020-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Je, Kuna Wakati Maalum Wa Kukata Kucha, Kukata Sharubu, Kunyofoa Nywele Za Kikwapa Na Kunyofoa Kinena?
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Twahara
020-Je, Kuna Wakati Maalum Wa Kukata Kucha, Kukata Sharubu,
Kunyofoa Nywele Za Kikwapa Na Kunyofoa Kinena?
Mambo haya hayana wakati maalumu wa kuyafanya, bali kinachoyadhibiti ni haja. Wakati wowote mtu anapohisi kwamba anahitajia kulifanya moja wapo, basi huo ndio wakati wake. La muhimu ni kuwa mtu asijiachie zikapita zaidi ya siku arobaini bila ya kufanya chochote. Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Anas aliyesema:
((Tumewekewa muda wa kuwa tusiachie zikapita siku zaidi ya arobaini bila kukata sharubu, kukata kucha, kunyofoa nywele za kikwapa na kunyoa kinena)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (275) na wengineo].