089-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kumuombea Anaekwambia Anakupenda Kwa Ajili Ya Allaah
Hiswnul-Muslim
089-Du’aa Ya Kumuombea Anaekwambia Anakupenda Kwa Ajili Ya Allaah
[200]
أَحَبَّـكَ الّذي أَحْبَبْـتَني لَه
Ahabbaka-lladhiy Ahbabtaniy Lah
Akupende Ambaye umenipenda mimi kwa ajili Yake[1]
[1]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه)
أَنَّ رَجُلًا كَانَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَمَرَّ بِهِ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! إِنِّي لَأُحِبُّ هَذَا .فَقَالَ لَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَعْلَمْتَهُ؟)) قَالَ: لَا. قَالَ: ((أَعْلِمْهُ)). قَالَ: فَلَحِقَهُ فَقَالَ: إِنِّي أُحِبُّكَ فِي اللَّهِ. فَقَالَ: أَحَبَّكَ الَّذِي أَحْبَبْتَنِي لَهُ
Mtu mmoja alikuwa (ameketi) pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akapita mtu mwengine akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nampenda huyu!” Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akamuuliza: ((Je umemjulisha?)) akasema: “Hapana”. Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akasema: ((Basi mjulishe)). Akainuka na kumwendea yule mtu akamwambia: “Hakika mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah”. Yule mtu akajibu: “Akupende Ambaye umenipenda mimi kwa ajili Yake”. - Abu Daawuwd (4/333) [5125], ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Sunan Abi Daawuwd (3/965)