039-Asbaabun-Nuzuwl: Az-Zumar Aayah 23-26: اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

039-Asbaabun-Nuzuwl Az-Zumar Aayah 23 - 26

 

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾ أَفَمَن يَتَّقِي بِوَجْهِهِ سُوءَ الْعَذَابِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ وَقِيلَ لِلظَّالِمِينَ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٢٤﴾ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٥﴾ فَأَذَاقَهُمُ اللَّـهُ الْخِزْيَ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara, zinasisimua kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainisha ngozi zao na nyoyo zao katika kumdhukuru Allaah. Huo ndio mwongozo wa Allaah Humwongoza kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa. Je, yule anayekinga kwa uso wake adhabu mbaya Siku ya Qiyaamah (ni sawa na atayesalimika nao?). Na madhalimu wataambiwa: Onjeni yale mliyokuwa mkiyachuma. Wamekadhibisha wale wa kabla yao, basi (Allaah) Akawaletea adhabu kutoka mahali wasipotambua. Allaah Akawaonjesha hizaya katika uhai wa dunia na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi, lau kama wangelikuwa wanajua. [Az-Zumar (39:23 - 26)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

  قال سعد بن أبي وقاص قال أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم : لو حَدَّثْتَنا ، فأنزل الله عز وجل : " اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ " 

 

Sa-’ad bin Abiy Waqqaasw amesema: Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walimwambia Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم): Tunatamani utuhadithie khabari, Allaah (عز وجل)  Akateremsha:

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa. [Az-Zumar (39:23)]

 

فقالوا : لو قصصت علينا فنزل نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ 

 

Wakasema: Tuna hamu utusimulie kisa, ikateremka:

 

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa. [Yuwsuf (12:3)]

 

فقالوا : لو ذكَّرتنا فنزل أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ   

Wakasema: Tungependa utukumbushe, ikateremka:

 

ألَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ

Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah. [Al-Hadiyd (57:16)]”

 

وعن ابن مسعود رضي الله عنه أن أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم مَلُّوا ملة ، فقالوا له : حَدِّثْنا فنزلت

 

Na toka kwa Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه)  kwamba Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  waliboeka sana, wakamwambia Rasuli: Tupashe khabari, na Aayah ikateremka.

 

 

Al-Qurtwubiy katika Tafsiyr yake ameandika: “Kauli Yake (سبحانه وتعالى):

 

 

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara, zinasisimua kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainisha ngozi zao na nyoyo zao katika kumdhukuru Allaah. Huo ndio mwongozo wa Allaah Humwongoza kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa….Al-Qurtubiy anatuambia:

 

 

Maana za Kauli Zake (سبحانه وتعالى):

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa. [Az-Zumar (39:23)]..

 

Ni kuwa makusudio ya kauli nzuri kabisa hapa ni Al-Qur-aan.

 

Na Aliposema:

 

فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُ

Wakafuata yaliyo mazuri yake zaidi. [Az-Zumar(39:18)]

 

Ni kuwa Anabainisha kuwa kizuri zaidi kinachosikilizwa na kutekelezwa ni kile Alichokiteremsha Allaah, nayo ni Al-Qur-aan.

 

 

 

 

Share