Al-Lajnah Ad-Daaimah: Aashuraa: Bid’ah Zake: Kuwachinjia Maiti, Mikusanyiko Ya Visomo

 

 

Miongoni Mwa Bid’ah Za ‘Aashurah Ni Kuchinja Kwa Ajili Ya Waliofariki

Na Kukusanyika Kusoma Qur-aan

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Kuna makaburi ya mawalii ambayo kila ikifika ‘Aashuraa huchinjwa mbuzi 40 na zaidi ya ng’ombe 10. Waislamu makhurafi hukutana na husoma Qur-aan kwa jina la du’aa za wafu kisha wanakula nyama za vichinjwa hivi. Shaykh tunaomba Fatwa na dalili ya masuala haya.

 

 

JIBU:

 

 

Kwanza: Ulichokitaja cha kuchinja vichinjwa katika makaburi ya mawalii ni shirki na wanaofanya hivyo wamelaaniwa kwa sababu ni vichinjwa vimechinjwa na kukusudiwa asiyekuwa Allaah. Imethibitika kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Amemlaani anayechinja kwa asiyekuwa Allaah.” Na kwa hili haifai kula mbuzi au ng’ombe waliochinjwa katika makaburi ya mawalii.

 

 

Pili: Kusoma Qur-aan kwa ajili ya wafu ni bid’ah iliyozushwa kwani imethibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kuwa amesema: “Atakayezusha katika jambo letu hili (Dini) kisichokuwepo basi hurejeshwa.”

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-‘Ilimiyyah Wal Iftaai, Mjeledi wa kwanza Swali la 2 na 3, Fatwa namba 6208].

 

Share