Mkate Wa Kumimina (Mkate Wa Sinia) -1
Mkate Wa Kumimina (Mkate Wa Sinia) -1
Vipimo
Mchele 1 Kikombe cha chai
Nazi ya unga 1 Kikombe cha chai
Sukari 1 Kikombe cha chai punguza kidogo
Maziwa vuguvugu (warm) 1 kikombe cha chai
Hamira 1 kijiko cha chai
Hiliki (Cardammom) 1/2 nusu kijiko
Ute wa Yai 1 yai moja
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
- Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka mchanganyiko uwe lani kabisa.
- Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke (ufure).
- Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
- Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
- Funika sufuria na uvumbike (bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
- Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)