Al-Lajnah Ad-Daaimah: Aashuraa: Kinachowajibika Siku Ya 'Aashuraa Je Inawajibika Zakaatul-Fitwr?
Kinachowajibika Siku Ya 'Aashuraa Na Je, Inawajibika Zakaatul-Fitwr?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nini kinachowajibika kwa Muislamu kufanya siku ya ‘Aashuraa? Na je Zakaatul-Fitwr inawajibika siku hiyo?
JIBU:
Imewajibika kwa Musilamu Swawm siku ya ‘Aashura kama ilivyothibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha Swawm siku ya ‘Aashuraa. Lakini Swawm ya Ramadhwaan ilipofaridhishwa, ikawa ni khiari mtu kufunga ‘Aashuraa aliyependa afunge na asiyependa asifunge.
Na hakuna Zakkatul-Fitwr siku ya ‘Aashuraa kama ilivyo katika ‘Iydul-Fitwr baada ya mwezi wa Ramadhwaan .
Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah 10/400 Fatwa namba 10962]