032-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Qunuwt Ya Witr

Hiswnul-Muslim

032-Du’aa Ya Qunuwt Ya Witr

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[116]

 

اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، (وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت) تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.

 

Allaahummah-diniy fiyman Hadayta, wa 'Aafiniy fiyman 'Aafayta, wa Tawallaniy fiyman Tawallayta, wa Baarik-liy fiymaa A'attawyta, wa Qiniy sharra maa Qadhwayta, fainnaka Taqdhwiy  walaa yuqdhwa 'Alayka. Innahu laa yadhillu man Waalayta, walaa ya'izzu man 'Aadayta, Tabaarakta Rabbanaa wa Ta'aalayta.

 

Ee Allaah! Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya pamoja na Uliowapa afya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya  wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hana ’izzah (hadhi)  Uliyemfanya adui) Umebarikika Ee Rabb wetu na Umetukuka[1]

 

 

 

 [117]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك

 

Allaahumma inniy a'uwdhu bi Ridhwaaka min sakhatwika, wa bi mu'aafaatika min 'uquwbatika, wa a'uwudhu Bika Minka, laa ukhswiy Thanaa-an 'Alayka, Anta kamaa Athnayta 'Alaa Nafsika.

 

Ee Allaah! Hakika mimi najikinga kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najikinga  Kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako kwa kadiri ya idadi yake, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe[2]

 

 

 

 [118]

 

اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك

 

Allaahumma Iyyaaka na'-budu, walaka nuswwaliy wa nasjudu, wa Ilayka nas-'aa wa nahfidu, narjuw Rahmataka wa nakhshaa 'adhaabak, inna 'adhaabaka bilkaafiriyna mulhaqq. Allaahumma innaa nasta'iynuka wa nastaghfiruka, wa nuthniy 'Alaykal-khayra, wa laa nakfuruka, wa nu-uminu Bika, wa nakhdhwa'u Laka, wa nakhla'u man yakfuruka.

 

Ee Allaah! Wewe tu Ndiye tunayekuabudu, na Kwako tunaswali na tunasujudu, na Kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji Rehma Yako na tunaogopa adhabu Yako, kwani adhabu Yako hakuna shaka kuwa makafiri itawafikia. Ee Allaah! Hakika sisi tunakutaka msaada na tunakuomba maghfirah na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anayekukufuru[3]

 

 

 

[1]Hadiyth ya Al-Hasan bin ‘Aliy (رضي الله عنهما) - Aswhaabus-Sunan wane; Abu Daawuwd [1425], At-Tirmdhiy [464], An-Nasaaiy (1/252), Ibn Maajah [1178], Ahmad (1/200), Ad-Daarimiy (1/373), Al-Haakim (3/173), Al-Bayhaqiy (2/209) [497, 4987]. Taz pia Swahiyh At-Tirmidhiy (1/144) na Swahiyh Ibn Maajah (1/194), na Irwaa Al-Ghaliyl ya Al-Albaaniy (رحمه الله)  (2/172).

[2]Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه), -Aswaabus-Sunan wane; Abu Daawuwd [ 1427], At-Tirmidhiy [3561], An-Nasaaiy (1/252), Ibn Maajah [1179], Ahmad (1/96, 118, 150), na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/180), Swahiyh Ibn Maajah (1/194) na Al-Irwaa (2/175)

[3]Hadyth ya ‘Umra bin Al-Khatwaab (رضي الله عنه) - Al-Bayhaqiy katika As-Sunan Al-Kubraa na ameisahihisha isnadi yake (2/211) na amesema Shaykh Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Arwaa Al-Ghaliyl na hii isnadi Swahiyh (2/170) nayo ni mawquwfun kwa ‘Umar (رضي الله عنه).

 

 

Share