07-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Akifunga Jiwe Tumboni Mwake Kwa Sababu Ya Njaa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

07-Zuhd Yake: Akifunga Jiwe Tumboni Mwake Kwa Sababu Ya Njaa

 

Alhidaaya.com

 

 

Njaa ni jambo gumu mtu kulivumilia kwani huenda likampeleka mtu kula yaliyokuwa ya haraam pindi akikosa chakula. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifunga tumbo lake kwa kitambaa ili kuzuia njaa:

 

عن أَنَس بْن مَالِكٍ قال:  جِئْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمًا فَوَجَدْتُهُ جَالِسًا مَعَ أَصْحَابِهِ يُحَدِّثُهُمْ وَقَدْ عَصَّبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ ، قَالَ أُسَامَةُ وَأَنَا أَشُكُّ  عَلَى حَجَرٍ ، فَقُلْتُ لِبَعْضِ أَصْحَابِهِ:  لِمَ عَصَّبَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَطْنَهُ؟ فَقَالُوا: مِنَ الْجُوعِ ‏.‏ فَذَهَبْتُ إِلَى أَبِي طَلْحَةَ وَهُوَ زَوْجُ أُمِّ سُلَيْمٍ بِنْتِ مِلْحَانَ فَقُلْتُ يَا أَبَتَاهُ ، قَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَصَّبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ فَسَأَلْتُ بَعْضَ أَصْحَابِهِ فَقَالُوا مِنَ الْجُوعِ ‏.‏ فَدَخَلَ أَبُو طَلْحَةَ عَلَى أُمِّي فَقَالَ هَلْ مِنْ شَىْءٍ فَقَالَتْ نَعَمْ عِنْدِي كِسَرٌ مِنْ خُبْزٍ وَتَمَرَاتٌ فَإِنْ جَاءَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَحْدَهُ أَشْبَعْنَاهُ وَإِنْ جَاءَ آخَرُ مَعَهُ قَلَّ عَنْهُمْ ‏.‏  

Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema:  Nilimtembelea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku moja na nikamkuta amekaa pamoja na Swahaba zake akiongea nao, na alikuwa amejifunga tumbo lake kwa kitambaa. Usaamah alisema: “Nina shaka kama kulikuwa na jiwe juu yake (tumbo lake) au la. Niliuliza baadhi ya Swahaba zake: Kwanini Rasuli amejifungakitambaa tumboni mwake?” Wakasema: “Kutokana na   njaa.” Nikaenda kwa Abuu Twalhah ambaye ni mume wa Umm Sulaym binti Milhaan, nikamwambia: “Ee Baba, nimemuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amefunga tumbo lake kwa kitambaa. Nikawauliza baadhi ya Swahaba zake wamesema ni kwa sababu ya njaa. Hapo Abuu Twalhah akamwendea mama yangu akamuuliza: “Je kuna chochote cha kula?” Akasema: “Naam nnavyo vipande vya mkate na baadhi ya tende. Atakapotujia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  pekee yake tutaweza kumpa na vitamshibisha, lakini   ikiwa atakuja pamoja wenginewe basi havitawatosheleza.”   [Muslim]

 

Na alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiomba du’aa ifuatayo ya kujikinga na njaa:

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْجُوعِ فَإِنَّهُ بِئْسَ الضَّجِيعُ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخِيَانَةِ فَإِنَّهَا بِئْسَتِ الْبِطَانَةُ

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na njaa kwani hiyo ni mbaya mno kulala nayo, na najikinga Kwako khiyana kwani hiyo ni dhamira ovu. [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Swahiyh An-Nasaaiy (3/1112)]

 

Na miongoni mwa mambo matatu aliyoyaomba katika Hadiyth mojawapo, amwaombea Ummah wake wasiangamizwe kwa sababu ya njaa:

 

قَالَ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ سَأَلْتُ رَبِّي ثَلاَثًا فَأَعْطَانِي ثِنْتَيْنِ وَمَنَعَنِي وَاحِدَةً سَأَلْتُ رَبِّي أَنْ لاَ يُهْلِكَ أُمَّتِي بِالسَّنَةِ فَأَعْطَانِيهَا وَسَأَلْتُهُ أَنْ لاَ يُهْلِكَ أُمَّتِي بِالْغَرَقِ فَأَعْطَانِيهَا وَسَأَلْتُهُ أَنْ لاَ يَجْعَلَ بَأْسَهُمْ بَيْنَهُمْ فَمَنَعَنِيهَا ‏"‏ ‏

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nilimuomba Rabb Wangu mambo matatu, Amenipa mawili, na Amenikatalia moja. Nilimuomba Rabb wangu Asiuangamize Ummah wangu kwa sababu ya njaa, Akanitakabalia hili, nikamuomba Ummah wangu usiangamizwe kwa kugharikishwa (mafuriko) Akanitakabalia hili,  na nikamuomba Rabb wangu  kwamba kusimwagwe  damu yoyote miongoni mwa watu wa Ummah wangu, lakini Hakunitakabalia hili.”  [Muslim]

 

Share