Chapati - 1

Chapati - 1

Vipimo

Unga mweupe wa ngano vikombe 4

Samli safi vijiko 3 vya kulia

Chumvii kijiko 1  chai

Maji vuguvugu (warm) vikombe 2

Samli ya kupikia chapati

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja.
  2. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
  3. Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano hivi.
  4. Finika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi hivi kwa kuufunika ili hewa isiingie.
  5. Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo.
  6. Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
  7. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
  8. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
  9. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.
  10. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.
  11. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
  12. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi

      13. Pika chapati kwenye frying pan moto wa kiasi. Ikiiva  upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress  na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha kulia cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri.

      14. Endelea namna hii huku unafuta frying pan na kitambaa  kisafi au karatasi za jikoni (tissue) baada ya  kila chapatti.

Kidokezo

  1. Unapomaliza kuzipika kila moja, zitandaze kwanza chapati katika sahani (au sinia) kubwa zipate kupoa ziwe kavu ili zisinyonyanye mafuta. Kisha tena ziweke katika sahani yako ya kawaida.
  2. Ni nzuri kutolea  na jam au asali

 

       3. Unaweza ku freeze chapati katika Freezer bags.  Kunja chapati  moja moja ziwe nusu.  Zifunike na Wax paper, kisha zitie kwenye freezer bags na uzihifadhi katika freezer.  Unapotaka kula, toa kwenye freezer na upashe moto katika Microwave. 

 

 

 

Share