06-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hakuwa Akiwakaripia Watoto Wala Watumishi Wake

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

06-Upole Wake: Hakuwa Akiwakaripia Watoto Wala Watumishi Wake

 

Alhidaaya.com

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa mwema kwa Watoto, akiwafahamu hisia zao, akiwahimiza kufanya mema na kuwafundisha maadili mema, akiwahimiza katika kuhudhuria Swalaah za jamaa na akiwanasihi na akisikiliza ushauri wao. Pia Watoto walipokosea hakuwakaripia wala kuwadharau au kuwatenga; mfano ni Anas bin Maalik (رضي الله عنه) ambaye alimhudumia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nyumba yake ambako aliishi naye kuanzia Hijrah mpaka kufariki kwake alisema:

 

خَدَمْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَشْرَ سِنِينَ، فَمَا قَالَ لِي أُفٍّ‏.‏ وَلاَ لِمَ صَنَعْتَ وَلاَ أَلاَّ صَنَعْتَ‏.‏

Nimemtumikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) miaka kumi (10), hakuniambia hata Uff (ni sauti inayoonyesha kughsika) na wala kunikaripia kwa kuniambia, “Kwa nini ulifanya hivi? Au kwa nini usifanye hivi!?” [Al-Bukhaariy]

 

   

 

Share