053-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Aliyepatwa Na Msiba

Hiswnul-Muslim

053-Du’aa Ya Aliyepatwa Na Msiba

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

[154]

إِنّا للهِ وَإِنَا إِلَـيْهِ رَاجِعُـونَ، اللهُـمِّ اْجُـرْني فِي مُصِـيبَتي، وَاخْلُـفْ لِي خَيْـراً مِنْـها.

 

Innaa liLLaahi wa innaa Ilayhi raaji’uwn, Allaahumma Ajirniy fiy muswiybatiy wa Akhlif liy khayran minhaa

 

Hakika sisi wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea, ee Allaah, Nilipe kwa msiba wangu na Nipe badala yake kilicho bora kuliko huo (msiba)[1]

 

 

 

[1]Hadiyth ya Ummu Salamah -(رضي الله عنها) , “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Mja yeyote atakayepatwa na msiba akasema:

إِنّا للهِ وَإِنَا إِلَـيْهِ رَاجِعُـونَ، اللهُـمِّ اْجُـرْني فِي مُصِـيبَتي، وَاخْلُـفْ لِي خَيْـراً مِنْـها

Allaah Atampa thawabu na Atambadilishia kwa kilicho bora zaidi)). Akasema Ummu Salamah: ”Alipofariki Abu Salamah nilisema kama alivyoniamrisha Rasuli wa Allaah, na Allaah Akanibadilishia aliyebora kuliko yeye naye ni Rasuli wa Allaah” - Muslim  (2/632) [918].

 

 

Share