006-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Shutuma kwa Mwenye Nyuso Mbili

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب ذمِّ ذِي الوَجْهَيْن

006-Mlango Wa Shutuma kwa Mwenye Nyuso Mbili

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ﴿١٠٨﴾

Wanajificha watu wasiwaone (wakitenda machafu) na wala hawajifichi kwa Allaah (wakamwonea haya), Naye Yu pamoja nao (kwa Ujuzi Wake) pale wanapokesha kupanga makri kwa maneno Asiyoyaridhia. Na Allaah daima kwa yale wayatendayo, Ni Mwenye Kuyazunguka (kwa Ujuzi Wake). [An-Nisaa: 108]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( تَجِدُونَ النَّاسَ مَعادِنَ : خِيَارُهُم في الجَاهِلِيَّةِ خِيَارُهُمْ في الإسْلاَمِ إِذَا فَقُهُوا ، وتَجِدُونَ خِيَارَ النَّاسِ في هَذَا الشَّأنِ أَشَدَّهُمْ كَرَاهِيَةً لَهُ ، وَتَجِدُونَ شَرَّ النَّاسِ ذَا الوَجْهَينِ ، الَّذِي يَأتِي هؤُلاءِ بِوَجْهٍ ، وَهَؤُلاءِ بِوَجْهٍ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Utawapata watu wenye nasaba nzuri wakijifakhiri kwayo: Walio bora katika ujahiliyah (zama za ujinga), ndio wanakuwa bora katika Uislamu wanapo fahamu (na kujua hukumu za kisheria). Na utawakuta walio bora katika jambo hili (la idara na uongozi) ni wenye kulichukia mno. Na utawapata wabaya zaidi miongoni mwa watu ni wale wenye nyuso mbili (wanafiki), ambao wanakuja kwa hawa kwa uso mmoja na kwa hawa kwa uso mwengine." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن محمد بن زيدٍ : أنَّ ناساً قالوا لِجَدِّهِ عبدِ اللهِ بن عمر رضي الله عنهما : إنَّا نَدْخُلُ عَلَى سَلاَطِيننَا فَنَقُولُ لَهُمْ بِخِلاَفِ مَا نَتَكَلَّمُ إِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِنْدِهِمْ . قَالَ : كُنَّا نَعُدُّ هَذَا نِفَاقاً عَلَى عَهْدِ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Zayd kuwa watu walikuja wakamwambia babu yake, 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Hakika sisi tunaingia kwa masultani wetu na kuwaambia wao kinyume na yale tunayozungumza tunapotoka kwao." Akasema: "Hakika sisi tulikuwa tukiona jambo hilo kuwa ni unafiki katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Al-Bukhaariy]

 

 

Share