11-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Swadaqah Hadi Kwamba Alipofariki Hakuacha Dirham Wala Dinari
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
11-Mifano Ya Ukarimu Wake:
Akitoa Swadaqah Hadi Kwamba Alipofariki Hakuacha Dirham Wala Dinari
Kutoa kwake swadaqah Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kulikuwa hadi alipofariki hakuwa na chochote cha kumiliki wala dirham wala dinari kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَخِي جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الْحَارِثِ قَالَ مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيْضَاءَ وَسِلاَحَهُ وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً.
Imepokelewa kutoka kwa ‘Amruw bin Al-Haarith, kaka yake mke wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Alipofariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha dirham wala dinari, wala mtumwa wala kijakazi, isipokuwa baghala wake mweupe (aliyekuwa akimpanda), na silaha na kipande cha ardhi alichokitolea swadaqah.” [Al-Bukhaariy]