009-Hiswnul-Muslim: Du’aa Baada Ya Kutawadha
Hiswnul-Muslim
009-Du’aa Baada Ya Kutawadha
[13]
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ
Ash-hadu an laa ilaaha illaAllaah, Wahdahu laa shariyka Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu
Nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah, Peke Yake, wala Hana mshirika, na ni nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba Muhammad ni mja wake na ni Rasuli Wake[1]
[14]
اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنْ التَّوَّابِينَ وَاجْعَلْنِي مِنْ الْمُتَطَهِّرِينَ
Allaahummaj-’alniy minat-ttawaabiyna waj-’alniy minal mutatwahhariyn
Ee Allaah, nijaaliye niwe miongoni mwa wenye kutubu na nijaalie miongoni mwa wenye kujitoharisha[2]
[15]
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
SubhaanakaAllaahumma wabihamdika, ash-hadu an laa ilaaha illa Anta astaghfiruka wa atuwbu Ilayka
Kutakasika ni Kwako ee Allaah, na Himdi ni Zako, nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, nakuomba unighufurie na natubia Kwako[3]
[1]Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir Al-Juhniy(رضي الله عنه) Hadiyth imetaja atakayesema hivyo na imemalizikia Hadiyth kauli ya Rasuli (صلى الله عليه وسلم) :
((إلاَّ فُتِحَتْ لَهُ أَبْواب الْجَنَّة الثَّمَانِيَة يَدْخُلُ مِنْ أيُّها شآء))
((...basi itafunguliwa milango ya Jannah minane kwa ajili yake aingie wowote atakao))
- Muslim (1/209)
[2]Hadiyth ya ‘Umar bin Khatwwab (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy (1/78) na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (1/18)
[3]Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy(رضي الله عنه) -An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah’ (Uk. 173), [81] na taz Irwaa al-Ghaliyl (1/135), (3/94),