057-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kugombana Msikitini, Kunyanyua Sauti Ndani Yake, Kusaka Kitu Kilichopotea, Kuuza, Kununua na Kuajiri na Mfano Wake katika Muamala

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة الخصومة في المسجد ورفع الصوت فِيهِ

ونشد الضالة والبيع والشراء والإجارة ونحوها من المعاملات

057-Mlango Wa Ukaraha wa Kugombana Msikitini, Kunyanyua Sauti Ndani Yake, Kusaka Kitu Kilichopotea, Kuuza, Kununua na Kuajiri na Mfano Wake katika Muamala

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّه سمعَ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( مَنْ سَمِعَ رَجُلاً يَنْشُدُ ضَالَّةً في المَسْجِدِ فَلْيَقُلْ : لاَ رَدَّها اللهُ عَلَيْكَ ، فإنَّ المَسَاجِدَ لَمْ تُبْنَ لِهذَا )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kumsikia mtu yeyote akitafuta kitu kilichopotea Msikitini, amwambie: 'Allaah asikurudishie kitu chako', kwani Misikiti haikujengwa kwa sababu ya hilo." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا رَأيْتُمْ مَنْ يَبِيعُ أَوْ يَبْتَاعُ في المَسْجِدِ ، فَقُولُوا : لا أرْبَحَ اللهُ تِجَارَتَكَ ، وَإِذَا رَأَيْتُمْ مَنْ يَنْشُدُ ضَالَّةً فَقُولُوا : لا رَدَّهَا الله عَلَيْكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Unapomuona mtu anafanya biashara ya kuuza au kununua Msikitini, mwambie: 'Allaah asikupatie faida katika biashara yako.' Na unapomuona mtu anasaka kitu kilichompotea, basi mwambie: 'Allaah asikurudishie kitu chako'." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 3

وعن بُريَدَةَ رضي الله عنه : أنَّ رَجُلاً نَشَدَ في المَسْجِدِ فَقَالَ : مَنْ دَعَا إِلَى الجَمَلِ الأَحْمَرِ ؟ فَقَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لا وَجَدْتَ ؛ إنَّمَا بُنِيَتِ المََسَاجِدُ لِمَا بُنِيَتْ لَهُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akitangaza ndani ya Msikiti kwa kusema: "Ni nani aliyemuita ngamia mwekundu?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Heri usimpate, hakika Msikiti imejengwa kwa lengo iliyo jengewa." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جدِّهِ رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَن الشِّراءِ والبَيْعِ في المَسْجِدِ ، وَأنْ تُنْشَدَ فِيهِ ضَالَّةٌ ؛ أَوْ يُنْشَدَ فِيهِ شِعْرٌ . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Shu'ayb kutoka kwa babake, kutoka kwa babu yake (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kununua na kuuza Msikitini na kusaka ndani yake kitu kilichopotea au kuimbwa ndani yake mashairi. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 5

وعن السائبِ بن يزيد الصحابي رضي الله عنه قَالَ : كُنْتُ في المَسْجِدِ فَحَصَبَنِي رَجُلٌ ، فَنَظَرْتُ فَإذَا عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه فَقَالَ : اذْهَبْ فَأتِنِي بِهذَينِ ، فَجِئْتُهُ بِهِمَا ، فَقَالَ : مِنْ أيْنَ أَنْتُمَا ؟ فَقَالاَ : مِنْ أهْلِ الطَّائِفِ ، فَقَالَ : لَوْ كُنْتُمَا مِنْ أهْلِ البَلَدِ ، لأَوْجَعْتُكُمَا ، تَرْفَعَانِ أصْوَاتَكُمَا في مَسْجِدِ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ! رواه البخاري .

Amesema Saaib bin Yaziyd, ambaye ni Swahaaba (Radhiwya Allaahu 'anhu): Nilikuwa Msikitini, mara mtu mmoja akanipiga mimi kwa kijiwe. Nikamuangalia na kumuona kuwa ni 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu), naye akaniambia: "Nenda ukaniletee wale watu wawili." Nikaja nao kwake, naye akawauliza: "Nyinyi munatoka wapi?" Wakasema: "Sisi ni watu wa Twaaif." Akawambia: "Lau mungekuwa ni watu wa mji huu (yaani Madiynah) ningewaadhibu, kwani nyinyi munanyanyua sauti zenu katika Msikiti wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Al-Bukhaariy].

 

 

Share