018-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuinuka Kutoka Kenye Rukuu

Hiswnul-Muslim

018-Du’aa Ya Kuinuka Kutoka Kenye Rukuu

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

 [38]

سَمِـعَ اللهُ لِمَـنْ حَمِـدَه

 

Sami’a Allaahu liman hamidah

 

Allaah Amemsikia mwenye kumsifu[1]

 

 

 

[39]

رَبَّنـا وَلَكَ الحَمْـدُ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُـبارَكاً فيه

 

Rabbanaa walakal-hamdu, hamdan kathiyran twayyiban mubaarakan fiyhi

 

Ee Rabb wetu, ni Zako Himdi, Himdi nyingi, nzuri, zenye Baraka[2]

 

 

 

[40]

 

مِلْءَ السَّمـواتِ وَمِلْءَ الأَرْض، وَما بَيْـنَهُمـا، وَمِلْءَ ما شِئْـتَ مِنْ شَيءٍ بَعْـدْ، أَهـلَ الثَّـناءِ وَالمَجـدْ، أَحَـقُّ ما قالَ العَبْـد، وَكُلُّـنا لَكَ عَـبدٌ، اللّهُـمَّ لا مانِعَ لِما أَعْطَـيْت، وَلا مُعْطِـيَ لِما مَنَـعْت، وَلا يَنْفَـعُ ذا الجَـدِّ مِنْـكَ الجَـد

 

Mil-as-samawaatil wamil-al-ardhwi wamaa baynahumaa, wamil-a maa Shi-ita min shay-in ba’du. Ahlath-thanaa-i walmajdi. Ahaqqu maa qaalal-‘abdu, wakullunaa Laka ‘abdun. Allaahumma laa maani’a limaa A’-twayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu

 

Zimejaa mbingu na zimejaa ardhi na vilivyomo ndani yake (Himdi Zako), na zimejaa (Himdi Zako) kwa Ulichokitaka baada yake, Wewe ni Mstahiki wa Sifa na Utukufu, ni kweli aliyoyasema mja (Wako), na sote (sisi) ni waja Wako, Ee Allaah, hakuna mwenye kukizuia Ulichokitoa, wala mwenye kutoa Ulichokizuia, na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako.[3].

 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/282)

 

[2]Hadiyth ya Rifaa’ah bin Raafi’ Az-Zurqiyy (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/284)

 

[3]Hadiyth ya Abu Sa’iy Al-Khudriyy (رضي الله عنه) - Muslim (1/346)

 

 

 

Share