10-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akipata Matone Ya Damu Usiku Ambayo Mara Huwa Ni Hedhi Na Mara Si Hedhi Nini Hukmu Ya Swawm?

10-Akipata Matone Ya Damu Usiku Ambayo Mara Huwa Ni Hedhi Na Mara Si Hedhi

Nini Hukmu Ya Swawm?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mara nyengine mwanamke anaona athari ndogo ya damu au nukta au tone katika  nyakati za siku. Mara nyengine huonekana akiwa ada yake wakati huo kabla ya kushuka, na wakati mwingine sio wakati wa ada yake. Ni nini hukumu ya Swawm yake katika hali zote mbili?

 

 

JIBU:

 

Jibu la swali hili nilishalijibu mapema. Kilichobakia ni kuwa ikiwa kuna nukta katika siku zake za hedhi na inaonekana ni damu ya hedhi anayoijua basi itakuwa ni hedhi.

 

 

 

Share