016-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Kufungulia Swalaah
Hiswnul-Muslim
016-Du’aa Za Kufungulia Swalaah
[27]
اللّهُـمَّ باعِـدْ بَيـني وَبَيْنَ خَطـايايَ كَما باعَدْتَ بَيْنَ المَشْرِقِ وَالمَغْرِبْ، اللّهُـمَّ نَقِّنـي مِنْ خَطايايَ كَمـا يُـنَقَّى الثَّـوْبُ الأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسْ، اللّهُـمَّ اغْسِلْنـي مِنْ خَطايـايَ بِالثَّلـجِ وَالمـاءِ وَالْبَرَدْ
Allaahumma baa’id bayniy wa bayna khatwaayaaya kamaa baa’adta baynal-Mashriqi wal-Maghrib. Allaahumma naqqiniy min khatwaayaaya kamaa yunaqqath-thawbul abyadhwu minad-danasi. Allaahumma-ghsiliniy min khatwaayaaya bith-thalji walmaai walbarad.
Ee Allaah niweke mbali na makosa yangu kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi, Ee Allaah nitakase na makosa yangu kama vile inavyoitakaswa nguo nyeupe na uchafu, Ee Allaah nisafishe na makosa yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu[1].
[28]
سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمْـدِكَ وَتَبارَكَ اسْمُـكَ وَتَعـالى جَـدُّكَ وَلا إِلهَ غَيْرُك
Subhaanaka-LLaahumma wabihamdika watabaarakas-Smuka wa Ta’aalaaa Jadduka walaa ilaaha Ghayruka
Utakasifu ni Wako Ee Allaah, na Himdi ni Zako, na Limebarikika Jina Lako, na Umetukuka Ujalai Wako, na hapana mwabudiwa wa haki, ghairi Yako[2].
[29]
وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين. اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت، أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت، وَاهْدِنـي لأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لا يَهْـدي لأَحْسَـنِها إِلاّ أَنْـت، وَاصْـرِف عَـنّْي سَيِّئَهـا، لا يَصْرِفُ عَـنّْي سَيِّئَهـا إِلاّ أَنْـت، لَبَّـيْكَ وَسَعْـدَيْك، وَالخَـيْرُ كُلُّـهُ بِيَـدَيْـك، وَالشَّرُّ لَيْـسَ إِلَـيْك، أَنا بِكَ وَإِلَيْـك، تَبـارَكْتَ وَتَعـالَيتَ، أَسْتَغْـفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيك
Wajjahtu wajhiya liLLadhiy fatwaras-samaawaati wal ardhwa haniyfan wamaa ana minal mushrikiyn. Inna swalaatiy, wanusuky, wamahyaaya wamamaatiy liLLaahi Rabbil ‘aalamiyn. Laa shariyka Lahu wabidhaalika umirtu wa anaa minal Muslimiyn. Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illa Anta. Anta Rabbiy wa ana ‘abduka, dhwalamtu nafsiy wa’taraftu bidhambiy faghfirly dhunuwbiy jamiy’an innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta. Wahdiniy liahsanil-akhlaaqi laa yahdiy liahsanihaa illa Anta, waswrif ‘annyi sayyiahaa laa yaswrif ‘anniy sayyiahaa illa Anta. Labbayka wasa’dayka walkhayru kulluhu biyadika, wash-sharru laysa Ilayka, ana bika wa Ilayka, Tabaarakta wa Ta’aalayta, astaghfiruka wa atuwbu Ilayka
Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu. Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Ndiye Rabb wangu na mimi ni mja Wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nighufurie madhambi yangu yote, hakika haghufurii madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia nzuri kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe. Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi Kwako, Umebarikika na Umetukuka, nakuomba maghfira na narudi Kwako kutubia[3]
[30]
اللّهُـمَّ رَبَّ جِـبْرائيل، وَميكـائيل، وَإِسْـرافيل، فاطِـرَ السَّمواتِ وَالأَرْض، عالـِمَ الغَيْـبِ وَالشَّهـادَةِ أَنْـتَ تَحْـكمُ بَيْـنَ عِبـادِكَ فيـما كانوا فيهِ يَخْتَلِفـون. اهدِنـي لِمـا اخْتُـلِفَ فيـهِ مِنَ الْحَـقِّ بِإِذْنِك، إِنَّـكَ تَهْـدي مَنْ تَشـاءُ إِلى صِراطٍ مُسْتَقـيم
Allaahumma Rabba Jibraaiyla wa Mikaaiyla wa Israafiyla, faatwiras-samaawaati wal ardhw, ’Aalimal ghaybi wash-shahaadah, Anta Tahkmu bayna ’ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwn. Ihdiniy limakhtulifa fiyhi minal haqqi biidhnika Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa swiraatwil-mustaqiym
Ee Allaah Rabb wa Jibiriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo ya ghaibu na yaliyo wazi, Wewe Unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wametofautiana kwa idhini Yako. Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka[4].
[31]
اللهُ أَكْبَـرُ كَبـيرا، اللهُ أَكْبَـرُ كَبـيرا، اللهُ أَكْبَـرُ كَبـيرا، وَالْحَـمْدُ للهِ كَثـيرا، وَالْحَـمْدُ للهِ كَثـيرا، وَالْحَـمْدُ للهِ كَثـيرا، وَسُبْـحانَ اللهِ بكْـرَةً وَأَصيـلا، أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّـيْطانِ مِنْ نَفْخِـهِ وَنَفْـثِهِ وَهَمْـزِه
Allaahu Akbar Kabiyraa, Allaahu Akbar Kabiyraa, Allaahu Akbar Kabiyrah, wal hamduliLLaahi kathiyraa, wal hamduliLLaahi kathiyraa, wal hamduliLLahi kathiyraa, wasubhaana-Allaahi bukratan wa aswiylaah, wasubhaana-Allaahi bukratan wa aswiylaah, wasubhaana-Allaahi bukratan wa aswiylaah. A’uwdhu biLLaahi minash-shaytwaani min nafkhihi wa nafthihi wa hamzihi
Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Himdi Anastahiki Allaah kwa wingi, Himdi Anastahiki Allaah kwa wingi, Himdi Anastahiki Allaah kwa wingi, Ametakasika Allaah asubuhi na jioni. Najikinga na Allaah kutokana na shaytwaan, na kibri yake, na kupulizia kwake na kutia kwake wasiwasi (katika nyoyo za binaadamu)[5]
[32]
اللّهُـمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ نـورُ السَّمـواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَـيِّمُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ) (وَلَكَ الْحَمْدُ) (أَنْتَ الْحَـقُّ، وَوَعْـدُكَ الْحَـقُّ ، وَقَوْلُـكَ الْحَـقُّ، وَلِقـاؤُكَ الْحَـقُّ، وَالْجَـنَّةُ حَـقُّ، وَالنّـارُ حَقُّ، وَالنَّبِـيّونَ حَـقُّ، وَمـحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حقُّ ، والسَّاعَةُ حَـقُّ) (اللّهُـمَّ لَكَ أَسْلَمتُ، وَعَلَـيْكَ تَوَكَّلْـت، وَبِكَ آمَنْـت، وَإِلَـيْكَ أَنَبْـتُ، وَبِـكَ خاصَمْتُ، وَإِلَـيْكَ حاكَمْـتُ، فاغْفِـرْ لي مـا قَدَّمْتُ، وَما أَخَّـرْتُ، وَما أَسْـرَرْتُ، وَما أَعْلَـنْتُ) (أَنْتَ المُقَـدِّمُ وَأَنْتَ المُـؤَخِّر، لاَ إلَهَ إِلاّ أَنْـت) (أَنْـتَ إِلـهي لا إلَهَ إِلاّ أَنْـت)
Allaahumma Lakal-Hamdu Anta Nuwrus-samaawati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Qayyimus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Rabbus-samawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hhamdu Laka Mulkus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Antal-Haqqu, wawa’dukal-haqqu, waqawlukal-haqqu, waliqaaukal-haqqu, wal-Jannata haqqun, wannaaru haqqun, wannabiyyuwna haqqun, wa Muhammadun SwallaAllaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam haqqun, was-saa’atu haqqun. Allaahumma Laka aslamtu, wa ’Alayka tawakkaltu, wabika aamantu, wa Ilayka anabtu, wabika khaaswamtu, wa Ilayka haakamtu, faghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu, wamaa a’lantu, Antal-Muqaddimu wa Antal-Muakh-khiru laa ilaaha illa Anta. Anta Ilaahiy laa ilaaha illa Anta
Ee Allaah, Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Mfalme wa mbingu na ardhi, na Himdi ni Zako, Wewe ni haki [kweli] na ahadi Yako ni ya kweli, na neno Lako ni la kweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na Jannah ni kweli, na Moto ni kweli, na Manabii ni kweli, na Muhammad SwallaAllaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam ni kweli, na Qiyaamah ni kweli. Ee Allaah, Kwako nimejisalimisha, na kwako nimetawakali, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimerejea kutubia.
Na kwa ajili Yako (au kwa hoja na dalili Zako) nimetetea (maadui Wako). Na nimeelekea Kwako kukufanya Wewe ni Hakimu Wangu (kuhukumu baina yetu). Basi nighufurie niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza; Wewe Ndiye Al-Muqaddimu (Mwenye kutanguliza) na Al-Muakh-khiru (Mwenye kuchelewesha), hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe; Wewe Ndiye Mwabudiwa wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe.[6]
[1]Hadiyth ya Abu Huraryah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (1/181), Muslim (1/4190)
[2]Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) - Aswhaab As-Sunan wanne na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (1/77) na Swahiyh Ibn Maajah (1/135)
[3]Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه) - Muslim (1/534)
[4]Hadiyth ya ‘Aishah (رضي الله عنها) - Muslim (1/534)
[5]Hadiyth ya Jubayr bin Mutw-‘im (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (1/203), Ibn Maajah (1/265), Ahmad (4/85), na Muslim kutoka kwa ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) kama hivyo na mna kisa humo (1/420)
[6]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abaas (رضي الله عنهما) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (3/3), (11/116), (13/371, 423, 465), na Muslim kwa ufupi kama hivyo (1/532)