Uzushi Wa Swalah Za Usiku
Uzushi Wa Swalah Za Usiku
Assalaamualaykum Ndugu Zangu,
Mimi Siku Zote Naamka Saa Nane Za Usiku --- Yaani Na Amshwa Naturally.
Nina Sali Kwa Mpango Ufuatao:
I. Sunnatil-udhuu Rakaa 2
II. Sunnati Rasulullah (s.a.w.) Rakaa 2
III. Thajjud Rakaa 2
IV. Sunna Ya Usiku Ule Raka ....kama Ilvyoandikwa
V. Sunnati Hajjat Rakaa 2 ,2,2, Mujibu Wa Haja Zangu.
VI.
Sunnati Tawba Rakaa 2
VII. Salaatul Witr Rakaa 3.
By The Time Nimewahi Zote Swalah Ya Fajr Ni Tayari. Na Endelea Kufanya Zikrullah Baada Ya Swalah Ya Fajr Mpaka Time Ya Ishraaq Na Tena Naendelea Kuwepo Kwenye Msala Kwa Zikrullah Mpaka Swalah Ya Dhuhaa.
Jee Ni Fafanulieni Wapi Nimekosea Na Nifanye Sahihi Namna Gani
Jazaakallahukheir Fiiamaanillah
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hakika hili ni jambo muhimu sana kwa kila Muislamu kwani katika kufanya ibada yoyote ikiwa ya vitendo au kauli, lazima masharti mawili yapatikane ndipo ibada hiyo ikubaliwe nayo ni:
1) Ikhlaas – Iwe kwa kutaka Ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na sio yenye Riyaa au sio yenye kutendeka kwa ajili ya maslahi ya kidunia.
2) Iwe inatokana na mafundisho ya Qur-aan na Sunnah. (kufanyika kwa mujibu wa mafunzo ya Qur-aan na Sunna sahihi).
Bila ya shaka sharti la kwanza dada yetu na wengi wetu tunalitimiza. Ama sharti la pili ndio baadhi yetu hatukulitambua ndipo tunapofanya ibada bila ya kupata dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah.
Tunakutajia hapa zilizo sahihi na zisizo sahihi kutokana na maelezo yako:
Swalaah |
Daraja Yake |
Dalili/Maelezo
|
Sunnatul- Wudhuu Rakaa mbili |
sahihi |
Dalili kuwa Bilaal (Radhwiya Allahu 'anhu) akiswali hata Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaota nyao zake zinatembmea Peponi kutekelza Swalaah hii kila baaya wudhuu. |
Sunnatul-Rasuul (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) |
sio sahihi |
Hakuna dalili yoyote. |
Tahajjud Rakaa 2 |
sahihi |
Unaweza kuswali mbili, au nne, au sita au nane ukamalizia na tatu za Witr
|
Sunnah ya usiku |
sahih |
Ni sawa na Tahajjud usiongeze zaidi ya hizo |
Sunnah ya Haja |
dhaifu |
Imepingwa na Maulamaa kuwa ni Hadiyth dhaifu. Muislamu anaomba haja zake kwa kuomba du'aa kama kawaida. |
Sunnah ya Tawbah |
sahihi |
Anapofanya mja dhambi anaswali Rakaa mbili kuomba maghfira |
Salaatul Witr |
sahihi |
Rakaa 3 unamalizia baada ya kuswali 8 au chini yake za Tahajjud |
Unavyomalizia kuwa inafika Alfajiri kisha unaendelea kufanya dhikru-Allah hadi litoke jua kisha unaswali Swalah ya Dhuhaa ni sawa kabisa na fadhila zake ni kupata thawabu kama vile umetimiza Hajj na Umra kamili kutona na Hadiyth ifuatayo:
((عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال : من صلى الفجر في جماعة ثم قعد يذكر الله حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة تامة تامة) ) أخرج الترمذي صححه الألباني .
Imetoka kwa Anas kwamba Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jama'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhy na kaisahihisha Al-Albaaniy]
Tanbihi: Fadhila hizi anazipata pia mwanamke sawa sawa atakaposwali nyumbani kwake. Tunakuombe dada yetu Allaah Azidi kukuelimisha upate kuona yaliyo haki uyafuate na ujiepushe na mambo ya uzushi yote.
Na Allaah Anajua zaidi