042-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Aliyeingiwa Na Wasiwasi Katika Swalaah Yake Au Kisomo Chake
Hiswnul-Muslim
042-Du’aa Ya Aliyeingiwa Na Wasiwasi Katika Swalaah Yake Au Kisomo Chake
[138]
أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطانِ الرَّجِيْمِ
Au’wudhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiym
Najikinga na Allaah kutokana na shaytwaan aliyelaaniwa. (Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu)[1] [yaani kama mwenye kupuliza].
[1]Hadiyth ya ‘Uthmaan bin Abi Al-‘Aasw (رضي الله عنه) amesema: “Nilimwambia Rasuli (صلى الله عليه وسلم): Ee Rasuli wa Allaah hakika Shaytwaan amenikalia kati yangu na kati ya Swalaah yangu na kisomo changu, ananitatiza. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akasema: ((Huyo ni Shaytwaan aitwae Khanzab ukimuhisi amekujia basi muombe Allaah kinga kutokana na [wasiwasi] naye, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu)) Akasema: ”Nikafanya hivyo Allaah akaniondoshea” - Muslim (4/1729) [2203].