08-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Swalaah Zetu Hazitimii Ila Baada Kutamka Shahada Mbili Na Kumswalia
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
08-Swalaah Zetu Hazitimii Ila Baada Kutamka Shahada Mbili Na Kumswalia
Katika Swalaah zetu tunapokaa kikao cha Tashahhud, huwa tunamtaja Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kushuhudia kwamba yeye ni Rasuli wa Allaah na kisha tunamswalia kwa kutamka Swalaah inayojulikana kwa ni Swalaatul-Ibraahimiyyah. Kikako cha Tashahhud ni mojawapo ya nguzo za Swalaah ambayo bila ya kufanya hivyo, Swalaah haitimii.
Tunavyotamaka tashahhud na aina za kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
التَّحِيّـاتُ للهِ وَالصَّلَـواتُ والطَّيِّـبات، السَّلامُ عَلَيـكَ أَيُّهـا النَّبِـيُّ وَرَحْمَـةُ اللهِ وَبَرَكـاتُه، السَّلامُ عَلَيْـنا وَعَلـى عِبـادِكَ الصَّـالِحـين، أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله، وَأَشْـهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه
At-tahiyyaatu liLLaahi, was-swalawaatu, wat-twayyibaatu, Assalaamu ‘alayka ayyuhan-Nnabiyyu warahmatu-Allaahi wa Barakaatuh, Assalaamu ‘alaynaa wa ’alaa ‘IbaadiLLaahis-swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu
Maamkuzi mema na Rehma na mazuri yote (ni kwa Allaah), amani ziwe juu yako ee Nabiy na Rehma za Allaah na Baraka Zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah walio wema. Nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Rasuli Wake. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/311), Muslim (1/301)]
اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّد كَمـا صَلَّيـتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد، اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّـد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد .
Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd. Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd.
Ee Allaah! Mswalie Muhammad, na jamaa wa Muhammad, kama Ulivyomswalia Ibraahiym na juu ya jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Ee Allaah! Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na juu ya jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. [Hadiyth ya Ka’ab bin ‘Ujrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/408)]
اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم، وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه كَمـا بارِكْتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد
Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa azwaajihi wa dhurriyaatihi, kamaa Swallayta ‘alaa aali Ibraahiyma, wa Baarik ‘alaa Muhammad, wa ’alaa azwaajihi wa dhurriyaatihi, kamaa Baarakta ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd
Ee Allaah! Mswalie Muhammad na wake zake na kizazi chake, kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym, na Mbariki Muhammad na wake zake na kizazi chake kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. [Hadiyth ya Abu Humayd As-Saa’adiy Al-Mundhir (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/407), Muslim (1/306) na tamashi lake]