069-Hiswnul-Muslim: Du’aa Kabla Ya Kula
Hiswnul-Muslim
069-Du’aa Kabla Ya Kula
[178]
Atakapo kula mmoja wenu chakula basi aseme:
بِسْمِ الله
BismiLLaahi
Kwa Jina la Allaah
(إذا نسي فليقل) بِسْمِ اللَّهِ أَوَّلَهُ وَآخِرَهُ
(Akisahau sema): BismiLLaahi awwalahu wa aakhirahu
Kwa Jina la Allaah, mwanzoni na mwishoni[1]
[179]
Yeyote ambaye Allaah Amemruzuku chakula aseme:
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَأَطْـعِمْنا خَـيْراً مِنْـهُ
Allaahumma Baarik lanaa fiyhi wa Atw-’imnaa khayran minhu
Ee Allaah Tubarikie [chakula hichi] na Tulishe bora kuliko hichi
Na yoyote ambaye Amemruzuku maziwa basi aseme:
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَزِدْنا مِنْهُ
Allaahumma Baarik lanaa fiyhi wa Zidnaa minhu
Ee Allaah Tubarikie [kinywaji] hichi na Utuzidishie[2]
[1]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عهما) , Kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم):
((إذا أكل أَحَدُكُمْ فَليَذْكُر اسْمَ اللَّه تعالى، فإنْ نسي أَنْ يَذْكُرَ اسْمَ اللَّه تَعَالَى في أَوَّلِهِ، فَليَقُلْ: بِسْمِ اللَّه أَوَّلَهُ وَآخِرَهُ))
((Atakapokula mmoja wenu, ataje Jina la Allaah Ta’aalaa, lakini akisahau kumtaja Allaah Ta’aalaa mwanzoni, basi aseme: ((Kwa Jina la Allaah, mwanzoni na mwishoni)) Abu Daawuwd (3/347), At-Tirmidhiy (4/288), Taz Swahiyh At-Tirmidhiy (2/167)
[2]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما)
((مَنْ أَطْعَمَهُ اللَّهُ الطَّعَامَ فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيهِ وَأَطْعِمْنَا خَيْرًا مِنْهُ وَمَنْ سَقَاهُ اللَّهُ لَبَنًا فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيهِ وَزِدْنَا مِنْهُ))
((Ambaye Allaah Amemruzuku chakula aseme: Ee Allaah Tubarikie [chakula hichi] na Tulishe bora kuliko hichi. Na ambaye Allaah Amemruzuku maziwa, aseme: Ee Allaah Tubarikie [kinywaji] hichi na Utuzidishie)) At-Tirmidhiy (5/506) [3455], na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/158).