Vilosa

Vilosa

 

 

Vipimo

Mchele - 1/2 Kikombe

Semolin - 1 Vikombe

Tui  la nazi - 3/4  Kikombe

Maziwa - 1/2 Kikombe

Mayai - 3

Hamira - 1 kijiko cha chai kijae

Rose essence - kidogo

Zaafarani - kidogo

Sukari - 1 kijiko cha chai

 

Namna ya kutayarisha na kutengeneza

  1. Roweka  mchele  tokea usiku
  2. Uchuje mchele maji yote
  3. Weka kwenye mashine ya kusagia (Blender)
  4. Tia mayai, maziwa, sukari, hamira , rose essence, zaafarani. Kasha usagesana mpaka chenga za mchele zote zisagike.
  5. Tia semolina na tui la nazi, kasha endelea kusaga katika blender, kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
  6. Mimina katika bakuli kubwa, funika iwache iuumuke.
  7. Ikishaumuka choma kama unavyochoma vitumbua.
  8. Shira ikipowa, tumbukiza Vilosa kwa kiasi kiasi , changanya na uvitoe  uviweke upande katika sahani ya kupakulia.
  9. Endelea kufanya mpaka vyote vimalizike.

Shira :  Tengeneza mapema ipowe. Na isiwe nzito

Sukari - 2 Vikombe

Maji - 1 kikombe

Zaafarani - kidogo

Rose - Essence

 

 

 

Share