Skip to main content

Fataawaa: Udhwhiyyah (Kuchinja)07-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kukopa kwa Ajili ya Udhwhiya Inafaa?

Kukopa kwa Ajili ya Udhwhiya Inafaa?

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Fakiri ambaye hana chochote mkononi pindi 'Iydul-Adhw-haa  inapofika lakini ni mwenye kutarajia kupokea mshahara wake wa mwezi basi na akope achinje kisha alipe?

JIBU:

Kama hatoweza kulipa kwa muda wa karibu basi haifai kwake kukopa ili achinje kwani hili litamfanya ashughulike na kulipa deni.

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/110)]