059-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hashr Aayah 09: ‏وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

059-Suwrah Al-Hashr: Aayah 9

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٩﴾

9. Na wale waliokuwa na masikani (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao, na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa (Muhaajiriyn), na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [Al-Hashr: 9]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ دَاوُدَ، عَنْ فُضَيْلِ بْنِ غَزْوَانَ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَجُلاً، أَتَى النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَبَعَثَ إِلَى نِسَائِهِ فَقُلْنَ مَا مَعَنَا إِلاَّ الْمَاءُ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏"‏ مَنْ يَضُمُّ، أَوْ يُضِيفُ هَذَا‏"‏‏.‏ فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ أَنَا‏.‏ فَانْطَلَقَ بِهِ إِلَى امْرَأَتِهِ، فَقَالَ أَكْرِمِي ضَيْفَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ مَا عِنْدَنَا إِلاَّ قُوتُ صِبْيَانِي‏.‏ فَقَالَ هَيِّئِي طَعَامَكِ، وَأَصْبِحِي سِرَاجَكِ، وَنَوِّمِي صِبْيَانَكِ إِذَا أَرَادُوا عَشَاءً‏.‏ فَهَيَّأَتْ طَعَامَهَا وَأَصْبَحَتْ سِرَاجَهَا، وَنَوَّمَتْ صِبْيَانَهَا، ثُمَّ قَامَتْ كَأَنَّهَا تُصْلِحُ سِرَاجَهَا فَأَطْفَأَتْهُ، فَجَعَلاَ يُرِيَانِهِ أَنَّهُمَا يَأْكُلاَنِ، فَبَاتَا طَاوِيَيْنِ، فَلَمَّا أَصْبَحَ، غَدَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ‏"‏ ضَحِكَ اللَّهُ اللَّيْلَةَ ـ أَوْ عَجِبَ ـ مِنْ فَعَالِكُمَا‏"‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ ‏((‏وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ‏))

Ametuhadithia Musaddad, ametuhadithia ‘Abdullaah bin Daawuwd toka kwa Fudhwayl bin Ghazawaan toka kwa Abiy Haazim toka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ya kwamba mtu mmoja alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akapeleka taarifa kwa wakeze (kuwauliza kama kuna chochote) nao wakasema, hatuna chochote isipokuwa maji tu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Nani atamchukua, au atamkaribisha huyu kwake? Mtu mmoja wa ki-Answaar akasema: Mimi. Akaondoka naye hadi kwa mkewe. Akamwambia: Mkirimu mgeni wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akamwambia: Hatuna kitu isipokuwa chakula cha wanangu. Akamwambia: Tayarisha chakula chako, halafu washa taa yako, na uwalaze watoto wanapotaka chakula. Akatayarisha chakula chake, akaiwasha taa, na akawalaza watoto. Halafu akajifanya kama vile anaiweka sawa taa yake akaizima. Wakaanza kumwonyesha kama wanakula, na wakalala bila kitu tumboni. Kulipopambazuka, alikwenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akamwambia: Allaah Alicheka usiku, - au Alifurahia - kitendo chenu. Hapo Allaah Akateremsha:

 

‏((‏وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ‏))‏

Na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

[Al-Bukhaariy]

 

حَدَّثَنَا أَبُو كُرَيْبٍ، مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلاَءِ حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، عَنْ فُضَيْلِ بْنِ غَزْوَانَ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ،‏‏ أَنَّ رَجُلاً، مِنَ الأَنْصَارِ بَاتَ بِهِ ضَيْفٌ فَلَمْ يَكُنْ عِنْدَهُ إِلاَّ قُوتُهُ وَقُوتُ صِبْيَانِهِ فَقَالَ لاِمْرَأَتِهِ نَوِّمِي الصِّبْيَةَ وَأَطْفِئِي السِّرَاجَ وَقَرِّبِي لِلضَّيْفِ مَا عِنْدَكِ - قَالَ - فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ‏))

Ametuhadithia Abuu Kurayb Muhammad bin Al-‘Alaa, ametuhadithia Wakiy’i kutoka kwa Fudhwayl bin Ghaz-waan kutoka kwa Abuu Haazim kutoka kwa Abuu Hurayrah kwamba mgeni alilala nyumbani kwa mtu mmoja katika Maanswaar, na kwake hakuwa na chochote isipokuwa chakula chake na chakula cha wanawe. Akamwambia mkewe: Walaze watoto, kisha izime taa, halafu sogeza (chakula) ulichonacho – Amesema - Ikashuka Aayah hii:

 

((وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ‏))

na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji.  

[Muslim]

 

Share