090-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kupita Mbele ya Wenye Kuswali

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم المرور بَيْنَ يدي المصلِّي

090-Mlango Wa Uharamu wa Kupita Mbele ya Wenye Kuswali

 

Alhidaaya.com

 

عن أَبي الجُهَيْمِ عبد اللهِ بن الحارِثِ بن الصِّمَّةِ الأنْصَارِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لَوْ يَعْلَمُ المَارُّ بَيْنَ يَدَيِ المُصَلِّي مَاذَا عَلَيْهِ لَكَانَ أنْ يَقِفَ أرْبَعِينَ خَيْراً لَهُ مِنْ أنْ يَمُرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ )) قَالَ الراوي : لا أدْرِي قَالَ : أرْبَعينَ يَوماً ، أَوْ أرْبَعِينَ شَهْراً ، أَوْ أرْبَعِينَ سَنَةً .متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abil Juhaym 'Abdillaah bin Al-Haarith bin Asw-Swimmah Al-Answariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)amesema: "Lau ungejua madhambi anayopata mwenye kupita mbele ya mtu anayeswali basi ingekuwa ni bora kwake kusimama arobaini kuliko kupita mbele yake." Amesema mpokezi wa Hadiyth hii: "Sina hakika alisema siku arobaini au miezi arobaini au miaka arobaini." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy] 

 

 

Share