mauaji madogo. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Wayahudi wamedanganya, lau Allaah Angalitaka kumuumba mtoto wewe usingaliweza kumzuia.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Atw-Twahaawiyy, na wapokezi wake ni madhubuti]
877.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {كُنَّا نَعْزِلُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَالْقُرْآنُ يَنْزِلُ، وَلَوْ كَانَ شَيْئًا يُنْهَى عَنْهُ لَنَهَانَا عَنْهُ اَلْقُرْآنُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِمُسْلِمٍ:{فَبَلَغَ ذَلِكَ نَبِيَّ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَلَمْ يَنْهَنَا}
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa tukifanya ‘Azl katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na Qur-aan inateremka. Lau kama (‘azl) ingekuwa ni jambo analokataza basi Qur-aan ingelitukataza.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Muslim inasema: “...habari hiyo ikamfikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wala hakutukataza.”
878.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ كَانَ يَطُوفُ عَلَى نِسَائِهِ بِغُسْلٍ وَاحِدٍ} أَخْرَجَاهُ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alikuwa akiwazungukia wakeze kwa josho moja.”[10] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
[1] Wanazuoni wote wamekubaliana kuwa kumuingilia mwanamke nyuma ni haraam.
[2] Kumkera na kumuudhi Muislamu ni jambo lisilotakiwa, ama kumuudhi jirani ni katika madhambi makubwa.
[3] Hadiyth hii inatufundisha kuwa wanawake waamiliwe kwa wema. Tabia ya mwanamke ni tofauti na ya mwanamume. Kuna sababu nyingi za matatizo anayoyapata mwanamke. Mwanamke ni kama ubavu, ambao ukiunyoosha utauvunja. Tabia ya maumbile aliyoumbwa nayo mwanamke haiwezi kubadilika.
[4] Hii ina maana ikiwa mtu ametoka safari ya mbali, si vizuri kuenda nyumbani kwake moja kwa moja. Ni vizuri kutuma taarifa ya kufika kwako kwanza. Kuna sababu nyingi kuhusu jambo hili. Mume anapoondoka, mwanamke hajiangalii kwa kujiremba na kujiweka vizuri kama kunyoa sehemu zake na usafi mzima wa mwili wake. Suala hili linaweza kuonekana dogo lakini linaweza kumfanya mume akapunguza mapenzi kwa mke wake.
[5] Ina maana ya kuelezea lile tendo kwa watu wengine, kwa hakika kufanya jambo hili kunapelekea katika kufanya jambo la haraam.
[6] Katika Hadiyth hii wamelaaniwa wanawake aina nne: 1-Wenye kuunga nywele, 2-Wenye kuungwa nywele, 3-Wenye kuchanja (tattoo), 4- Wenye kuchanjwa (tattoo) katika miili yao.
[7] Judhaamah bint Wahb ni dada yake ‘Ukaashah bin Mihdhan kwa mama, jina lake lingine ni Jundal Al-Asadiyyah. Alikuwa ni Swahaba miongoni mwa Waislamu wa mwanzo. Alihajiri Madiynah. Alikuwa ni mke wa Anis bin Qataadah.
[8] Ghiylah ni mwanamume amjamii mkewe naye ananyonyesha au akiwa ni mjamzito.
[9] ‘Azl ni kumjamii mkewe na ukifika wakati wa kushusha manii akayamwaga nje kwa ajili ya kupanga kizazi. Suala la uhalaal na uharaam wa ‘Azl ni kuwa kuna Hadiyth kuhusiana na suala hili. Ikiwa imeamuliwa kuwa ‘Azl ni halaal na kwa wakati huo huo Shariy’ah haipendekezi. Kwa kadhia ya mwanamke ambaye afya yake ni mbaya hapa ‘Azl itakuwa lina lengo la kuokoa maisha.
[10] Lengo la Hadiyth hii kuwa ugawaji wa muda haukuwa wajibu kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Ingalikuwa ni wajibu kwake kama kwa watu wengine asingelazimika kuwazunguka wote kwa usiku mmoja.