Tarehe Ya Hijriy

Kibainisho Muhimu

Nasaha Na Ukumbusho Wa Swawm Ya ‘Arafah Ili Ufutiwe Madhambi Ya Miaka Miwili!

 

Nasaha Na Ukumbusho wa Swawm Ya ‘Arafah

Ili Ufutiwe Madhambi Ya Miaka Miwili!

 

Alhidaaya.com

 

Ndugu Waislamu tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kufunga Swawm siku ya 'Arafah tarehe 9 Dhul-Hijjah ambayo fadhila yake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili kwa dalili ifuatayo:  

 

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]

 

 

 

Bonyeza Hapa Upate: Fadhila Za Siku Ya 'Arafah

Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)

 

 

 

Bonyeza Hapa Upate: Ukumbusho Wa  Kutamka Maneno Bora Kabisa Siku Ya ‘Arafah

Pamoja Na Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi, Na Kuomba Du'aa,

Kuomba Maghfirah Na Kumuomba Allaah Akuache Huru Kutokana Na Moto!

 

 

Ratiba Ya ‘Ibaadah Za Kutekeleza Siku Tukufu Ya ‘Arafah

 

 

Bonyeza Hapa Upate Hukmu Ya Swawm Ya 'Arafah

Inapoangukia Ijumaa Au Jumamosi

 

 

 

Bonyeza Hapa Upate Takbira

 

 

 

 

 

 

 

Share

Tunawakumbusha Kutamka Maneno Bora Kabisa Siku Ya ‘Arafah, Kuomba Maghfirah Na Kuepushwa Na Moto!

 

Tunawakumbusha Kutamka Maneno Bora Kabisa Siku Ya ‘Arafah

Pamoja Na Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi, Na Kuomba Du'aa,

Kuomba Maghfirah Na Kumuomba Allaah Akuache Huru Kutokana Na Moto!

 

 Alhidaaya.com

 

Kwanza: Inapoingia Alfajiri ya Siku ya ‘Arafah, inapasa kutamka kwa wingi maneno yafuatayo ambayo ni maneno bora kabisa aliyoyatamka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Manabii kabla yake kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي

“Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na (maneno) yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:

لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير

Laa Ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku Walahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr. 

 

Hapana mwabudiwa wa haki  ila Allaah, Pekee, Hana mshirika, Ufalme ni Wake, na Himdi zote ni Zake Naye juu ya kila kitu ni Muweza.  [At-Tirmidhiy]

 

Pili: Siku ya ‘Arafah ni Siku ambayo Allaah ('Azza wa Jalla) Huteremka duniani kwa uteremko unaolingana na Utukufu Wake na kuwaacha huru kwa wingi waja Wake kutokana na Moto kwa dalili:

 

 عنْ عَائِشَةَ أنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "‏مَا مِنْ يَوْمٍ أَكْثَرَ مِنْ أَنْ يُعْتِقَ اللَّهُ فِيهِ عَبْدًا مِنَ النَّارِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ وَإِنَّهُ لَيَدْنُو ثُمَّ يُبَاهِي بِهِمُ الْمَلاَئِكَةَ فَيَقُولُ مَا أَرَادَ هَؤُلاَءِ"‏‏.‏

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambayo Allaah Anayoacha kwa wingi huru waja kutokana na Moto kama siku ya ‘Arafah.  Na huwa karibu kisha Anajigamba kwao kwa Malaika na Husema: Wametaka nini hawa? [Muslim]

Na katika Riwaayah nyingine:

اشْهَدُوا مَلاَئِكَتِي أَنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ. صحيح الترغيب

((“Shuhudieni Malaika wangu kwamba hakika Mimi Nimewaghufuria”)) [Swahiyh At-Targhiyb (1154)]

 

Tatu: Bakia katika 'ibaadah baada ya Swalaah ya Adhuhuri na khasa usikose baada ya Alasiri mpaka iingie Magharibi, kwa Haaj aliyejaaliwa kusimama ‘Arafah na kwa asiyejaaliwa kwenda Hajj. Lisikushughulishe jambo lolote jengine ila umdhukuru Allaah ('Azza wa Jalla) khasa kwa maneno hayo ya:

 

لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير

na kumuomba maghfirah kwa wingi, kuomba du’aa na kuomba Allaah ('Azza wa Jalla) Akuache huru kutokana na Moto pamoja na wazazi wako na ahli zako, vizazi vyako, jamaa zako, nduguzo katika Iymaan na Akutaqabalie haja zako. Wakati huo ni muhimu kabisa katika Siku hiyo tukufu ya ‘Arafah kutokana na Hadiyth ifuatayo:

      

عن عبدالله بن عمرو إنَّ اللهَ عزَ وجلَّ يباهي ملائكتَهُ عشيةَ عرفةَ بأهلِ عرفةَ فيقولُ : انظروا إلى عبادي أتوني شُعثا غُبرا

((Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Huwafakharisha watu ‘Arafah kwa Malaika Wake kuanzia mchana mpaka jioni ya ‘Arafah na Husema: “Watazameni waja Wangu wamenijia wakiwa timtimu wamejaa vumbi.”)) [Musnad Ahmad (12/42) na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1153), Swahiyh Al-Jaami’ (1868), Taz pia As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1503)

 

Bonyeza hapa upate Takbira:

 

 

 

Share

Ukumbusho Wa Takbiyr Katika Masiku Kumi Na Tatu Ya Dhul-Hijjah: Tarehe 1–13 Dhul-Hijjah

 

Ukumbusho Wa Takbiyr Katika Masiku Kumi Na Tatu Ya Dhul-Hijjah:

Tarehe 1 – 13 Dhul-Hijjah

 

Alhidaaya.com

 

 

Ndugu Waumini! Tukumbushane kuifufua Sunnah ya kuleta Takbiyr kuanzia unapoandama mwezi wa Dhul-Hijjah mpaka mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani kuanzia tarehe 1 Dhul-Hijjah mpaka 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake kutokana na dalili zifuatazo:

 

Allaah ('Azza wa Jalla) Anaamrisha:

 

لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ

((Ili washuhudie manufaa yao; na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu kwa yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo.    [Al-Hajj  28]

 

Na pia:

 

كَانَ إبْن عَمَر وَأبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّه عَنْهُما يَخْرُجَانِ إِلَى السُّوقِ فِي أَيَّامِ العَشْرِ يُكَبِّرَانِ، وَيُكَبِّرُ النَّاسُ بِتَكْبِيرِهِمَا .

Ibn 'Umar na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walikuwa wakienda sokoni katika siku kumi (za Dhul-Hijjah) na kutamka Takbiyr kwa sauti na watu wakiwaigiza. [Al-Bukhaariy]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ

Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika.  [Al-Baqarah: 203]

 

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku maalumu ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah[Al-Qurtwubiy: 3.3]

 

Takbiyr katika masiku haya matukufu ni aina mbili:[1]

 

Takbiyr Al-Mutwlaq: Za Nyakati Zote:

 

Takbiyr wakati wote mchana na usiku, mahali popote ulipo, tokea unapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na inaendelea mpaka siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah) na kumalizika baada ya kuingia Magharibi.

 

Takbiyr Al-Muqayyad: Za Kuthibitika Mahali Maalumu Na Nyakati Maalumu, Za Kukadirika:

 

Takbiyr baada ya kila Swalaah za fardhi na huanza baada ya Swalaah ya Alfajiri Siku ya 'Arafah mpaka mpaka baada ya Swalaah ya Alasiri siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah).

 

Inavyopasa kufanya Takbiyr:

 

   اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ،  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد

Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd

 

Bonyeza bango upate takbiyrah kwa sauti:

 

 

 

[1] Takbiyr hizo za masiku haya matukufu zimetekelezwa na baadhi ya Maswahaba watukufu na ni Mustahabb (imependekezwa) na wengi katika Salaf wa madhehebu ya Hanbaliy, Ash-Shaafi’iyy, Hanafiy na wengineo kama ifuatavyo:  

Imaam An-Nawawiy - Al-Majmuw’ (5/32).

Ibn Rajab - Fat-hul-Baariy (6/125, 130).

Ibn Taymiyyah - Majmuw’ Al-Fataawaa (24/220. 222).

Imaam Ibn Baaz - Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (13/355).

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Ash-Sharh Al-Mumti’ (5/166), Majmuw’ Fataawaa wa Rasaail Al-‘Uthyamiyn (16/262, 265).

 

Share

Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah - 01 - 10 Dhul-Hijjah

 

 

Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah:  1 - 10 Dhul-Hijjah

 

Alhidaaya.com

 

Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo ‘amali njema huwa na thawabu nyingi mno. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa mbele ya Allaah ambazo 'amali yoyote inayotendwa humo ni yenye kupendwa mno na Allaah:     

        

عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ)) يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ قَاُوا:  يَا رَسُولَ اللَّهِ وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟  قَالَ: ((وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْ)) البخاري

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah kama (‘amali zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Je, hata kuliko kupigana jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyetoka (kwenda kupigana jihaad) mwenyewe na mali yake kisha kisirudi chochote katika hivyo.” [Al-Bukhaariy]

 

Ee ndugu Muislamu! Usiache fursa hii kukupita kujichumia thawabu tele kutokana na uzito wa malipo katika masiku haya. Hivyo basi tunawanasihi kusoma yafuatayo kuhusu fadhila za masiku haya kumi ya Dhul-Hijjah pamoja na amali za kutenda katika masiku haya matukufu kabisa mbele ya Allaah ('Azza wa Jalla):

 

Bonyeza Endelea...

 

 

Share

12-Dhul-Hijjah: Mafunzo Katika Miezi Ya Hijri: Ya Kutekeleza Na Ya Kujiepusha

 

12-Dhul-Hijjah

Mafunzo Mbalimbali Ya Hajj

Mafunzo Katika Miezi Ya Hijri: Ya Kutekeleza Na Ya Kujiepusha

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 

Ukumbusho Wa Mas-ala Ya Hajj

 

 

Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayenuia Kuchinja

 

 

 

Ukumbusho Wa Takbiyr Katika Masiku Kumi Na Tatu Ya Dhul-Hijjah: Tarehe 1–13 Dhul-Hijjah

 

 

Tunawakumbusha Kutamka Maneno Bora Kabisa Siku Ya ‘Arafah, Kuomba Maghfirah Na Kuepushwa Na Moto!

 

 

Nasaha Na Ukumbusho Wa Swawm Ya ‘Arafah Ili Ufutiwe Madhambi Ya Miaka Miwili!

 

 

 

Katazo La Swiyaam (Funga) Ayyaamut-Tashriyq: 11, 12, 13 Dhul-Hijjah Na Amali Za Kutenda

 

 

 

Nasiha

 

 

Umuhimu Wa Kukimbilia Kutekeleza Nguzo Ya Hajj  

 

 

Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah - 01 - 10 Dhul-Hijjah

 

 

Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja) – Hajj

 

 

Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake

 

Amali Za Kutenda Ayyaamut-Tashriyq: Tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah Na Katazo La Swiyaam

 

 

Mdhukuru Allaah Kwa Wingi Na Omba Maghfirah Baada Ya Kutenda Mema Katika Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah

 

 

Ratiba Ya ‘Ibaadah Za Kutekeleza Siku Tukufu Ya ‘Arafah

 

 

Vitabu:

 

 

 

 

 

http://www.alhidaaya.com/sw/swahiy_fiqh_as_sunnah

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Hajj Na 'Umrah

 

 

 

 

 

 

Fataawaa Za 'Ulamaa:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah: Anayetia Niyyah Kuchinja Asikate Au Kunyoa Nywele Au Kukata Kucha

 

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah: Nani Wa Kujizuia Kukata Nywele Na Kucha Katika Kuchinja (Udhwhiyah)?

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Udhwhiyah (Kuchinja) Ni Sunnah Iliyosisitizwa Kwa Mwenye Uwezo

 

 

Imaam Ibn Baaz - Vipi Kuigawa Nyama Ya Udhw-hiyah

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuigawa Nyama Ya Udhw-hiyah Kama Zawadi Au Swadaqah Iwe Freshi Si Ya Kupikwa

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Masharti Ya Udhwhiyah Ni Yepi?

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Haijuzu Kumpa Mchinjaji Wa Udhw-hiyah Nyama Kama Ujira Wake

 

 

 

Imaam Ibn Baaz - Hukmu Ya Kuchinja Kwa Kutumia Mkono Wa Kushoto

 

 

 

Al-Lajnah Ad-Daa'imah: Hukmu Ya Kumuita Mtu Aliyetoka Kuhiji Jina La “Haji”

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kujiita Au Kuitwa “Haji Fulani”

 

 

 

Kauli Za Salaf:

 

 

Imaam Ibn Hajar: Sababu Za Utukufu Wa Masiku Kumi Ya Dhul-Hijjah

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Chukua Fursa Kutenda Mema Masiku Kumi Dhul-Hijjah

 

 

 

Makala:

 

 

 

 

Mashairi:

 

 

Tufanye Mema Kwa Wingi, Siku Kumi Dhul-Hijjah

 

Hija Yao Taqabali, Tunakuomba Jalali

 

Twamshukuru Manani, Wamehiji Kwa Salama

 

 

 

Zingatio:

 

Zingatio: Rabb Awatakabalie Hijjah Zao Pamoja Na Sisi Kughufuriwa Madhambi Yetu

 

Zingatio: Hijjah Wajibu Wetu

 

Zingatio: Siku Kumi Tukufu Za Dhul-Hijjah

 

 

 

Maswali Na Majibu:

 

 

 

 

Uzushi Wa Unoadaiwa Ni Fadhila Za Siku Kumi Za Dhul-Hijjah

 

 

Kuzuia Kukata Nywele Na Kukata Kucha Ni Kwa Familia Nzima Au Kwa Mtu Mmoja Anayechinja Au Kugharamia Uchinjaji?

 

 

Fadhila Za Siku Ya ‘Arafah, Sababu Zake Na Tofauti Ya Nyakati Baina Ya Nchi

 

 

Dhul-Hijjah: Haifai Kufunga (Swawm) Ayyamut-Tashriyq (Masiku ya 11-13 Dhul-Hijjah)

 

 

Dhul-Hijjah: Inafaa Kufunga (Swawm) Siku Zote 9 Za Dhul-Hijjah?

 

 

Dhul-Hijjah: Inafaa Kulipa Deni La Ramadhwaan Pamoja Na Niyyah Ya Swawm Za Naawafil Kama Dhul-Hijjah?

 

 

Dhul-Hijjah: Kauli Za 'Ulamaa Kuhusu Hadiyth Za Mama Wa Waumini Za Swiyaam Siku 9 Dhul-Hijjah

 

 

Dhul-Hijjah: Nini Sababu Ya Swawm Ya 'Arafah?

 

 

Dhul-Hijjah: Swawm Ya 'Arafah Ipi Sahihi Kuwafuata Hujaji Au Kufuata Nchi Uliyoko?

 

 

Hukmu Ya Swawm Ijumaa Ikiwa Ni Siku Ya 'Arafah Au 'Aashuraa

 

 

 

 

 

 

 

Share