28-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Atakuwa Wa Kwanza Kuingia Jannah Pamoja Na Ummah Wake

 

 

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

28-Atakuwa Wa Kwanza Kuingia  Jannah Pamoja Na Ummah Wake

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa wa kwanza kuingia Jannah (Peponi):

 

 

عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ آتِي بَابَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَسْتَفْتِحُ فَيَقُولُ الْخَازِنُ مَنْ أَنْتَ فَأَقُولُ مُحَمَّدٌ ‏.‏ فَيَقُولُ بِكَ أُمِرْتُ لاَ أَفْتَحُ لأَحَدٍ قَبْلَكَ ‏"‏مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Thaabit kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nitaufikia mlango wa Jannah Siku ya Qiyaamah, utafunguliwa kisha mlinzi wake atauliza: “Nani wewe?” Nitasema: Mimi Muhammad. Atasema: Nimeamrishwa kukufungulia wewe tu si mwenginewe kabla yako)) [Muslim]

 

 Na katika Hadiyth nyengine atakuwa wa kwanza kugonga mlango wa Jannah:

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَنَا أَكْثَرُ الأَنْبِيَاءِ تَبَعًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَنَا أَوَّلُ مَنْ يَقْرَعُ بَابَ الْجَنَّةِ ‏"‏ ‏.‏مسلم

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Miongoni mwa Manabii, mimi nitakuwa ndiye mwenye wafuasi wengi kabisa Siku ya Qiyaamah na wa kwanza kuugonga mlango wa Jannah)) [Muslim]

 

Na pia Ummah wake tutakuwa wa kwanza kuingia Jannah:

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ نَحْنُ الآخِرُونَ الأَوَّلُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَنَحْنُ أَوَّلُ مَنْ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ بَيْدَ أَنَّهُمْ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِنَا وَأُوتِينَاهُ مِنْ بَعْدِهِمْ فَاخْتَلَفُوا فَهَدَانَا اللَّهُ لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ فَهَذَا يَوْمُهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ هَدَانَا اللَّهُ لَهُ - قَالَ يَوْمُ الْجُمُعَةِ - فَالْيَوْمُ لَنَا وَغَدًا لِلْيَهُودِ وَبَعْدَ غَدٍ لِلنَّصَارَى ‏"‏ ‏.‏ البخاري ، مسلم  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sisi ni (Ummah) wa mwisho lakini ni wa kwanza siku ya Qiyaamah. Sisi ni wa kwanza kuingia Jannah ingawa wao (Mayahudi na Manaswara) walipewa Kitabu kabla yetu nasi tumepewa baada yao. Allaah Ametuongoza katika haki katika waliyokhitilafiana kwa idhini Yake. Hii ni siku (Ijumaa) waliyokhitilafiana, nasi Allah Ametuongoza nayo Hivyo watu wanatufuata kwani kesho (Jumamosi) ni siku ya Mayahudi na inayofuatia (Jumapili) ni ya Manaswara)) [Al-Bukhaariy, Muslim  na wengineo]

 

Share