035-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Riya

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم الرياء

035-Mlango Wa Uharamu wa Riya

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ ﴿٥﴾

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki [Al-Bayyinah: 5]

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ  ﴿٢٦٤﴾

Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu [Al-Baqarah: 264]

يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾

Wakijionyesha kwa watu na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu. [An-Nisaa: 142]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( قَالَ الله تَعَالَى : أنَا أغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ ، مَنْ عَمِلَ عَمَلاً أشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ )) . رواه مسلم .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Amesema Allaah Ta'aalaa: Mimi ni mkwasi kwa wenye kunishirikisha kutokana na shirki hiyo. Mwenye kufanya amali ambayo kwayo Amenishirikisha Mimi na mwengine, Nitamuacha yeye na shirki yake." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( إنَّ أَولَ النَّاسِ يُقْضَى يَومَ القِيَامَةِ عَلَيْهِ رَجُلٌ اسْتُشْهِدَ ، فَأُتِيَ بِهِ ، فَعَرَّفَهُ نِعْمَتَهُ ، فَعَرَفَهَا ، قَالَ : فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا ؟ قَالَ : قَاتَلْتُ فِيكَ حَتَّى اسْتُشْهِدْتُ . قَالَ : كَذَبْتَ ، وَلَكِنَّكَ قَاتَلْتَ لأَنْ يُقَالَ : جَرِيءٌ ! فَقَدْ قِيلَ ، ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ في النَّارِ. وَرَجُلٌ تَعَلَّمَ العِلْمَ وَعَلَّمَهُ ، وَقَرَأَ القُرآنَ ، فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا . قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا ؟ قَالَ : تَعَلَّمْتُ العِلْمَ وَعَلَّمْتُهُ ، وَقَرَأتُ فِيكَ القُرآنَ ، قَالَ : كَذَبْتَ ، وَلكِنَّكَ تَعَلَّمْتَ لِيُقَالَ : عَالِمٌ ! وَقَرَأتَ القُرْآنَ لِيُقَالَ : هُوَ قَارِئٌ ؛ فَقَدْ قِيلَ ، ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ في النَّارِ . وَرَجُلٌ وَسَّعَ اللهُ عَلَيْهِ ، وَأعْطاهُ مِنْ أصْنَافِ المَالِ ، فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ ، فَعَرَفَهَا . قَالَ : فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا ؟ قَالَ: مَا تَرَكْتُ مِنْ سَبيلٍ تُحِبُّ أنْ يُنْفَقَ فِيهَا إِلاَّ أنْفَقْتُ فِيهَا لَكَ. قَالَ : كَذَبْتَ ، ولكِنَّكَ فَعَلْتَ لِيُقَالَ : جَوَادٌ ! فَقَدْ قِيلَ ، ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ في النَّارِ )) . رواه مسلم .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Hakika mtu wa kwanza atakaye hukumiwa Siku ya Qiyaamah ni mtu aliyekufa shahidi (vitani). Ataletwa na kuonyeshwa neema zote alizopatiwa, naye atakubali. Ataulizwa: "Ulizitumia vipi neema hizo?" Atajibu: "Nilipigana kwa ajili yako mpaka nikafa." Ataambiwa: "Umesema uwongo, hakika wewe ulipigana ili uitwe: Shujaa! Kwa hakika uliitwa hivyo." Kisha Ataamrisha ashikwe kwenye paji lake la uso, akokotwe mpaka motoni. Mtu mwengine ni yule aliyejifunza elimu na akaifundisha na akaisoma Qur-aan Ataletwa na kuonyeshwa neema zote alizopatiwa, naye atakubali. Ataulizwa na kusoma Qur-aan kwa ajili yako." Ataambiwa: "Umesema uwongo, hakika wewe ulijifunza ili uitwe: Mwanachuoni! Na ulisoma Qur-aan ili uitwe Qaari (msomaji mzuri wa Qur-aan). Kwa hakika uliitwa hivyo." Kisha Ataamrisha ashikwe mpaka atiwe motoni. Na mtu mwengine ni yule aliyepanuliwa na Allaah, na akapatiwa aina zote za mali. Ataletwa na kuonyeshwa neema zote alizopatiwa, naye atakubali. Ataulizwa: "Ulizitumia vipi neema hizo?" Atajibu: "Hakuna njia yoyote ambayo Unapenda itolewe mali kwayo isipokuwa nilitoa kwa ajili yako." Ataambiwa: "Umesema uwongo, lakini wewe ulifanya hivyo ili uitwe: Mtoaji sana! Kwa hakika uliitwa hivyo." Kisha ataamrisha ashikwe mpaka motoni." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أن نَاساً قَالُوا لَهُ : إنَّا نَدْخُلُ عَلَى سَلاَطِيننَا فَنَقُولُ لَهُمْ بِخِلاَفِ مَا نَتَكَلَّمُ إِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِندِْهِمْ ؟ قَالَ ابنُ عُمَرَ رضي الله عنهما : كُنَّا نَعُدُّ هَذَا نِفاقاً عَلَى عَهْدِ رسول الله صلى الله عليه وسلم . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kulikuja watu waliomuuliza: "Hakika sisi tunaingia kwa sultani wetu na kumwambia yeye kinyume na yale tunayozungumza tunapotoka kwake." Akasema: "Hakika sisi tulikuwa tukiona jambo hilo kuwa ni nifaki (unafiki) katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 4

وعن جُندب بن عبد اللهِ بن سفيان رضي الله عنه قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ سَمَّعَ سَمَّعَ الله بِهِ ، وَمَنْ يُرائِي يُرائِي اللهُ بِهِ )) . متفق عَلَيْهِ .

ورواه مسلم أَيضاً من رواية ابن عباس رضي الله عنهما .

Imepokewa kutoka kwake Jundub bin 'Abdillaah bin Sufyaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutaka asikike (kwa lile alilofanya ili watu wamsifu) Allaah Atamfanya asikike kwa hilo (kwa kuonyesha niya yake ya hakika Siku ya Qiyaamah), na yule mwenye kujonyesha, Allaah Atamuonyesha kwa hicho (kuionyesha nia yake halisi, kwa kumdhalilisha)." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Na Muslim ameipokea Hadiyth hii kutokana na riwaayah ya Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa).

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَعَلَّمَ عِلْماً مِمَّا يُبْتَغَى بِهِ وَجْهُ اللهِ عزوجل لاَ يَتَعَلَّمُهُ إِلاَّ لِيُصِيبَ بِهِ عَرَضاً مِنَ الدُّنْيَا ، لَمْ يَجِدْ عَرْفَ الجَنَّةِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) . رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيحٍ 

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kujifunza elimu, ambayo huwa ni kwa ajili ya kupata radhi za Allaah Ta'aalaa, kisha mtu akajifunza si kwa lengo hilo isipokuwa apate mapato ya kidunia hatapata harufu ya Pepo Siku ya Qiyaamah." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

Share