52-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Alikuwa Katika Nifaas Akatekeleza Nguzo Zote Isipokuwa Twawaaf Na Sa’y Akahisi Ametoharika Akamilishe Twawaaf Al-Ifaadhwah?

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

51-Alikuwa Katika Nifaas Akatekeleza Nguzo Zote Isipokuwa Twawaaf Na Sa’y 

Akahisi Ametoharika Akamilishe Twawaaf Al-Ifaadhwah?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

 

Mwanamke mwenye nifaas atakapoanza nifaas yake siku ya Tarwiyah na kukamilisha nguzo za Hajj isipokuwa Twawaaf na Sa’y ila akaona kuwa ‘kuna ishara za awali’ kuwa ametoharika baada ya kupita siku kumi. Je, atajitoharisha na na kuoga na kukamilisha nguzo iliyobakia ambayo ni Twawaaf Ya Hajj?   

 

 

JIBU:

 

Hapana haijuzu kwake kukoga na kutufu hadi ahakikishe kwa yakini kabisa tohara yake. Kinachofahamika katika swali hili hapa ni kuwa ‘kuna ishara za awali’  ni kuwa bado hajaona utohara kwa ukamilifu wake,  hivyo hapana budi kwanza aone tohara kwa ukamilifu wake na muda wa kuwa atakuwa ametoharika basi na akoge na atekeleze Twawaaf na Sa’yi. Akipata wasaa kabla ya Twawaaf basi hamna neno; kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu Hijjah kwa Yule aliyefanya Sa’y kabla ya kutufu akasema: “Si vibaya.”

 

 

Share