060-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa kwa Anayetaka Kuchinja Kukata Nywele au Kucha Zake Mpaka Achinje Pindi Linapoingia Kumi la Kwanza la Dhul Hijjah

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب نهي من دخل عَلَيْهِ عشر ذي الحجة

وأراد أنْ يضحي عن أخذ شيء من شعره أَوْ أظفاره حَتَّى يضحّي

060-Mlango Wa Kukatazwa kwa Anayetaka Kuchinja Kukata Nywele au Kucha Zake Mpaka Achinje Pindi Linapoingia Kumi la Kwanza la Dhul Hijjah

 

Alhidaaya.com

 

عن أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ كَانَ لَهُ ذِبْحٌ يَذْبَحُهُ ، فَإذَا أَهَلَّ هِلاَلُ ذِي الحِجَّةِ ، فَلاَ يَأخُذَنَّ من شَعْرِهِ وَلاَ مِنْ أظْفَارِهِ شَيْئاً حَتَّى يُضَحِّيَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Umm Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuwa na mnyama anayetaka kumchinja (siku ya Iydul Adhha), basi ajizuwie kukata nywele na kucha zake pindi unapoandama mwezi wa Dhul Hijjah mpaka achinje." [Muslim]

 

 

Share