008-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Ruhusa ya Kusema Uongo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب بيان مَا يجوز من الكذب

008-Mlango Wa Kubainisha Ruhusa ya Kusema Uongo

 

Alhidaaya.com

 

 

اعلَمْ أنَّ الكَذِبَ ، وإنْ كَانَ أصْلُهُ مُحَرَّماً ، فَيَجُوزُ في بَعْضِ الأحْوَالِ بِشُروطٍ قَدْ أوْضَحْتُهَا في كتاب : " الأَذْكَارِ "  ، ومُخْتَصَرُ ذَلِكَ : أنَّ الكلامَ وَسيلَةٌ إِلَى المَقَاصِدِ ، فَكُلُّ مَقْصُودٍ مَحْمُودٍ يُمْكِنُ تَحْصِيلُهُ بِغَيْرِ الكَذِبِ يَحْرُمُ الكَذِبُ فِيهِ ، وإنْ لَمْ يُمْكِنْ تَحْصِيلُهُ إِلاَّ بالكَذِبِ ، جازَ الكَذِبُ . ثُمَّ إنْ كَانَ تَحْصِيلُ ذَلِكَ المَقْصُودِ مُبَاحاً كَانَ الكَذِبُ مُبَاحاً ، وإنْ كَانَ وَاجِباً ، كَانَ الكَذِبُ وَاجِباً . فإذا اخْتَفَى مُسْلِمٌ مِنْ ظَالِمٍ يُريدُ قَتْلَهُ ، أَوْ أَخذَ مَالِهِ وأخفى مالَه وَسُئِلَ إنْسَانٌ عَنْهُ ، وَجَبَ الكَذِبُ بإخْفَائِه . وكذا لو كانَ عِندَهُ وديعَةٌ ، وأراد ظالمٌ أخذها ، وجبَ الكذبُ بإخفائها . وَالأحْوَطُ في هَذَا كُلِّهِ أن يُوَرِّيَ . ومعْنَى التَّوْرِيَةِ : أنْ يَقْصِدَ بِعِبَارَتِهِ مَقْصُوداً صَحيحاً لَيْسَ هُوَ كَاذِباً بالنِّسْبَةِ إِلَيْهِ ، وإنْ كَانَ كَاذِباً في ظَاهِرِ اللَّفْظِ ، وبالنِّسْبَةِ إِلَى مَا يَفْهَمُهُ المُخَاطَبُ ، وَلَوْ تَرَكَ التَّوْرِيَةَ وَأطْلَقَ عِبَارَةَ الكَذِبِ ، فَلَيْسَ بِحَرَامٍ في هَذَا الحَالِ .

وَاسْتَدَل العُلَمَاءُ بِجَوازِ الكَذِبِ في هَذَا الحَالِ بِحَديثِ أُمِّ كُلْثُومٍ رَضِيَ اللهُ عنها، أنها سمعتْ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( لَيْسَ الكَذَّابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ ، فَيَنْمِي خَيْراً أَوْ يَقُولُ خَيْراً )) . متفق عَلَيْهِ .

زاد مسلم في رواية : قالت أُمُّ كُلْثُومٍ : وَلَمْ أسْمَعْهُ يُرَخِّصُ في شَيْءٍ مِمَّا يَقُولُ النَّاسُ إِلاَّ في ثَلاَثٍ، تَعْنِي : الحَرْبَ ، والإصْلاَحَ بَيْنَ النَّاسِ ، وَحَديثَ الرَّجُلِ امْرَأَتَهُ ، وَحديثَ المَرْأَةِ زَوْجَهَا .

 

Jueni ya kwamba japokuwa uongo asili yake ni haramu, lakini inaruhusiwa katika baadhi ya hali kwa masharti ambayo nimeyaweka wazi katika kitabu changu cha Al-Adhkaar. Na muhtasari wa hayo ni: Hakika mazungumzo ni njia ya kufikia lengo la halali, hivyo kila lengo zuri ambalo linaweza kufikiwa kwa ukweli inakuwa ni haramu kusema uongo. Na ikiwa haliwezi kufikiwa isipokuwa kwa kusema uongo, hapo uongo unajuzu kuutumia. Kisha ikiwa kufikia lengo hilo ni mubaha, hivyo kusema uongo pia utakuwa ni mubaha na ikiwa ni wajibu, hivyo uongo itakuwa ni wajibu. Kwa mfano, ikiwa Muislamu amejificha kutokana na dhalimu ambaye anataka kumuua au kuchukua mali yake na akaficha mali yake na akaulizwa mtu kuhusu yeye, katika hilo ni wajibu kusema uongo. Na hivyo hivyo kama mtu atakuwa ameweka amana ya mtu mwengine, na dhalimu akawa anataka kuichukua hiyo amana ya mtu ni wajibu kuificha hiyo amana ya watu. Na lililo bora katika jambo hili ni kutumia Tawriyah. Na maana ya Tawriyah ni kukusudia kwa kutumia ibara ambayo lengo lake ni sahihi kwake yeye lenye maana kadha ambayo itamfanya msikilizaji kuelewa vingine na japokuwa dhahiri yake ni uongo. Na lau pia ataacha Tawriyah na kutumia ibara ya uongo moja kwa moja haitakuwa haramu katika hali hii.

 

Na wanazuoni wametoa dalili katika kujuzisha uongo katika hali hii kwa ile Hadiyth ya Umm Kulthuwm bint 'Uqbah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ya kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Si muongo yule mwenye kusuluhisha baina ya watu, hivyo kuifikia kheri au kusema maneno mazuri." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy].

 

Ameongeza Muslim katika riwaayah yake: "Amesema Umm Kulthuwm (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Na sijawahi kumsikia kuruhusu uongo katika mambo wanayozungumza watu ila katika hali tatu: yaani katika wakati wa vita, na kusuluhisha baina ya watu na mazungumzo ya mume kwa mkewe na mke kwa mumewe."

 

 

Share