040-Hiswnul-Muslim: Du’aa Aliyepatwa Na Shaka Katika Iymani Yake

Hiswnul-Muslim

040-Du’aa Aliyepatwa Na Shaka Katika Iymani Yake

www.alhidaaya.com

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

[132]

 

1-Aombe kinga kwa Allaah (aseme:)

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم

Au’wudhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiym

 

 

2-Aondoe moyoni kile kitu alichokifanyia shaka[1]

 

 

[134]

 

3-Kisha aseme:

آمَنْـتُ بِاللهِ وَرُسُـلِه

Aamantu BiLLaahi wa Rusulih

 

Nimemuamini Allaah na Rasuli Wake[2]

 

 

[135]

 

 

4-Kisha asome kauli ya Allaah Ta’aalaa:  

  هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣

 

3. Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi. [3]

 

 

 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) – Kauli mbili hizo ni katika Hadiyth moja aliyoitoa Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/336) [3276], Muslim (1/120) [134], [214].

[2]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Muslim (1/119, 120) [134], [212].

[3]Ameisoma hivyo ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) - Abu Daawuwd (4/329) [5110] na ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (3/962). Aayah Suwratul Hadiyth (57:3). Na katika Muslim [2713] amepokea kuhusu Tafsiyr ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) Majina manne (ya Allaah) yaliyotajwa katika Aayah kwa du’aa yake (صلى الله عليه وسلم)

 

اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ, وَأَنْتَ الآَخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ, وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ, وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ

((Ee Allaah, Wewe Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yako, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yako, na Uliye juu hakuna kitu juu Yako, na Uliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Wewe)).

 

 

Share