Imaam Ibn Taymiyyah: Kung’ang’ania (Ta’asswub) Kumpenda Imaam Mmoja Na Kuwacha Wengine

 

Kung’ang’ania (Ta’asswub) Kumpenda Imaam Mmoja Na Kuwacha Wengineo

 

Imaam Ibn Taymiyyah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Amesema Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

 

Atakayekuwa na ta’asswub (kung’ang’ania) kumpenda mmoja kati ya Maimamu akawaacha wengineo ni kama vile kafanya ta’asswub kwa Swahaba mmoja na kawaacha wengine.

 

 

Mtu huyo atakuwa ni kama Raafidhw (Shia) ambae ana ta’asswub na 'Aliy akawaacha Makhalifa Watatu (wengine) na akaacha pia jamii ya Maswahaba wengineo.

 

 

Mtu huyo atakuwa ni kama Khaarij  ambaye  anamtusi 'Uthmaan na 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhumaa).

 

 

Basi hizi ni njia za watu wa bid'ah na matamanio ambao zimethibiti hoja zake katika Kitabu na Sunnah na Ijmaa' wakakemewa  kuwa wametoka nje ya Shariy'ah na Manhaj ambayo ametumwa nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Kwa hiyo, atakayefanya ta’asswub na yeyote katika Maimaam akawaacha wengine basi atakuwa amefanana na hao (waliotajwa). Ni sawa sawa ikiwa atafanya ta’asswub kwa (Imaam) Maalik au kwa Ash-Shaafi'iy au kwa Abuu Haniyfah au kwa Ahmad au wengineo.

 

 

Kisha kiwango cha mwenye kuta’asswub kwa mmoja kati ya hao (Maimaam) anakuwa ni mjinga kwa kukadiriwa elimu yake na Dini yake, na mbele ya watu wengineo anakuwa ni mjinga na dhalimu, na Allaah Anaamrisha watu kushikamana na ‘ilmu na uadilifu, na Anakataza ujinga na dhulma.

 

 

[Majmuw' Al-Fataawaa 2/253]

 

Share