091-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapolipa Deni
Hiswnul-Muslim
091-Du’aa Unapolipa Deni
[202]
بارَكَ اللهُ لَكَ في أَهْلِكَ وَمالِك، إِنَّما جَـزاءُ السَّلَفِ الْحَمْدُ والأَداَءُ
Baaraka Allaahu laka fiy ahlika wa maalika. Innamaa jazaaus-salafi Alhamdu wal adaau
Allaah Akubariki katika familia yako na mali yako, hakika malipo ya deni ni kushukuru na kulipa[1]
[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Abiy Rabiy’ah Al-Makhzumiyyu (رضي الله عنه),
استَقْرَضَ مِنِّي النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَرْبَعِينَ أَلْفًا فَجَاءَهُ مَالٌ فَدَفَعَهُ إِلَيَّ وَقَالَ: ((بَارَكَ اللَّهُ لَكَ فِي أَهْلِكَ وَمَالِكَ إِنَّمَا جَزَاءُ السَّلَفِ الْحَمْدُ وَالْأَدَاء))
“Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alinikopa elfu arubaini. Akapata mali akanilipa akasema:
بارَكَ اللهُ لَكَ في أَهْلِكَ وَمالِك، إِنَّما جَـزاءُ السَّلَفِ الْحَمْدُ والأَداَءُ
((Allaah Akubariki katika familia yako na mali yako, hakika malipo ya deni ni kushukuru na kulipa)) - An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah (Uk. 300) [372], na Ibn Maajah (2/809) [2424] na angalia: Swahiyh ibn Maajah (2/55)