051-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuamini Fali (Mkosi)

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن التَّطَيُّرِ

051-Mlango Wa Kukatazwa Kuamini Fali (Mkosi)

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ عَدْوَى وَلاَ طِيَرَةَ ، وَيُعْجِبُني الفَألُ )) قالُوا : وَمَا الفَألُ ؟ قَالَ : (( كَلِمَةٌ طَيِّبَةٌ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoa kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana magonjwa ya kuambikizwa wala kisirani lakini ninapenda Al-Fa'lu." Akaulizwa: "Al-Fa'lu ni nini?" Akasema: "Neno zuri." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawud na At-Tirmidhiy].

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا عَدْوَى وَلاَ طِيَرَةَ . وإنْ كَانَ الشُّؤمُ في شَيْءٍ فَفِي الدَّارِ ، وَالمَرْأَةِ ، والفَرَسِ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana magonjwa ya kuambukizwa wala kisirani. Ikiwa kungekuwa na mkasi basi ingekuwa katika nyumba, mwanamke na farasi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawud na At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 3

وعن بُريْدَةَ رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ لا يَتَطَيَّرُ . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haamini kabisa mambo ya fali na kisirani." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

Hadiyth – 4

وعن عُروة بن عامر رضي الله عنه قال : ذُكِرَتِ الطِّيَرَةُ عِنْدَ رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فقالَ : (( أحْسَنُهَا الفَألُ . وَلاَ تَرُدُّ مُسْلِماً فإذا رَأى أحَدُكُمْ ما يَكْرَهُ ، فَليْقلْ : اللَّهُمَّ لاَ يَأتِي بِالحَسَناتِ إلاَّ أنْتَ ، وَلاَ يَدْفَعُ السَّيِّئَاتِ إلاَّ أنْتَ ، وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إلاَّ بِكَ )) حديث صحيح رواه أبو داود بإسناد صحيح .

Amesema 'Urwah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Ilitajwa mikosi mbele ya Rasuli wa Alaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akasema: "Iliyo bora zaidi ni Al-fa'ul, na fali haimrudishi nyuma Muislamu, hivyo akiona mmoja wenu linalomchukiza na aseme: 'Allaahumma laa yaatiy bil hasanaati illaa Anta walaa yadfa'u as-sayyi'ati ilaa Anta walaa Hawla walaa Quwwata illa Bika (Ee Rabb Wangu! Jambo zuri haliji ila kutoka Kwako wala hapana wa kuondosha jambo ovu isipokuwa Wewe wala hapana hila wala nguvu isipokuwa kuwezeshwa na wewe'." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh] 

 

Share