Mchuzi Wa Kamba

Mchuzi Wa Kamba
 

Vipimo 

Viazi (mbatata) -  2

Kamba -  1 Lb                

Vitunguu -   2

Nyanya -  2

Pilipili hoho (green pepper) -  1

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai

Tangawizi - 1 kijiko cha chai

Uzile (bizari ya pilau ya unga-Jiyra) - ½ kijiko cha chai

Pilipili manga -  ½ kijiko cha chai

Pilipili ya unga -  ½ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo -  ½ kijiko cha chai

Chumvi -  kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha

 1. Changanya kamba na  thomu, tangawizi, pilipili manga, pilipili ya unga, jira na chumvi.
 2. Katakata vitunguu weka pembeni.
 3. Katakata pilipili hoho weka pembeni.
 4. Katakata Nyanya weka pembeni.
 5. Menya viazi na uvikate vidogo vidogo.

Namna Ya Kupika 

 1. Kaanga kamba mpaka wabadilike rangi, watie kwenye bakuli.
 2. Kaanga viazi mpaka viwive na vibadilike rangi, vitoe, mimina kwenye bakuli.
 3. Kaanga pilipili hoho viwive na vibadilike rangi, vitoe.
 4. Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi, mimina nyaya kaanga pamoja, kisha tia nyanya ya kopo na chumvi.
 5. Endelea kukoroga.
 6. Mimina maji kama robo kikombe, ukishawiva vizuri, mimina katika bakuli la mchanganyiko na ukoroge kidogo ili vichanganyike tayari kwa kuliwa.

 

 

 

 

Share