034-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ukiwa Na Wahka Na Huzuni

Hiswnul-Muslim

034-Du’aa Ukiwa Na Wahka Na Huzuni

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

 

[120]

 

اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ، ابْنُ عَبْـدِكَ، ابْنُ أَمَتِـكَ نَاصِيَتِي بِيَـدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤكَ، أَسْأَلُـكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ، سَمَّـيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أِوْ أَنْزَلْتَـهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْـتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِـكَ، أَوِ اسْتَـأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْـبِ عِنْـدَكَ، أَنْ تَجْـعَلَ القُرْآنَ رَبِيـعَ قَلْبِـي، وَنورَ صَـدْرِي، وجَلَاءَ حُـزْنِي، وذَهَابَ هَمِّـي 

Allaahumma inniy ‘abduka, ibnu-‘abdika, ibnu-amatika, naaswiyaatiy Biyadika, maadhwin fiyya hukmuka, ‘adlun fiyya qadhwaauka, as-aluka bikullismin huwa Laka, sammayta bihi Nafsaka aw Anzaltahu fiy Kitaabika, aw ‘Allamtahu ahadan min Khalqika, awis-staa-tharta bihi fiy ‘ilmil-ghaybi  ‘Indaka, an Taj-’alal-Qur-aana rabiy’a qalbiy, wanuwra swadriy, wajalaa huzniy, wadhahaaba hammiy.

 

Ee Allaah hakika mimi ni mja Wako, mwana wa mja Wako, mwana wa mja wako mwanamke, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Kwako Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yoyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijuwa) katika ilimu ya ghaibu Kwako, nakuomba Ujaalie Qur-aan kuwa ni rabiy' (uhuisho, raha, furaha na ustawisho) wa moyo wangu na nuru ya kifua changu, na ufumbuzi wa  huzuni yangu[1]

 

Mwanamke aseme:

 اللَّهُمَّ إنِّي أَمَتُك، بِنْتُ عَبْدِك، بنتُ أَمَتِك[2]

 

Allaahumma inniy amatuka, bintu ’abdika, bintu amatika ... 

 

Ee Allaah, hakika mimi mja Wako mwanamke, binti wa mja wako, binti wa mja Wako mwanamke...

 

 

 [121]

اللّهُـمَّ إِنِّي أَعْوذُ بِكَ مِنَ الهَـمِّ وَالْحُـزْنِ، والعًجْـزِ والكَسَلِ والبُخْـلِ والجُـبْنِ، وضَلْـعِ الـدَّيْنِ وغَلَبَـةِ الرِّجال.

 

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika minal hammi walhuzni, wal ‘ajzi walkasli, walbukhli, waljubni, wadhwal-‘id-dayni waghalabatir-rijaal

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kutokana na wahka na huzuni na kushindwa nguvu na  uvivu na ubakhili na uoga na uzito wa deni na kushindwa na watu[3]

 

 

 

 

[1]Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) - Ahmad (1/391) [452], Al-Haakim (1/509) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Al-Kalimi Atw-Twayyib [124].

 

[2] Majmuw’ Fataawaa Ibn Baaz (6/76) na Majmuw’ Fataawa Ibn Taymiyyah (2/177).  

 

[3]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) Al-Bukhaariy (7/158) [6363], Taz Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/173). At-Tirmidhiy “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akizidisha kuisoma du’aa hii”.

Share