074-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muddath-thir Aayah 11- 31: ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
074-Al-Muddath-thir Aayah 11 - 31
Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا﴿١١﴾
Niache Mimi na yule Niliyemuumba Pekee.
وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا﴿١٢﴾
Na Nikamjaalia mali tele.
وَبَنِينَ شُهُودًا﴿١٣﴾
Na watoto wanaoonekana.
وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا﴿١٤﴾
Na Nikamuandalia kwa sahali maandalizi mazuri.
ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ﴿١٥﴾
Kisha anatumaini Nimuongezee.
كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا﴿١٦﴾
Laa, hasha! Hakika yeye amekuwa anidi na mpinzani wa Aayaat Zetu. [Al-Muddath-thir: 11-16]
(mpaka Aayah 31)
Sababun-Nuzuwl:
قال إسحاق: حدثنا عبد الرزاق عن معمر عن أيوب السختياني عن عكرمة عن ابن عباس أن الوليد بن المغيرة جاء رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فقرأ عليه القرآن فكأنه رق له، فبلغ ذلك أبا جهل فأتاه، فقال: "يا عم إن قومك يريدون أن يجمعوا لك مالا". قال: لم؟ قال: ليعطوكه فأنت أتيت محمد لتعرض ما قبله، قال: قد علمت قريش أني من أكثرها مالا، قال: فقل فيه قولا يبلغ قومك أنك منكر له. قال: وماذا أقول، فوالله ما منكم رجل أعرف بالأشعار مني ولا أعلم برجزه ولا بقصيده مني ولا بأشعار الجن، والله ما يشبه الذي يقول شيئا من هذا. ووالله إن لقوله الذي يقوله حلاوة، وإن عليه لطلاوة، وإنه لمثمر أعلاه، مغدق أسفله، وإنه ليعلو ولا يعلى، وإنه ليحطم ما تحته. قال: لا يرضي عنك قومك حتى تقول فيه. قال: قف عني حتى أفكر فيه. فلما فكر قال: إن هذا إلا سحر يؤثر يأثره عن غيره فنزلت: {ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا، وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَمْدُودًا، وَبَنِينَ ...
Is-haaq amesema Abdur-Razaaq ametuhadithia kutoka kwa Ma’mar kutoka kwa Ayyuwb As-Sakhtiyaaniy kutoka kwa ‘Ikrimah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kuwa Al-Waliyd bin Al-Mughiyrah alikwenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsomea Qur-an akawa Waliyd kama kwamba ameathiriwa nayo na kulainika. Habari hiyo ikamfikia Abuu Jahal akamjia akasema: “Ee ‘ammi yangu, kwa hakika watu wako wanataka wakukusanyie mali.” Akasema: “Kwa nini?” Akasema: “Ili wakupatie kwani wewe umemwendea Muhammad ukamuaridhie upate (chakula au mali) yaliyoko kwake!” Akasema: “Ma-Quraysh wote wanajua kuwa mimi ni mtu mwenye mali nyingi.” Akasema: “Basi useme maneno ambayo yatawafikia kuwa wewe unampinga.” Akasema: “Niseme nini? Wa-Allaahi hakuna mtu mwenye kujua mashairi kuliko mimi wala kuliko yeyote katika majini! Na naapa kwa Allaah Ayasemayo (Muhammad) hayafanani na chochote katika haya! Wa-Allaahi kwa hakika maneno ayasemayo (Qur-aan), yana haiba na yanavutia mno! Sehemu yake ya juu kabisa ni neemefu na chini yake inabubujika kwa baraka, na inaangamiza kilicho chini yake!” Abuu Jahl akasema: “Hawatakuwa radhi kwako watu wako hadi useme yaliyo dhidi yake.” Akasema: “Niondokee mbali hadi nifikirie!” Baada ya kufikiri, akasema: “Kwa hakika huu ni uchawi unaoathiri na huathiri wengineo!” Ikateremka:
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا﴿١١﴾
Niache Mimi na yule Niliyemuumba Pekee.
وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا﴿١٢﴾
Na Nikamjaalia mali tele.
وَبَنِينَ شُهُودًا﴿١٣﴾
Na watoto wanaoonekana.
وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا﴿١٤﴾
Na Nikamuandalia kwa sahali maandalizi mazuri.
ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ﴿١٥﴾
Kisha anatumaini Nimuongezee.
كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا﴿١٦﴾
Laa, hasha! Hakika yeye amekuwa anidi na mpinzani wa Aayaat Zetu.
[Hadiyth ameinukuu Al-Haakim katika Al-Mustadrak (2/506-507) na Atw-Twabariy katika Jaami’ Al-Bayaan (29/156) ni Swahiyh] Na pia angalia Al-Bidaayah Wan-Nihaayah (3/60)
Aayah zinazoendelea kuhusiana na tukio hilo:
سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا﴿١٧﴾
17. Nitamshurutisha adhabu ngumu asiyoiweza.
إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ﴿١٨﴾
18. Hakika yeye alitafakari na akakadiria.
فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿١٩﴾
19. Basi alaaniwe na angamie mbali namna alivyokadiria.
ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿٢٠﴾
20. Kisha alaaniwe na angamie mbali namna alivyokadiria.
ثُمَّ نَظَرَ﴿٢١﴾
21. Kisha akatazama.
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ﴿٢٢﴾
22. Kisha akakunja kipaji na akafinya uso kwa ghadhabu.
ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ﴿٢٣﴾
23. Kisha akageuka nyuma na akatakabari.
فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ﴿٢٤﴾
24. Akasema: “Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni sihiri inayonukuliwa.
إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ﴿٢٥﴾
25. “Hii si chochote isipokuwa ni kauli ya binaadamu.
سَأُصْلِيهِ سَقَرَ﴿٢٦﴾
26. Nitamuingiza kumuunguza kwenye moto mkali mno.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ﴿٢٧﴾
27. Na nini kitakachokujulisha huo moto mkali mno?
لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ﴿٢٨﴾
28. Haubakishi na wala hauachi (kitu kisiinguzwe).
لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ﴿٢٩﴾
29. Wenye kubabua vikali ngozi.
عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ﴿٣٠﴾
30. Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.
وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ﴿٣١﴾
31. Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika, na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni jaribio kwa wale waliokufuru; ili wayakinishe wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie iymaan wale walioamini; na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini; na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: “Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu?” Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa Amtakaye na Anamuongoa Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Rabb wako isipokuwa Yeye Pekee, na haya si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa binaadamu.