10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Godoro Na Mto Wake Ulikuwa Duni

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

10-Zuhd Yake Godoro Na Mto Wake Ulikuwa Duni

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth zifuatazo zinaelezea kuhusu godoro na mto aliokuwa akilalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): 

 

عن عَائِشَةَ، قَالَتْ كَانَ وِسَادَةُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الَّتِي يَتَّكِئُ عَلَيْهَا مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ ‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba “Mto wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  aliokuwa akiulalia ulitengenezwa kwa ngozi ya mnyama iliyojazwa magamba ya mtende. [Muslim]

 

 Na Hadiyth ndefu ya ‘Umar bin Al-Khatwwaab (رضي الله عنه) pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipojitenga mbali na wakeze:

 

“…Mlangoni wa chumba chake kulikuwa na mtumwa, ambaye nilikwenda kwake, nikamwambia: “Niombee ruhusa kwake ili niweze kuingia”. Akaniruhusu na nikaingia ili kumuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akiwa amejinyoosha juu ya jamvi lililoacha alama ubavuni mwake. Chini ya kichwa chake kulikuwa na mto wa ngozi, ndani yake mna usumba na kulikuwa na ngozi zilizokuwa zimetundikwa na majani kwa ajili ya kutengeneza ngozi. [Al-Bukhaariy]

 

Na pia kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Mto wake aliokuwa akilalia usiku, ulikuwa ni wa ngozi uliojazwa ufumwele.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuwd (4146) na At-Tirmidhiy. Iko katika Swahiyhul Jaami’i (4714)].

 

Na kuhusu godoro lake:

 

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ فِرَاشُ رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ أُدْمٍ حَشْوُهُ لِيفٌ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Godoro la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi iliyotiwa magamba ya mtende." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share